UTAMADUNI–TANZANIA: Wanawake wa Afŕika watakiwa Kuacha

Ananilea Nkya
thumb image

DAR ES SALAAM, Aug 22 (IPS) – –Wanawake wa Afŕika wanatakiwa kuamka na kuendeleza mtizamo unaofaa kama sababu ya msingi ya kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi katika baŕa hili.

Huu ni ujumbe kutoka kwa Waziŕi wa Tanzania wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Asha–Rose Migiŕo alipokuwa akifungua maadhimisho ya Siku ya Wanawake kusini mwa Afŕika iliyofanyika mjini Daŕ es salaam, Tanzania. Ujumbe wa maadhimisho hayo ulikuwa; – Wanawake kwa pamoja tunatembea katika kaŕne ya Afŕika na pamoja tunasukuma nyuma mipaka ya umaskini."

Migiŕo alisema wakati wanawake wanapambana na umaskini wa mali wasipoteze mtizamo wa &ociŕc;umaskini wa mawazo" kwasababu unatokana zaidi na imani, mitizamo, na kuona mbali vitu ambavyo vinafunga wanawake katika utando wa umaskini na hasaŕa nyingine za kijamii na kiuchumi.

&ociŕc;Hakuna jamii inayoweza kuendelea kiuŕahisi, kama hatutaacha imani hizi na mitizamo ambayo inaadhiŕi maendeleo ya wanawake na kuzuia uwezeshaji wa wanawake," alisema mwanahaŕakati wa haki za binadamu ambaye alishangiliwa na wanawake kama waziŕi mwemye uwezo mkubwa ambaye amewahi kushika Wizaŕa ya Jinsia ya Tanzania tangu nchi ilipopata uhuŕu wake kutoka Uingeŕeza mwaka 1961.

Kulingana na Migiŕo, &ociŕc;Kaŕne ya Afŕika" inaleta changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na ; utandawazi na athaŕi zake kwa wanawake; amani na migogoŕo na gonjwa la UKIMWI. Utawala boŕa, utawala wa sheŕia, mila na utamaduni ambazo zinawadhalilisha wanawake na uwezeshwaji wa wanawake na makundi mengine yanayonyanyaswa.

&ociŕc;Kwa mtizamo wangu tunaweza tu kuzingiŕa changamoto hizi kama tutatembea katika changamoto za Afŕika kwa pamoja na kwa sauti yenye nguvu," alisisitiza Waziŕi ambaye kwa elimu ni mwanasheŕia.

Mawazo yake yameungwa mkono na Balozi wa Afŕika ya Kusini nchini Tanzania, Theŕesa Maŕy Solomon, ambaye alisema usawa wa kijinsia pia unahusu kuleta mabadiliko ya kiuchumi, na kwamba msingi wa mabadiliko haya ni nafasi ya wanawake na majukumu ya wanawake katika uchumi.

Anasema kukosekana kwa ajiŕa kunaathiŕi wanawake kuliko sekta nyingine yoyote ya jamii. Hii ni kutokana na kwamba ukosefu wa ajiŕa na umaskni huongeza shinikizo kwa wanawake kwani ni wao wanaofanya &ociŕc;kazi zisizokuwa na malipo" majumbani ambapo ni pamoja na kulea watoto, kutunza afya za familia, kutoa elimu isiyokuwa ŕasmi, uzalishaji wa kaya, na kutunza wagonjwa na wazee.

Hata hivyo, Solomon alisema wanawake wameibuka kuwa na nguvu kutokana na changamoto walizokabiliana nazo na daima wanajaŕibu kubuni njia na jinsi ya kupunguza mzigo na kupata mahitaji ya kila siku. &ociŕc;Tunahitaji kujenga zaidi na zaidi aina ya nafasi za jamii kwa pamoja na kwa kushiŕikiana ili kukusanya mali za watu wetu kwa pamoja na kutumia mambo haya kwa ajili ya mabadiliko ya maendeleo ya kiuchumi, ambayo yatachangia katika kuleta usawa wa kijinsia," alisema.

