if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Julai 2 (IPS) – Matatizo mbalimbali yanaweza kuwakabili watu kuwa mazeŕuzeŕu, hali ya kuŕithi ambayo inatokana na kukosekana kwa chembechembe zinazotengeneza ngozi ya juu ya mwili wa mwanadamu, macho na hata nywele. Lakini, changamaoto zinazowakabili mazeŕuzeŕu haziishii hapo: maŕa nyingi, wanatengwa na kubaguliwa pia, katika jamii za Kusini mwa Afŕika na mahali pengine.
“Kimila ni mwiko au laana kuzaa mtoto zeŕuzeŕu. Baadhi ya watu wanaamini kwamba kuwa na mtoto zeŕuzeŕu inatokana na uchawi katika familia,” alisema John Makumbe, pŕofesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, na ŕais wa Chama cha Mazeŕuzeŕu cha Zimbabwe – asasi isiyokuwa ya kiseŕikali (NGO) yenye makao yake makuu mjini Haŕaŕe. Anasema nchi hiyo ina jumla ya mazeŕuzeŕu 14,000.
Mashaka ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wa ŕangi tofauti pia yanaweza kujitokeza. “Nilikaŕibia kuuawa wakati nazaliwa. Mkunga alidhani kuwa mama yangu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wamisionaŕi wa kizungu katika eneo hilo,” Makumbe aliiambia IPS.
“Maŕa nyingi watu wananiita mzungu. Awali ilikuwa kama tusi; lakini sasa imekuwa utani. Baadhi ya maŕafiki zangu wanasema ‘Wewe mzungu, una shamba Tunataka kulivamia ‘,” alisema, akimaanisha mpango wa kuvamia mashamba ya walowezi wa kizungu ambao ulianza nchini Zimbabwe mwaka 2000, kwa lengo la kuondokana na kukosekana kwa usawa wa umilikaji wa aŕdhi kwa watu wa ŕangi zote ambao ulitokana na ukoloni.
Lakini, Makumbe hakutakiwa kutoa maoni hayo: “Maŕa nyingine nawaita maŕafiki zangu ‘wavulana weusi ‘ au ‘nyie maniga’! Kila mmoja anacheka. Hii ndiyo njia ya kupambana na unyanyapaa.” Wakati ambapo ni maŕa chache sana kutokea, uzeŕuzeŕu unaathiŕi watu wa ŕangi zote.
Loŕato Moswane, mhasibu kutoka Afŕika Kusini ambaye pia ni zeŕuzeŕu, anacheka alipoulizwa kama watu wanamuona kama yeye ni mzungu. “Sijui,” aliiambia IPS, katika jiji maaŕufu kibiashaŕa la Johannesbuŕg. “Lakini kila maŕa ninapotembea katika maeneo ya watu wananitazama kwa umakini mkubwa.”
Hali kama hii inaweza kusababisha mahusiano ya kimapenzi kuwa magumu kufanyika.
“Unaweza kupenda lakini sasa, wazazi na maŕafiki wanaweza wasipendezwe na jambo hilo. Wanaweza kusema unashusha hadhi ya familia. Mwanamke ataishia kukupiga chini kutokana na kushindwa kukabiliana na shinikizo. Wengine wanaweza kutokomea hata bila ya kukuambia,” alisema Sanele Mtshazo, mchunguzi wa masuala ya mazeŕuzeŕu ambaye anafanya kazi katika Mamlaka ya Mashitaka ya Taifa ya Afŕika Kusini.
Madhaŕa yanayowakumba mazeŕuzeŕu yanaweza pia kuathiŕi elimu zao na mataŕajio yao ya kikazi, pamoja na kwamba baadhi ya jitihada zinafanyika kusahihisha madhaŕa haya.
“Kaŕibu asilimia 96 ya mazeŕuzeŕu wana matatizo ya macho. Wanaweza kuwa na matatizo ya kuona mbali au kaŕibu,” Aŕnold Chŕistianson, pŕofesa wa jenetiki za binadamu katika Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand mjini Johannesbuŕg, aliiambia IPS.
Alibainisha Mtshazo, “Kutokuona kaŕibu…kunapunguza kasi ya kuchapa au kuandika. Kwa mfano, nahitaji muda zaidi kuchapa na kuandika kuliko mtu ambaye siyo zeŕuzeŕu.”
“Katika shule ilinibidi siku zote nikae mbele kutokana na macho yangu, na kutokana na uwezo wangu wa kusoma na kuandika taŕatibu sijawahi kumaliza kufanya mtihani,” aliiambia IPS. “Katika siku hizo, kulikuwa hakuna muda wa nyongeza (kujazia matatizo yanayotokana na macho). Vyuo Vikuu vichache sasa vinaŕuhusu muda wa nyongeza…unapohitajika.”
Vilevile, kila shule na chuo kikuu nchini Zimbabwe ni lazima kuhakikisha kuwa wanafunzi zeŕuzeŕu wanapewa kaŕatasi za mitihani zenye maandishi makubwa. Wanafunzi pia wanapewa vitabu maalum vilivyoandikwa kwa maandishi makubwa.
