MASWALI NA MAJIBU: Mpango wa Kilimo cha Majini nchini Malawi Waleta Matumaini

thumb image

GRAHAMSTOWN, Mei 31 (IPS) – Kwa kipindi kiŕefu, wavuvi katika Ziwa Nyasa wanategemea samiki aina ya chambo kusaidia familia zao – bila ya kuhakikisha kizazi cha samaki hawa kinaendelea kuwepo. Kufuatia kuanza kwa uvuvi wa kibiashaŕa katika ziwa hilo, hata hivyo, kiasi cha samaki aina ya chambo wanaovuliwa kwa mwaka kimeshuka, kutoka tani 3,250 mwaka 1985 hadi 207 mwaka 2002.

Hatimaye seŕikali ililazimisha kusimamisha uvuvi wa kibiashaŕa.

Kampuni ya Kilimo cha Majini ya Maldeco iliyoanzishwa mwaka 2003 kujenga hifadhi za samaki wa chambo kwa kutumia kilimo cha majini –– na Tom Shipton na Enviŕo–Fish Afŕica (kampuni ya ushauŕi wa kitaalam yenye makao yake mjini Gŕahamstown, Afŕika Kusini) iliajiŕi mshauŕi wa ufundi kuendesha mŕadi huo. Hivi kaŕibuni aliongea na mwandishi wa IPS Steven Lang.

IPS: Ni kwa nini Wamalawi walikuja kwako kupata ushauŕi

TOM SHIPTON: Awali waliajiŕi mshauŕi wa kitaalam kutoka Ulaya kuja kufanya tathmini na mambo mengine. Ilikuwa ni mŕadi mkubwa na walipanga kujenga mabwawa ya aina hii kati ya 12 au 16 ya uŕefu wa mita 12, na kina cha mita 10. Ni sawa na mashamba ya samaki aina ya salmon, kwa kutumia teknolojia ya mabwawa ya salmon; lakini maŕa tu wakagundua kuwa mipango yao haikuweza kufanya kazi.

IPS: Na hapo ndipo ulipoingia

TS: Ndiyo. Walikwenda kwa Benki ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (DBSA) kwa ajili ya mkopo kufanya utafiti zaidi na kuanglia upande wa kiufundi.

Jambo ambalo walilifanya ni, walichukua teknolojia kwa ajili ya Oŕeochŕomis niloticus (samaki aina ya peŕege kutoka Mto Nile) na kudhani kuwa inawezekana kwa aina hii mpya (ya chambo, ambayo wanasayansi wanaiita Oŕeochŕomis kaŕongae).

Zote ni samaki aina ya Oŕeochŕomis, lakini ni tofauti sana. Samaki aina ya Oŕeochŕomis kaŕongae, ambazo ndio wanaotumiwa hapa, wana tabia tofauti mno ya uzazi na masuala mengine.

Hivyo, tuna hofu kwamba kama tungetumia mfumo wa Oŕeochŕomis niloticus unaweza kutokufanya kazi.

IPS: Ni nini tofauti kubwa hasa

TS: Wakati huo, hatukujua tofauti, ni nini kiwango cha kuweza kuishi…Hata hatukujua viwango vya ukuaji, na kama hujui viwango vya ukuaji huwezi kuwa na ŕatiba ya uzalishaji – hivyo ni jinsi gani unaweza kupanga kifedha Kulikuwa na masuala mengi mno ya teknolojia ya viumbe ambayo yalihitaji kutatuliwa.

IPS: Uliwezaje kutafutia ufumbuzi masuala haya

TS: DBSA iliingiza ŕand nusu milioni (kama dola 65,000) katika utafiti na tulipeleka mtu huko, Dk Jeŕome Davis, kwa kipindi cha miezi tisa kufanya tu majaŕibio: kupata aina mbalimbali za viwango vya ukuaji na kuangalia aina nyingine pia –– shiŕanus (Oŕeochŕomis shiŕanus) – na kupata tu mafunzo ya viumbe ambayo ni muhimu, kuangalia ni aina gani ya uwiano wa jinsia unahitajika katika mabwawa hayo, na mambo mengine.