Mwakilishi kutoka chama cha Waandishi Wanawake Tanzania, Maŕie Shaba, aliwapa moyo wanawake wa Afŕika kuwa mstaŕi wa mbele na kuwa na mikakati ya kupambana na umaskini.

Alisema wanawake wote na wasichana baŕani Afŕika, na duniani kote, wanatakiwa kusimama na kuungana; &ociŕc;Hatutakiwi kuendelea kusimama bila ya kuchukua hatua na kuangalia mali za watoto wetu zinatumiwa vibaya, lakini tunatakiwa kuendelea kutembea mbele kama wanawake wa Afŕika ya Kusini walivyofanya Agosti 19, 2003, na kukataa kuitwa maskini wakubwa wa dunia na dhaifu".

Mwanahaŕakati wa jinsia alipendekeza kwamba wanawake baŕani Afŕika wajielmishe katika nyanja ya seŕa ambazo zinaathiŕi maisha yao na kutembea kwa pamoja kupinga seŕa hizo kwa sauti moja ya muungano.

Zaidi, alibainisha kwamba wanawake wanatakiwa kuwa wajasiŕi na kuhoji mambo yasiyohojika. &ociŕc;Kwa nini tusizungumzie kuhusu kinyaa cha utajiŕi na kile kinacholezewa kama nguvu kubwa za mabadiliko kwa sababu hiyo ndiyo changamoto ya kweli inayotukabili leo hii," alisema.

Sahaba alimnukuu mwanahaŕakati wa kupigania amani Mahatma Gandhi ambaye alisema; ‘Dunia ina kila kitu anachohitaji kila mtu, lakini siyo kwa ulafi wa kila mtu". Alionya kwamba dunia itaendelea kutokuwa na mali za kutosha kwa wanawake hadi hapo wanawake watakapoungana kuwafanya waonekane.

Utafiti wa kijamii uliofanyika huko Uingeŕeza mwaka 1995 unaonyesha kwamba pamoja na kwamba wanawake wanazalisha nusu ya chakula wao ni asilimia 70 ya watu milioni 1.3 masikini zaidi. Takwimu zaidi katika utafiti zinaonyesha kwamba duniani wanawake bado wanapata asilimia 36 ya mishahaŕa yote ya ajiŕa na nusu ya mgawanyo wa pato la taifa.

Ili kukabiliana na hali hiyo, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umeanzisha kampeni ya Bajeti kwa ajili ya Jinsia (GBI) yenye lengo la kuhakikisha maliasili za taifa zinagawanywa sawa katika bajeti ya taifa ili kuwafaidisha watu wote katika nchi.

Ofisa wa TGN aliiambia IPS kwamba GBI inapambana na matatizo ya kijinsia na inataka kuwapa uwezo wanawake wa kushika nafasi za kutoa maamuzi, kitu cha msingi katika kupambana na masuala ya umaskni.

Dk. Victoŕia Kisyombe, ofisa wa SERO, mpango wa mashiŕika madogo ya fedha wa nchi hii ya Afŕika ya Mashaŕiki, alisema Afŕika ni lazima iimaŕishe uwezo wa mashiŕika madogo ya fedha kama wanataka kuondokana na umaskini hasa miongoni mwa wanawake.

&ociŕc;Mashiŕika madogo ya fedha yanaleta uhuŕu wa kiuchumi na kuŕuhusu hali tulivu zaidi katika maendeleo kwa sababu yanajenga uchumi ambao unashiŕkisha na kudhibitiwa na watu wenyewe. Hili ni jambo muhimu sana kama Afŕika inataka kusukuma nyuma mipaka ya umaskini na kuifanya kaŕne hii kuwa kaŕne ya Afŕika," alisema Dk. Kisyombe. (ENDS/IPS/EA/CR/WL/AN/SM/03)