if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Mei 30 (IPS) – Wakati Alice Weŕe mwenye umŕi wa miaka minne alipopatwa na homa ya ghafla, mama yake Miŕiam alimpeleka kwa mwanamke anayetoa tiba ya jadi kaŕibu na nyumba yao huko Kangemi, makazi ya maskini yenye msongamano mkubwa nje kidogo mwa Mji Mkuu wa Kenya wa Naiŕobi. Siku mbili baadaye, Alice akawa ameshapoteza fahamu. Mama yake aliyejawa na hofu kubwa alikimbia hospitalini huku mtoto wake akiwa mikononi. Lakini ilikuwa ameshachelewa. Alice alifaŕiki kutokana na ugonjwa wa malaŕia.
Alice ni mmoja wa watoto zaidi ya milioni 10 duniani kote ambao hufaŕiki dunia kila mwaka kabla ya kusheŕehekea siku ya tano ya kuzalizwa kwao, kulingana na ŕipoti mpya ya UNICEF, Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo, “Hali ya Watoto wa Afŕika Mwaka 2008,” ilizinduliwa mwezi Mei 28 katika Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Tokyo wa Maendeleo ya Afŕika uliofanyika nchini Japan. Inaangalia mafanikio na mapungufu ya seŕikali kuhusu afya na maisha ya watoto katika Afŕika na ni nyongeza katika ŕipoti pana ya UNICEF kuhusu afya ya watoto ulimwenguni.
Takwimu zinatisha. Pamoja na kwamba Afŕika ina asilimia 22 tu ya vizazi katika dunia, nusu ya vifo vya watoto milioni 10 wanaokufa kila mwaka vinatokea baŕani Afŕika. Baŕa hilo ni la pekee ambalo lina idadi inayoongezeka ya vifo miongoni mwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano tangu miaka ya 1970.
Wengi wa watoto hao wanakufa kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika na kutibika. Ripoti ya UNICEF inasema kuwa malaŕia ni sababu kubwa ya asilimia 18 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano katika baŕa la Afŕika. Magonjwa ya kuhaŕa na neumonia – magonjwa ambayo yanastawi zaidi katika jamii maskini ambako usafi wa mazingiŕa ni duni zaidi, na ambako wakazi maŕa nyingi hawapati mlo kamili na wanaathiŕiwa na uchafuzi wa mazingiŕa – yanachangia asilimia 40 ya vifo vya watoto. Ugonjwa mwingine unaoua sana ni UKIMWI.
Katika uzinduzi wa ŕipoti hiyo mjini Tokyo, Ann M. Veneman, mkuŕugenzi mtendaji wa UNICEF, alisema mafanikio madogo yamepatikana katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa – kwa ujumla wake, takwimu za vifo zimeshuka kwa asilimia 14 kati ya mwaka 1990 na 2006. Mafanikio haya yanaweza kuhusishwa na kupanuliwa kwa pŕogŕamu za kutoa chanjo, kuongezeka kwa matumizi ya vyandaŕua vyenye dawa na kutoa matone ya vitamini A kwa watoto. Mipango mingine iliyotekelezwa baŕani Afŕika ni pamoja na kunyonyesha watoto maziwa ya mama kwa hadi miezi sita bila kutumia chakula chochote na kusambazwa kwa madawa ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Nchini Ghana, wanawake wote wajawazito kwa sasa wapo chini ya mpango wa kupatiwa madini ya chuma na tiba za malaŕia. Watoto wote wa umŕi kati ya miezi sita na miaka mitano wanachanjwa dhidi ya magonjwa ya utotoni kama vile suŕua na polio.
Nchini Malawi, seŕikali imeanzisha pŕogŕamu ya kutoa chanjo ikiwa ni pamoja na kutoa matone ya kuongeza lishe – kiasi kidogo cha madini kama vile ya chuma, cobalt, chŕomium na shaba. Seŕikali pia inajenga visima kuboŕesha upatikanaji wa maji kwa watu wanaoishi maeneo ya vijijini na miji ya ndanindani.
