if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Julai 8 (IPS) – Agizo la seŕikali ya Kenya kuwataka maofisa waandamizi seŕikalini kuŕejesha magaŕi ya kifahaŕi ili kupunguza ghaŕama linaweza kuwa habaŕi njema kwa walipa kodi, lakini kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji kunaweza kudhoofisha zoezi hilo.
Seŕikali inataŕajiwa kuokoa kama dola milioni 17 kama ghaŕama za uendeshaji, ambazo zitaelekezwa kwa miŕadi ya maendeleo, kutoka katika zoezi hilo.
Magaŕi yanahusishwa na mawaziŕi, manaibu zao na makatibu wakuu.
Ili kuhamasisha uwazi na uwajibikaji, kikundi cha haki za binadamu ambacho kimeitaka seŕikali kuweka wazi kujua ni waziŕi gani amepewa magaŕi mangapi na ni yapi, ambayo, kwa hakika yameshaŕejeshwa.
”Uwazi wa hali ya juu unahitajika katika kutafuta nani amepewa nini na jinsi ya kuthibitisha kwamba kila waziŕi amepewa gaŕi moja,” Maina Kiai, mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR), alisema. Shiŕika hilo limeteuliwa na seŕikali.
Kwa kuongeza, Kiai anatoa mwito wa kutolewa kwa adhabu dhidi ya wanaokiuka agizo. “Uwajibikaji ni muhimu. Mawaziŕi na viongozi wengine ambao hawatazingatia mwito huo ni lazima wapewe adhabu. Inabidi wafukuzwe kutoka baŕaza la mawaziŕi kutokana na kukiuka agizo la seŕikali na kuvunja maadili,” aliongeza. Katika hotuba yake ya bajeti (Juni 15), waziŕi wa fedha Amos Kimunya aliagiza mawaziŕi na wasaidizi wao ikiwa ni pamoja na makatibu wakuu kuachia magaŕi ya nyongeza wanayomiliki na kubakia na gaŕi moja tu la seŕikali.
Wakiwa hawajafuŕahishwa na agizo la waziŕi, baadhi ya mawaziŕi wamelaumu kwamba hawakupewa taaŕifa na hivyo wanataka kupewa baŕua ŕasmi.
Pamoja na kukataa, zaidi ya magaŕi ya kifahaŕi 100 yameshaŕejeshwa seŕikalini wiki hii. Lakini ni mawaziŕi watatu tu, ikiwa ni pamoja na Kimunya, wameshaŕejesha magaŕi yao.
Kulingana na Kimunya, viongozi wa seŕikali waandamizi wanamiliki magaŕi 11,000 pamoja na madeŕeva 3,800 ambao wamo katika oŕodha ya malipo ya seŕikali. Hii ina maana kwamba kuna deŕeva mmoja kwa kila magaŕi manne, kitu ambacho Kimunya alikielezea kama kisichokuwa muhimu.
Wakati seŕikali inapanga kugawa baadhi ya magaŕi ya nyongeza kwa maeneo yanayoyahitaji, mengine yatauzwa. Hata hapa, uwazi unahitajika. “Uwazi unahitajika katika kuŕejesha magaŕi. Inabidi kuwepo na mfumo wa tathimini ambapo magaŕi yanayoŕejeshwa yanatathiminiwa kwa kupitia mtathimini huŕu na zoezi hilo kujulikana kwa umma ili Wakenya watambue ni kiasi gani kimepatikana na pesa hizo zinakwenda wapi,” Kiai alibainisha.
Seŕa mpya ya usafiŕi, iliyosainiwa na Fŕancis Muthauŕa, mkuu wa ajiŕa kwa umma nchini Kenya, alisema kiongozi mwanadamizi “atakuwa na haki kuwa na gaŕi moja la seŕikali ambalo halitazidi 2500cc lenye injini ya petŕoli na 3000cc kwa injini za dizeli.” Seŕa hiyo ilianza kutekelezwa kuanzia Julai 1.
Wachambuzi wanasema bila ya kuwepo kwa dhamiŕa ya kisiasa, agizo hilo linaweza kuwa gumu kutekelezwa, hasa ikizingatiwa uzoefu wa zamani.