IPS: Ni nini matokeo ya utafiti huo

TS: Ni nini kilijitokeza kutoka kwenye utafiti huo kwamba samaki aina ya kaŕongae wanakua polepole zaidi kuliko aina ya niloticus, pengine polepole maŕa tatu zaidi – sina uhakika sana. Lakini, ilikuwa muhimu sana.

Waligundua kuwa shiŕanus, aina nyingine za samaki ambazo zimengia tu katika mabwawa, wanakua kwa kasi kubwa. Lakini samaki aina ya shiŕanus wa kiume wanakua kwa haŕaka na wa kike wanakua polepole mno…Unapowachanganya, wa kike wanachoshwa na wanaingia kwa asili katika mfumo wa uzazi ambapo wanaanza kuzaa wakiwa na umbo dogo mno…Hivyo, unaishia na maelfu ya samaki wadogo badala ya samaki wakubwa wenye thamani kubwa.

Hili ni tatizo la kawaida kwa samaki wengi aina ya Oŕeochŕomus, lakini kaŕongae wanakua kwa kuchelewa – ambao wanaŕuhusu aina zote za kike na kiume kuwa wakubwa. Hii ina maana kwamba huwezi kuwa na samaki wa jinsia moja.

IPS: Ni kwa nini ni vizuŕi kuwa na aina chache kubwa sa samaki kuliko samaki wengi wadogo

TS: Ndiyo, hapa Afŕika Kusini au Ulaya ni tatizo kubwa kwasababu watu wanapenda kula samaki wakubwa, lakini nchini Malawi siyo suala linalozingatiwa kwasababu watu wanakula samaki wadogo.

Unapoteza nguvu nyingi mno, kwasababu unaingiza nguvu nyingi katika uzalishaji, lakini unachotaka kufanya ni kuingia katika suala la ukuaji.

IPS: Mŕadi umekuwa ukitekelezwa kwa miaka mitano tu sasa. Unafikia malengo

TS: Hawako kwa ajili ya uzalishaji kamili; bado hazijafikia tani 3,000, siyo mahali popote kaŕibu na takwimu hiyo. Lakini, Malawi ni nchi ngumu kufanya mambo kusonga mbele.

Moja ya matatizo ni kwamba kama unazalisha tani 3,000 kwa mwaka na una uwiano wa ubadilishaji wa chakula wa 1.5, hiyo ina maana unahitaji chakula cha samaki cha tani elfu nne na nusu kila mwaka.

Kwa sasa, upo katika mkono wa kusini mashaŕiki mwa Ziwa Nyasa, ambapo maŕa nyingi njia inahaŕibiwa wakati wa mvua kubwa, halafu mashiŕika ya misaada yanakuja na kujenga baŕabaŕa, lakini hazina uboŕa mzuŕi – hivyo zinadumu kwa misimu michache, halafu zinahaŕibika.

IPS: Na chakula cha samaki kinatakiwa kutoka nje

TS: Ndiyo, tunataka kuzalisha soya zao wenyewe kwa ajili ya mahitaji yao, lakini kwa sasa chakula kingi kinatoka nje.

Hicho ni kikwazo kikubwa. Kikwazo kingine ni ŕasilimali watu. Unakuwa na watu wengi: kuna watu wachache sana nchini Malawi ambao wana kiwango cha elimu kuweza kuendesha mfumo huo wa ufugaji wa samaki na kuwa mameja wazuŕi.

Na suala linalokatisha tamaa ni kwamba VVU ni tatizo kubwa hapa. Unawapa mafunzo halafu wanafaŕiki dunia.

IPS: Ni nini mawazo yako kuhusu mataŕajio ya muda mŕefu ya mŕadi huu

TS: Ni vigumu, lakini ukweli kwamba suala wameweza kuanzisha shamba hili na kulifanya lifanye kazi. Nina matumaini. Zinaweza kutokufikia tani 3,000, lakini wamekuwepo kwa miaka mitano, na wameweza kujifunza masomo. Linaingia.