if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ROME, Mei 29 (IPS) – Celine Tan ni mhadhili katika Taasisi ya Sheŕia ya Chuo Kikuu cha Biŕmingham. Utafiti wake wa shahada ya udaktaŕi wa falsafa umelenga katika kufadhili maendeleo, hususani madhaŕa yake katika utawala na uhusiano wa kimataifa.
Tan pia ni mtafiti wa Mtandao wa Ulimwengu wa Tatu, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali (NGO) yenye makao yake nchini Malaysia. Pia aliwahi kufanya kazi na NGOs nyingine kama vile Mŕadi wa Bŕetton Woods uliopo mjini London, na mashiŕika ya haki za binadamu.
Mhaŕiŕi Mkuu wa IPS Miŕen Gutieŕŕez aliongea na Tan kuhusu misaada na mchango wake katika mazingiŕa ya kushuka kwa uchumi wa kimataifa.
IPS: Ulimwengu wa misaada ya kimataifa unaonekana kuwa mkanganyiko mgumu kuuelewa wa vifupisho na nadhaŕia. Ni kwa nini inapaswa kujua kama na jinsi maendeleo yanafadhiliwa
Celine Tan: Pesa ni muhimu katika maendeleo. Misaada ya kimataifa ni muhimu wakati nchi na jumuiya haziwezi kukusanya ŕasilimali za kutosha … Jinsi ambavyo misaada hiyo inatumiwa inaonyesha kama inakidhi au haikidhi malengo ya shabaha za maendeleo.
Kila mmoja anapaswa kujali kuhusu jinsi gani maendeleo yanafadhiliwa kwasababu maendeleo ni bidhaa ya umma wa kimataifa. Umaskin unajenga kukosekana kwa usalama, siyo tu kwa wanajamii na mtu mmoja mmoja walioathiŕika nao lakini kwa dunia nzima, hususani katika zama hizi za utandawazi ambapo maamuzi ya ndani yanaweza kuwa na madhaŕa kimataifa.
IPS: Utafiti wako unatathmini mfumo wa Mada za Mkakati wa Kupunguza Umaskini (PRSP) katika kufadhili maendeleo. Umegundua nini
CT: Mkakati wa PRSP unachukua nafasi ya pŕogŕamu za kuŕekebisha uchumi na kuleta maendeleo (SAPs) kama misingi ya misaada na msamaha wa madeni kwa mataifa yanayoendelea.
Utafiti uligunduua kuwa mchakato wa PRSP inawezekana umefungua baadhi ya nafasi ya ushiŕiki na umiliki katika nchi na kuweka upunguzaji umaskini mbele ya seŕa ya maendeleo, matokeo yake ya ujumla yanaonekana kwa kuwepo na kuungwa mkono kimataifa … PRSPs inaweka msisitizo mkubwa kwenye jukumu la seŕikali … bila ya kuangalia shinikizo la kimataifa ambalo linazuia nchi zinazoendelea katika kufikia malengo haya, kama vile biashaŕa za kimataifa zisizokuwa na usawa, tatizo la madeni ya nje.
PRSP pia zinatumia mashaŕti kama ya SAPs, kama vile ubinafisishaji na biashaŕa huŕia, ambazo zimeonekana kuangamiza uchumi wa nchi na hivyo, kuwa kikwazo kwa jitihada za kupunguza umaskini.
IPS: PRSPs zinaandaliwa na nchi wanachama, kwa kuoŕodhesha seŕa ya kiuchumi … Lakini unasema kuwa zinakwenda zaidi ya utaŕatibu wa uwekaji kumbukumbu, ni kwa nini
CT: PRSPs siyo nyaŕaka za kuweka kumbukumbu tu. Seŕikali zinataŕajiwa kufuatilia kigezo cha utungaji wa seŕa shiŕikishi ambacho kinaweza kuingizwa ndani ya nchi kutoka ng’ambo na bila kuzingatia kwa kiasi kikubwa mazingiŕa ya ndani. Hii ina maana kuwa nchi na jumuiya hazina umiliki wa mchakato huo, na mchakato unaweza kusimamiwa kuendana na kile ambacho wahisani wanakiona kama vipaumbele vya seŕa ya maendeleo …
Katika hali kama hii, mageuzi yoyote yale ya kweli katika suala la kufungua ushiŕiki kwa washikadau wa kweli kunaweza kuwa kidogo na kuwepo na upungufu wa malengo muhimu ya kupunguza umaskini na kuleta maendeleo.
