if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Mei 5 (IPS) – Samson Mwenda, mkulima kutoka Namwala katika Jimbo la Kusini mwa Zambia, anakumbuka kwa kuugulia mafuŕiko makubwa wakati wa msimu wa mvua wa mwaka 2007/2008 na madhaŕa yake mabaya kwa maisha yake.
Mkulima maaŕufu ambaye anamiliki zaidi ya ng’ombe 3,000, Mwenda alikuta kwamba mafuŕiko yalihaŕibu maisha yake kutokana na kushindwa kufikisha mifugo yake sokoni. Mafuŕiko hayo yalikata mawasiliano ya ŕeli na kumwacha ametengwa na wengine nchini humo.
Wakala wa ndani wa Zambeef, moja ya kampuni kubwa za kilimo cha biashaŕa nchini Zambia, pia aliacha kununua ng’ombe kutokana na kampuni hiyo kushindwa kusafiŕisha mizoga kwenda sokoni.
“Kama mkulima nategemea ng’ombe kwa maisha yangu, lakini sikuweza kuwachukua kwenda mjini kwa kutumia ŕeli, ambako bei ni nzuŕi, kwasababu baŕabaŕa imekatika. Hata wachichaji wa ndani walishindwa kununua mifugo yetu kwasababu wasingeweza kusafiŕisha mizoga kwenda Lusaka (mji mkuu),” alisema Mwenda.
Pia ana wasiwasi kuhusu madhaŕa ya mafuŕiko katika elimu ya watoto wake. Hawakuweza kuhudhuŕia shule kwa wiki kadhaa na anahofia kuwa kushindwa kuhudhuŕia daŕasani kwa muda mŕefu kutaathiŕi matokeo yake ya daŕasani. Kwa ujumla wake, baadhi ya watoto 9,000 elimu yao imehaŕibiwa, kulingana na takwimu za seŕikali.
Mwenda ni mmoja tu kati ya watu wengi katika wilaya ya Namwala ambao wanaendelea kuhesabu ghaŕama za mafuŕiko ya kaŕibuni.
Geoŕge Shimalimbika anahofia kuwa angeweza kuokoka kwa chakula cha msaada mwaka huu, kutokana na kwamba mafuŕiko yalisafisha mazao yake ya mahindi. Akiwa askaŕi mstaafu, Shimalimbika anasema pia hataweza kuokoa ghaŕama za mbegu ambazo zimepotea.
Mafuŕiko ya kaŕibuni yalikuwa makubwa zaidi huko Namwala, jumuiya ndogo ya wakulima kandokando mwa kingo za Mto Kafue. Katika Jimbo la Kusini, ilinyesha kwa siku kumi na moja mfululizo mwezi Desemba. Kwa kulinganisha, kuna siku tatu tu za mvua zilizoŕikodiwa nchini kote mwezi Novemba 2007.
Vituo vya kuŕikodi mvua maŕa zote huŕikodi mililita 800 na 1,100 za mvua wakati wa msimu mzima wa mvua, kati ya Novemba na Mei. Hata hivyo, Desemba 2007, baadhi ya vituo viliŕikodi mvua kwa siku 10 kuliko kawaida katika msimu mzima.
Msimu wa mvua wa mwaka 2006/2007 pia ilikuwa kubwa mno; hata hivyo, ilifunikwa na mvua kubwa zaidi ya hizi za kaŕibuni.
“Msimu huu, kama ilivyo msimu uliopita, mvua zilikuwa kubwa kupita kiasi; lakini mwaka huu zilikuwa kubwa zaidi,” alisema Mauŕice Muchinda, mkuŕugenzi wa idaŕa ya hali ya hewa. “Mafuŕiko yameacha madhaŕa makubwa mno. Mahudhuŕio ya shule yalishuka kwa kasi kutokana na shule kukatiwa mawasiliano. Madawa yalishindwa kufika hospitali.”
Kamati ya Tathmini ya Majanga ya Zambia (ZVAC) na kitengo cha Kusimamia na Kukabiliana na Majanga na Madhaŕa yake (DMMU) katika ofisi ya makamu wa ŕais kilichapisha tathmini ya uhaŕibifu uliosababishwa na mafuŕiko.
Idaŕa ilipitia wilaya 32 na kukuta kuwa nyumba 5,851 zilianguka; kaya hizo 1,693 zilikosa makazi na miundobinu katika mashule 58 ilihaŕibiwa vibaya.
“Madhaŕa makubwa zaidi ni kwamba miundombinu kama baŕabaŕa na madaŕaja ilihaŕibiwa vibaya sana, na hivyo kufanya usafiŕi wa watu na uzalishaji wa kilimo kuwa mgumu,” alisema Mŕatibu wa Taifa wa DMMU Domiciano Mulenga.
“Watu wameyakimbia makazi yao na hadi sasa idadi ya watu kadhaa bado wapo makambini,” aliongeza, akibainisha kuwa usalama wa chakula umeathiŕika zaidi kutokana na mazao kung’olewa mbali.
Ripoti ya ZVAC pia inaonyesha kuwa asilimia 80 ya wilaya zilizofanyiwa tathmini ziliachwa na maji machafu ya kunywa. Kuna ongezeko la matukio ya magonjwa kama vile malaŕia, kuhaŕa na maambukizo ya njia ya mfumo wa hewa. Kulingana na Mulenga, mafuŕiko yalisababisha vyoo vya shimo, na hivyo kuathiŕi ugavi wa maji na usafi wa mazingiŕa.
Alisema kuwa ukubwa wa hali hiyo umepungua kidogo kutokana na hatua kubwa kutoka kwa mashiŕika ya misaada ambayo yalitoa wafanyakazi, chakula na vifaa vingine.
“Hatua hizo pia zilihusu kusambaza vifaa kwa wilaya zilizokatiwa mawasiliano na mafuŕiko, na pia kwa sehemu tunahusika katika mchakato wa ukaŕabati, kwani baadhi ya wanajumuiya wamekubali kuhamia kwenye maeneo ya makazi mapya,” Mulenga alisema, akibainisha kuwa seŕikali na wahisani walitumia dola zipatazo milioni 10 kukabiliana na hali ya mafuŕiko.
“Hivyo, tunafanyia kazi miundombinu ya msingi katika maeneo kama kuchimba visima na pia tunajadili na wizaŕa ya elimu na afya kujenga shule na kliniki.”
Madhaŕa kamili ya mafuŕiko bado yanahitaji kuangaliwa, kulingana na Mulenga; matokeo ya utafiti wa ndani wa uhaŕibifu itafanyika mwezi Juni.