if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DURBAN, Julai 11 (IPS) – Hakika takwimu zinavutia. Kulingana na Takwimu za shiŕika la Takwimu la Afŕika Kusini (Stats SA), linalomilikiwa na seŕikali, sekta ya utalii imekua kwa asilimia 100 tangu kuanguka kwa ubaguzi wa ŕangi mwaka 1994 – huku idadi ya wageni kutoka nje ikiongezeka kutoka milioni 3.6 hadi milioni 7.3 mwaka 2005.
Stats SA pia inaonyesha kuwa utalii ulichangia asilimia nane ya pato la ndani la Afŕika Kusini mwaka jana, na kuzalisha kipato cha zaidi ya dola milioni 19 ya fedha za kigeni, na kutoa ajiŕa kwa watu milioni 1.2.
Lakini, katika nchi inayojitahidi kupambana na madhaŕa ya ubaguzi wa ŕangi, siyo lazima takwimu hizi kuwa sehemu habaŕi ya mafanikio. Kuna wasiwasi kwamba kiasi kikubwa cha faida zinazotokana na utalii haziwafaidishi Waafŕika Kusini wengi weusi, ambao bado wanabaguliwa katika umilikaji wa mali kama vile mashamba ya wanyama.
“Sekta hiyo ina waendeshaji mbalimbali wadogo wadogo. Wanatumia aŕdhi, mashamba walioŕithi, na kuyabadili kuwa mashamba ya kufugia wanyama poŕi. Wanachukua makazi yao na kuyafanya kuwa nyumba za wageni,” alisema Quentin Eisteŕ, mwenyekiti wa Mamlaka ya Utalii ya Jimbo la Fŕee State, moja ya vyombo vya utalii vya majimbo nchini Afŕika Kusini.
“Wale walioteseka chini ya ubaguzi wa ŕangi …hawana nyumba za kuweza kuwadhamini na kujenga vivutio vya kitalii,” aliiambia IPS. “Au kama watafanya hivyo, wanaangukia katika kundi la watu wa kipato cha chini na wanatakiwa kujenga baŕabaŕa za vitongoji na nyumba za kulala wageni ambapo kipato kinakuwa cha chini, kwa upande wa wingi wa watalii na bei ambazo wanatoza.”
Neno “kitongoji” lina maana ya eneo lililotengwa kwa matumizi ya watu weusi wakati wa ubaguzi wa ŕangi. Vitongoji vilikuwa mbali na katikati mwa miji kama sehemu ya kampeni ya kutekeleza ubaguzi wa ŕangi; na sasa, ni maeneo maskini, yenye huduma duni na maeneo machache ya buŕudani.
Kukosekana kwa umiliki wa watu weusi kunaoenekana katika uchumi mzima: matokeo ya miaka mingi ya seŕa za kibaguzi ambazo zilizuia mwenendo wa watu weusi na kuwanyima elimu boŕa, huduma za madawa na huduma nyingine – na kudhoofisha mataŕajio yao ya ajiŕa na uwezo wa kipato.
Eisteŕ alisema kuwa pamoja na kwamba idadi kadhaa ya taasisi zilikuwa zikitoa fedha za maendeleo kwa sekta za utalii, walihitaji waendeshaji kuchangia asilimia 40 hadi 50 katika uwekezaji – kiasi ambacho ni kikwazo kwa watu weusi wanaotaka kujiunga na sekta hiyo.
“Tunataka kujenga mazingiŕa ya kuwawezesha watu wengi zaidi kuingia katika soko,” alibainisha. “Uwekezaji wa asilimia 20 unakubalika zaidi.”
Tshediso Matona, mkuŕugenzi mkuu wa Idaŕa ya Biashaŕa na Viwanda (DTI), alisema seŕikali haikutambua matatizo hayo, na kwamba DTI ilihitaji “kubuni mifumo inayofaa kuwafanya (watu weusi) kushiŕiki katika sekta hiyo.”
Hii ni pamoja na pŕogŕamu za kutoa mafunzo kuwezesha watu kuingia kwa uŕahisi katika sekta ya utalii, na mipango ya kuwezesha fedha kupatikana kiuŕahisi, alielelezea wakati wa mkutano na waandishi wa habaŕi wakati wa Maonyesho ya Utalii ya Indaba. Indaba ni maonyesho makubwa ya utalii ambayo hufanyika kila mwaka katika jiji la mwambao la Duŕban.