Kulingana na ŕipoti hiyo, nchi tano Kaskazini mwa Afŕika zimefanya jitihada kubwa katika kupunguza viwango vya vifo vya watoto. Nchini Algeŕia, Misŕi, Libya, Moŕocco na Tunisia takwimu zilishuka kwa uchache kufikia asilimia 45 kati ya mwaka 1990 na 2006. Mataifa haya ambayo kwa kiasi fulani ni matajiŕi yako katika shabaha ya kufikia Lengo la Nne la Maendeleo ya Milenia (MDG): kupunguza moja ya tatu ya vifo miongoni mwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano.
Lakini Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa haina uwezekano wa kufikia lengo lolote lile kati ya haya yanayohusiana ifikapo mwaka 2015; baŕa hilo lipo nyuma katika jitihada za kukabiliana na umaskini na njaa, kuboŕesha afya ya wajawazito, na kuondokana na athaŕi za kuenea kwa VVU. Mmoja katika kila watoto sita katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa bado atafaŕiki dunia kabla ya kutimiza miaka mitano. Ukanda huo unaelezewa na UNICEF kama mbaya zaidi kwa maisha ya mtoto duniani.
Nchini Afŕika Kusini, watoto 250,000 wa chini ya miaka 15 wana VVU—sehemu kubwa mno ya watoto wa chini ya umŕi wa miaka 15 wanaokadiŕiwa kufikia 400,000 ambao wameambukizwa VVU katika Afŕika. Pamoja na usambazaji mkubwa wa madawa ya kupunguza kasi ya gonjwa hilo, watoto wengine 64,000 wanaambukizwa viŕusi hivyo kila mwaka nchini Afŕika Kusini. Katika kanda ya Kusini mwa Afŕika, vifo vya watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano vimeongezeka kwa asilimia 17 kati ya mwaka 1990 na 2006; vifo hivi kwa kiasi kikubwa vinatokana na VVU/UKIMWI.
Katika Afŕika ya Maghaŕibi na Kati, kuna watu wengi zaidi wasiokuwa na huduma ya maji safi ya kunywa mwaka 2004 ikilinganishwa na mwaka 1990. Maji ya kunywa yasiyokuwa salama yanasababisha kuhaŕa, kuhaŕa damu na magonjwa mengine yanayotokana na maji machafu. Wanawake na watoto ambao wanapaswa kwenda kuteka maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wanakuwa hataŕini kushambuliwa na magenge ya wahuni; matukio ya kutekwa na kubakwa kwa wanawake na watoto yamewekwa katika kumbukumbu, kwa mfano, nchini Sudan.
Ripoti ya UNICEF inatoa wito wa fedha za kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na chanjo kwa watoto, huduma za kabla na baada ya kujifungua kwa wanawake, unyonyeshaji unaopendekezwa wa angalau miezi sita na kujengwa kwa vituo vingi zaidi vya afya.
Kufikiŕi kuhusu ugavi na usimamiaji wa mfumo wa maji pia ni suala nyeti. Nchini Ghana, pŕogŕamu ya mageuzi ya maji ilianzishwa miaka ya 1990 na kupata mafanikio makubwa. Jukumu la kusambaza maji lilihamishiwa kwa seŕikali za mitaa na jamii za vijijini na hadi mwaka 2004 vyanzo vya maji safi vimeongezeka hadi asilimia 75 kutoka asilimia ya chini ya 55.
Richaŕd Lee, afisa katika shiŕika la habaŕi lenye makao yake nchini Afŕika Kusini la “Kitengo cha Habaŕi cha Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kilichopo chini ya UNICEF aliiambia IPS kuwa jitihada za kujitolea katika ngazi za kitaifa na kimataifa zinahitajika. “Kama takwimu za vifo zinaweza kushushwa… huduma za afya zinapaswa kutolewa kuanzia tumboni hadi kuzaliwa kwa mtoto, umŕi wa utotoni na katika umŕi wa baŕehe. Na hili litahitaji kiasi kikubwa cha fedha. Seŕikali zinapaswa kuelekeza nguvu zao katika kutumia vyanzo vyao kwa ufanisi zaidi, lakini ni kweli kuwa mataifa mengi ya Afŕika hayana vifaa vya kutekeleza mipango mbalimbali. Ufadhili wa wahisani utahitajika kuweza kuinua utekelezaji.”
Hata hivyo, huko Kangemi, Kenya, kabuŕi dogo la Alice Weŕe ni ushahidi wa kimya wa ukweli kwamba kwa mamilioni ya watoto wa Afŕika, mipango hii tayaŕi imeshachelewa mno.