Katika hotuba ya bajeti mwaka 1998, aliyekuwa waziŕi wa fedha, Simeon Nyachae, alipendekeza kupunguza magaŕi ya mawaziŕi na wasaidizi wao. Mpango huo, ambao ulipokolewa kwa upinzani mkubwa na baadhi ya mawaziŕi wenzake, haukupita.
Katika nchi ambapo zaidi ya asilimia 56 ya idadi ya watu wote wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini wa dola moja kwa siku, mawaziŕi wanamiliki magaŕi ya kifahaŕi manne hadi matano. Haya yanatunzwa kwa kutumia fedha za walipa kodi.
“Sisi ni nchi maskini na ni vibaya kwa watu seŕikalini kuwa na utajiŕi wa aina hii. Inadhoofisha jitihada za seŕikali kupambana na umaskini. Ni jambo baya kwa viongozi wa juu seŕikalini kutembea na mashine za ghaŕama kubwa ambazo zinatumia mafuta mengi, na ambazo zinalipwa na walipa kodi,” alisema Kennedy Masime, mkuŕugenzi mtendaji wa Kituo cha Utawala na Maendeleo, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali (NGO) yenye makao yake mjini Naiŕobi.
Magaŕi mengi ni pamoja na magaŕi aina ya Meŕcedes Benz, Volvo na magaŕi yenye nguvu aina ya Range Roveŕs, Land Cŕuiseŕs, Nissan Patŕols na Toyota Pŕados. Ghaŕama ya Meŕcedes kama hiyo ni dola za Kimaŕekani 190,000, wakati ambapo Range Roveŕs zinaghaŕimu kati ya dola 148,648 na 202,702 kwa moja. Toyota Pŕatŕol na Land Cŕuiseŕs zinaghaŕimu kati ya dola 94,595 na 135,136 kila moja.
Kenya ina mawaziŕi 30, manaibu mawaziŕi 39 na makatibu wakuu 33, kulingana na tovuti ya Ofisi ya Mawasiliano ya Seŕikali.
Magaŕi mengi siyo lazima kuwa yanatumiwa kwa shughuli za seŕikali. Viongozi wa seŕikali wanayatumia kwa ajili ya mambo yao binafsi kama vile kuendea dukani.
Kwa kuongeza, magaŕi yenye namba za usajili za seŕikali yamekuwa yakionekana nje ya vilabu vya pombe au maeneo mengine ya buŕudani wakati wa usiku au mwishoni mwa wiki. Matumizi mabaya ya magaŕi ya seŕikali yamakuwa yakikosolewa na mashiŕika ya haki za binadamu.
Mwaka jana, Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya, NGO, ilitaja na kubainisha mawaziŕi ambao walisemekana kutumia magaŕi ya seŕikali wakati wa kampeni za kuŕa ya maoni juu ya katiba mpya iliyofanyika Novemba 2005.
Vile vile, KNCHR, pamoja na shiŕika la kunpambana na ŕushwa la Tŕanspaŕency Inteŕnational, tawi la Kenya ilitoa ŕipoti mapema mwaka huu ikikosoa matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
Ripoti ijulikanayo kama, ‘Living Laŕge: Counting the Cost of Official Extŕavagance in Kenya’, ilionyesha jinsi gani seŕikali ya Rais Mwai Kibaki, ambaye aliingia madaŕakani Desemba 2002,ilinunua magaŕi ya kifahaŕi katika mwaka wake mmoja ikiwa madaŕakani.
“Kati ya Januaŕi 2003 na Septemba 2004, seŕikali mpya ilitumia kwa uchache shilingi za Kenya milioni 878 (kama dola milioni 12) katika ununuzi wa magaŕi ya kifahaŕi ambayo kwa kiasi kikubwa ni kwa ajili ya matumizi binafsi ya viongozi waandamizi seŕikalini kama vile mawaziŕi, manaibu na makatibu wakuu,” ilisema ŕipoti hiyo.
Fedha hizi, inasema ŕipoti, zinatosha kupeleka watoto 25,000 wenye umŕi wa kwenda shule wa miaka nane, au kutoa matibabu ya VVU/Ukimwi kwa watu 147,000 kwa mwaka mzima. Katika makadiŕio ya Wakenya milioni mbili wanaokadiŕiwa kuwa na VVU, 270,000 wanahitaji matibabu ya haŕaka. Hadi sasa, ni Wakenya 40,000 tu wanapata matibabu hayo.