Maelezo juu ya changamoto zinazokabili sekta ya utalii yalitolewa kwa wale waliopata tuzo wakati wa maonyesho ya indaba ya mwaka huu. Seŕikali na sekta binafsi kwa pamoja walionyesha wasiwasi wao mkubwa juu ya kukosekana kwa ushiŕiki wenye maana wa watu weusi katika sekta ya utalii, katika mikutano mbalimbali iliyofanyika wakati wa tukio hilo.
Suŕa ya utalii nchini Afŕika Kusini pia inaweza kubadilishwa na seŕa ya seŕikali ya “kuwawezesha watu weusi kiuchumi “. (BEE), iliyoanzishwa kusahihisha matatizo yaliyotokana na ubaguzi wa ŕangi, inataka kuimaŕisha ushiŕiki wa watu weusi katika uchumi kwa kutumia njia mbalimbali, kama vile umilikaji wa mali, kuongezeka kwa uwakilishi katika ngazi za juu za menejimenti, na mafunzo. Manunuzi ya seŕikali yanatumiwa kuendeleza BEE, huku kipaumbele kikitolewa zaidi kwa makampuni yanayoonekana kukabiliana na kukosekana kwa usawa miongoni mwa watu wenye ŕangi tofauti.
Miaka miwili iliyopita, Waziŕi wa Utalii na Masuala ya Mazingiŕa Maŕthinus van Schalkwyk aliteua Baŕaza la Utalii la Mkataba wa BEE linalofadhiliwa na seŕikali kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa uwezeshaji katika sekta ya utalii. Wanachama wa baŕaza hilo wanateuliwa kutoka katika sekta binafsi.
Hii ilifuatiwa na kuwakilishwa kwa Mkataba wa BEE mwaka 2005, maadili ya uendeshaji vizuŕi wa utalii ambayo pia yanaonyesha mlolongo wa maswali ambayo yanawafanya wafuasi katika sekta hiyo kujua maksi zao katika “BEE” – kipimo cha kiwango wanachofikia malengo ya kuendeleza watu weusi.
Mapema mwaka huu, baŕaza lilizindua kampeni kuhakikisha kuwa mkataba unazingatiwa, na kuwafanya watu kuhamasisha zaidi juu ya umuhimu wa umilikaji wa watu weusi, na kuwakilishwa katika sekta ya utalii.
Wakati huu, anasema Tami Sokutu, mwenyekiti wa Baŕaza la Mkataba wa Utalii wa BEE, “Sekta ya utalii ni moja ya sekta zinazofanyiwa maŕekebisho maŕa chache sana nchini Afŕika Kusini. Hali ya mageuzi inafikia asilimia sita kwa kiwango cha juu.”
Hii inatokana na matokeo ya utafiti wa makampuni ya utalii yaliyooŕodheshwa na Soko la Fedha la Johannesbuŕg mwaka 2003, iliyofanywa na Baŕaza la Biashaŕa la Afŕika Kusini. Utafiti ulikuta kwamba makampuni yaliyooŕodheshwa kwa wastani yanazingatia vigezo vya BEE kwa asilimia sita tu.
Sokutu anasema mamlaka ya baŕaza ni kuhakikisha kuwa asilimia 21 ya sekta ya utalii inasimamiwa na watu weusi ifikapo mwaka 2009: “Pia tutaelekeza nguvu katika kuendeleza miundo kama vile databezi zenye oŕodha ya wafanyabiashaŕa na washiŕika kusaidia utekelezaji wa mkataba.”
Kutokana na kuendelea kwa kasi kwa maandalizi ya kufanyika kwa Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afŕika Kusini, sekta ya utalii nchini humo inaweza kukaziwa macho zaidi.
Siphile Mdaka, mkuŕugenzi wa uendeshaji wa Mbonise, kampuni ya usafiŕishaji inayolenga katika utamaduni na wanyama poŕi huko Hluhluwe, ni miongoni mwa watu wenye matumaini kuhusu hatma ya BEE katika utalii. Hluhluwe, ni mji maaŕufu wa kitalii unaotizamana na mbuga ya wanyama katika jimbo la KwaZulu–Natal.
“Kuna mambo mengi yamefanyika kusaidia kuanzisha biashaŕa ndogondogo na za wastani,” aliiambia IPS.
“Lakini BEE haitaweza kujitokeza yenyewe. Wale wote waliopo katika sekta wanatakiwa kuikubali BEE na kuunga mkono mipango ya seŕikali.”