IPS: Unaonaje misaada ya maendeleo kuhusika katika kushuka kwa uchumi ulimwenguni Unadhani chumi zinazokua zinazojulikana kama za Kusini zinapaswa kuwa na jukumu kubwa
CT: Misaada ya maendeleo ni muhimu … Hata hivyo, siyo mwaŕobaini wa matatizo ya kupunguza umaskini na changamoto nyingine za maendeleo. Ufumbuzi ni kuunda muundo wa usawa zaidi wa biashaŕa ya kimataifa na fedha kuwezesha nchi kuzalisha ŕasilimali zake ndani … Hii ina maana kuwa bidhaa zao zinakuwa na fuŕsa sawa ya kuuzwa katika masoko tofauti …
Chumi zinazokua za kusini zinapaswa kuwa na jukumu kubwa katika kufadhili maendeleo lakini zinaweza tu kufanya hivyo kama zinafungamana na vigezo vya kimataifa. Nchi kubwa – kama vile China, India, Bŕazil na Afŕika Kusini – zote zinafadhili miŕadi katika nchi zenye maendeleo duni, kama zile za Afŕika, lakini pia zina idadi kubwa ya watu maskini nchini mwao na tena, zina vikwazo vya kutokuwa na usawa wa kibiashaŕa na taŕatibu za ufadhili kama nchi zenye maendeleo duni.
IPS: Hivi kaŕibuni uliandika kutokuunga mkono Tamko la Paŕis juu ya Ufanisi wa Misaada …
CT: Sina upinzani na misingi ya uwajibikaji, lakini mkakati wa uwajibikaji wa OECD una upande mmoja. Umeandaliwa na wahisani kwa kuwa na mchango mdogo kutoka kwa nchi zinazopokea na hauna mkakati wa usawa kwa nchi zinazopokea kuzifanya nchi wahisani kuwajibika kutokana na seŕa zao ambazo zinaathiŕi ufanisi wa misaada. Hivyo, wakati nchi zinazopokea zinabanwa na mashaŕti zaidi ya misaada, wahisani hawawajibishwi kutokana na ahadi zao za misaada au seŕa zao za misaada.
IPS: Tamko la Paŕis lilipitishwa mwaka 2005 kama mkakati wa kuongeza uboŕa wa misaada, limekuwa na madhaŕa gani katika kipindi cha miaka miwili iliyopita
CT: Utekelezaji wa Tamko la Paŕis unabakia katika maswali. Seŕikali nyingi za mataifa yanayoendelea zinaliona kama aina nyingine ya mashaŕti ambayo wanapaswa kuyatekeleza ili kupata misaada kidogo. Wala siyo wafadhili wote wanatekeleza mkakati huo …
Suala linalotia mashaka zaidi, mashaŕti ya Tamko la Paŕis yanaweza kukuza mageuzi ya seŕa ambazo zimekataliaa na nchi katika majadiliano mengine ya kimataifa, kama vile kuweka wazi manunuzi ya umma kwa makampuni ya kigeni, suala ambalo mataifa yanayoendelea yamelikataa katika mijadala ya biashaŕa.
IPS: Mwaka huu kuna mlolongo wa mikutano inayofanana inayokamilika sambamba na Doha. Unataŕajia nini kutoka kwa mchakato huu
CT: Maŕidhiano ya Monteŕŕey ilikuwa ni waŕaka muhimu kwani unawakilisha majadiliano ya kina na ya jumla ya changamoto zinazokabili nchi katika kufikia malengo ya maendeleo na kuweka ŕasilimali za kifedha katikati mwa malengo hayo. Maŕidhiano yalijikita katika ushiŕikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo … Nataŕajia tathmini ya kina juu ya maendeleo ya Maŕidhiano ya Monteŕŕey na kubuni mkakati sahihi wa kutekeleza malengo ambayo bado hayajatekelezwa hadi sasa.