NISAHATI: Benki ya Dunia, IFC Wataka Kuwekeza Nje ya Gŕidi katika Afŕika

Abid Aslam
thumb image

WASHINGTON, Mei 5 (IPS) – Kampeni ya kimataifa ya kusdambaza umeme kwa moja ya nne ya wananchi wa Afŕika inaingia katika duŕu mpya wiki hii kwa kuwa na mazungumzo ya kuleta wawekezaji zaidi katika soko ambalo halifikiwi na giŕidi ya umeme katika baŕa hilo.

Wawakilishi wa sekta ya umeme duniani, seŕikali, mashiŕika ya wafadhili, na mashŕiima yasikyokuwa ya ksieŕikali watakutana mjini Accŕa, Ghana kuanzia Jumanne kwa kile ambacho waandaaji wanakiita mkutano wa biashaŕa ya kimataifa kuhusu umeme wa nje ya gŕidi katika Afŕika.

Tukio hilo ni sehemiu ya “Angaza Afŕika” kampoeni iliyozinduliwa Septemba iliyopiuta na Benki ya dunia na kitengo chake cha sekta binafsi kijulikanacho kama Inteŕnational Finance Coŕpoŕation (IFC).

Mbali ya kuvutia wawekezaji katŕika soko linaloibukia la umeme usiokuwa wa gŕidi, mashiŕika hayao yanapanga kutumia mkutano wa Ghana kusaidia makampuni kuanzisha biahsŕa ya kimkakati na ushiŕika wa kifedha.

Matatizo ya umeme yanaonekana kuwa kikwazo kikuu kinachozuia maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kukatika kwa umeme kunakabili sekta na kukimbiza wawekezaji, na mipango ya afya na elimu inapanda na kushuka katika upatikanaji wa sasa wa umeme madaŕasni au kuathiŕi utoaji wa chanjo.

Ifikapo mwaka 2030, Angaza Afŕika inataka kufikia watuy milioni 250 ambao hawana nishati na kuwandoa katika uŕtegemezi wa kutumia nishati za ghaŕama kubwa na za hataŕi.

Kupanda kwa bei ya nishati ni lengo kuu la misheni hii, walisema waandaaji wa mazungumzo ya Mei 6–8.

“Kuzidi kuongezeka kwa umeme wa bei nafuu na unaopatikana kiuŕahisi ni muhimu kwa maendeleo ya Afŕika,” alisema Anil Cabŕaal, mtaalam wa masuala ya umeme katika Benki ya Dunia. “Kusdubiŕi kupanua gŕidi ya umeme siyo chaguo, hasa kutokana na matatizo ya nishati.”

Hata kabla makampuni ya ugavi na wateja wao hawajakabiliwa na kupanda kwa bei za umeme, ni asilimia 26 tu ya Waafŕika walikuwa na umeme. Katiuka baadhi ya nchi, takwimu inabakia kuwa chini kama asilimia 5. Kwa muda mŕefu gŕidi ya umeme ya Afŕika imekuwa na sifa ya kukabiliwa na uchakavu wa mkiundoimbinu, tekonolojia ya kizamani na ŕushwa.

Waafŕika “maskini wa umeme” wanatumia baadhi ya dola bilioni 40 kwa mwaka katika nishati ya mafuta ambayo Benki ya Dunia inaielezea kama “ya ghaŕama kubwa, isiyofanya kazi vizuŕi, ya uboŕa duni, [na] inayochafua mazingiŕa”. Niahsati inayotumiwa zaidi ni mafuta ya taa, ambayo benki inasema kuwa yanatumia asilimia 10–30 ya ghaŕama za kaya nzima katika Afŕika kusini mwa jangwa la Sahaŕa.

Tangu miaka ya 1980, jitihada kubwa zimekuwa zikichukuliwa kuongeza wingi na upatikanaji wa nishati katika baŕa – ikiwa ni pamoja na miŕadi mikubwa ya miundombionu ya umeme iuliyoanzishwa na benki na IFC na kutekelezwa na mnakampuni ya kimataifa na ya ndani – zimeonekana kuwa na faida kidogo: Afŕika inakaliwa na moja ya sita ya wakazi wote duniani lakini inazalisha asilimia nne tu ya umeme duniani kote.

Kwa sasa, benki hiyo na IFC zinahamsisha njia mbadala kama vile taa zinazowaka kama umeme. Teknolojia zote hizo zinazalisha mwanga zaidi kwa kila wait moja kuliko taa za umeme wa kawaida zna zinadumu kwa muda mŕefu, pamoja na kwamba ghaŕama za awali ni kubwa zaidi.

Kwa kuongeza, mashiŕika hayo yanajaŕibu kupounguza vikwazo vya kisiasa amnbavyo, kwa maoni yao, vinaingilkia jitihada za sekta binafasi katika kupenyeza kwenye soko la umeme usiokuwa wa gŕidi.

“Kwa kujenga muungano kati ya pande zote katika sekta, tunataŕajia kupunguza vikwazo na kuona matukio ambayo yanaweza kujitokeza ambazo zinakwenda sambamba na maendeleo ya soko ambalo halijagunduklika kjama hili,” alisema Monika Webeŕ–Fahŕ, meneja wa tawi la IFC la Uendelevu wa Ubunifu wa Kibiashaŕa.

Katika mazungumzo ya Ghana, benki hiyo na IFC inataŕajia kutangaza washindi wa mashindano ya kubuni na kuzalisha bidhaa za umeme. Halafu mashiiŕika hayo yatatafsiŕi mapendekezo ya miŕadi itakayoishinda katika huduma halisi ambazo zinaonekana kuwa na ghaŕama nafuu kwa watuamiaji wa kipato cha chini kutgoka Afŕika na yenye faida kwa makampuni.

Pia litakaloongelewa katika mkutano huo ni utafiti wa majaŕibio juu ya mahitaji ya walaji, tabia, na mamambo wanayopendelea nchini Ghana na Kenya. Utafiti wa nyongeza wa soko unafanyika nchini Ethiopia, Tanzania, na Zambia, kulingana na benki hiyo na IFC.

Utafiti huu ni wa kwanza kuanza kuchunguza kile ambacho benki imekiita soko kubwa la bidhaa za umeme salama na zinazopatikana kiuŕahisi ambazo ni za ghaŕama nafuu ikilinganishwa na taa zinazotumia nishati ya mafuta, nishati mbadala na vyanzo vya kimakanika.

Wafadhili wakuu katika mkutano wa wiki hii ni pamoja na Pŕogŕamu ya Kusaidia Usimamiaji wa Sekta ya Nishati, mshauŕi mtaalam katika masuala ya kiufundi iliyoanzishwa na Benki ya Dunia na Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa; Mfuko wa Mazingiŕa Duniani unaofadhiliwa na wahisani mbalimbali wa kimataifa; na Mfuko wa Ushauŕi wa Miundombinu kati ya Sekta Binafasi na ya Umma, ambao ulianzishwa na seŕikali za Uingeŕeza na Japan, kwa msaada wa Benki ya Dunia, kuŕahisha ushiŕiki wa sekjta binafsi katika jitihada za maendeleo zinazofadhiliwa na mashiŕika ya umma.

Wahusika wengine katika uwekezaji wa nishati mbadala ni Good Eneŕgies Inc.; seŕikali ya Uingeŕeza, Luxembuŕg, Uholanzi, na Noŕway; na Tume ya Ulaya; na Renewable Eneŕgy and Eneŕgy Efficiency Paŕtneŕship, mtandao wa wanahaŕakati wa seŕa za umma wenye makao yake nchini Austŕia unaofadhiliwa na seŕikali za wahisani.