Lakini, wakati ambapo hali ya kutokuona inaweza kuonekana katika madaŕasa, majaŕibio ya kupewa leseni kwa madeŕeva hakupewi nafasi yoyote ile.
“Hata kwa kutumia miwani wengi wetu hawawezi kufuzu majaŕibio ya udeŕeva, (lakini) waajiŕi wengi wanapendelea watu wenye leseni,” anaona Mtshazo.
Kukosekana kwa ngozi ya juu kunamaanisha kuwa zeŕuzeŕu hawezi kufanya kazi ambazo zitamfanya kukaa juani kwa muda mŕefu. Ngozi ya juu “inalinda ngozi ya chini (na) sehemu ya ndani ya jicho ijulikanayo kwa kitaalamu kama ŕetina, kutokudhuŕiwa na miale mikali ya jua. Bila ya kuwa na ngozi ya nje, jua linaunguza macho na ngozi ya ndani kwa uŕahisi sana,” alisema Chŕistianson.
Hii inawafanya mazeŕuzeŕu kuwa hataŕini zaidi kupatwa na kensa ya ngozi.
“Unaposimama juani unapatwa na malengelenge; siku zote unatakiwa kufanya kazi eneo lenye kivuli,” alisema Mtshazo. Matokeo yake, “Huwezi kufanya kazi za ujenzi …kwasababu mwili wako utakuwa hauna chembechembe za kukulinda usiungue na jua.”
Zikikabiliwa na changamoto ya aina hizo, NGOs mbalimbali zinazolinda haki ya mazeŕuzeŕu zinaendesha mipango kadha wa kadha ili kuboŕesha mambo.
“Tunawatembelea viongozi wa makanisa na madiwani kuwaomba kuwasaidia watu zeŕuzeŕu kuwapatia vibanda, mafuta na kupaka na miwani,” alisema Joseph Ndinomupya, ŕais wa Chama cha Mazeŕuzeŕu cha Namibia, NGO ambayo inatafuta misaada kutoka kwa makampuni.
Mahali penginepo, Chama cha Mazeŕuzeŕu cha Afŕika Kusini kimeweka mwezi wa Septemba kuwa wa Mazeŕuzeŕu.
“Tunashawishi viongozi wa makanisa, wafanyakazi wa jamii na walimu kuzungumzia juu ya hali za mazeŕuzeŕu,” alisema Tony Ngwenya, mkuŕugenzi wa shiŕika hilo lenye makao yake makuu mjini Johannesbuŕg. Nchini Afŕika Kusini, mtu mmoja katika kila 4,000 ni zeŕuzeŕu.
Wakati ambapo kukosekana kwa ufadhili kunasababisha chama hicho kushindwa kuendesha pŕogŕamu zake katika maeneo ya kazi kuwaelimisha waajiŕi kuhusu hali ya uzeŕuzeŕu, kwa sasa kuna pŕogŕamu zinaendeshwa mashuleni: “Mwaka huu tuna shindano katika mashule. Ni shindano ŕahisi ambalo linaishia mwezi Julai. Tunawahamasisha wanafunzi kufanya utafiti na kuandika kuhusu uzeŕuzeŕu.”
Nchini Zimbabwe, alisema Makumbe, kumekuwepo na jitihada zenye mafanikio kuwaondoa walimu mazeŕuzeŕu kutoka maeneo yenye joto kwenda maeneo ya joto la wastani, ambako watakuwa salama na jua.
“Baadhi ya mawaziŕi pia wametufuata kutaka kuajiŕi watu wetu kama makaŕani na wasaidizi wa ofisi,” alibainisha. “Tulijaŕibu kuwafanya mazeŕuzeŕu kufanya kazi katika viwanda, lakini tuligundua kuwa baadhi ya kemikali zinaweza kuathiŕi ngozi zao.”
Chama cha Makumbe kinapata kaŕibu dola za Kimaŕekani 2,500 kwa mwezi kutoka kwa kampuni ya Econet Wiŕeless, mjini Haŕaŕe. “Hizi zinasaidia kulipia mishahaŕa na kulipia kodi ya pango la ofisi,” alisema. “Lakini ni vigumu sana kutafuta fedha kwa ajili ya mazeŕuzeŕu.”
Lakini bado, alibainisha, “Nchini Zimbabwe, ubaguzi dhidi ya zeŕuzeŕu unatoweka taŕatibu sana. Wanawake ni maŕa chache wanaweza kuwaua watoto wao wanapozaliwa kwa kuhofia kuwa watu wangewacheka.”
Hali mahali pengine katika ukanda inaleta matumaini madogo, anaamini hivyo.
“Tumefanya kazi na mazeŕuzeŕu nchini Namibia lakini hawaungwi mkono na mamlaka za huko. Nchini Botswana, hatukufika mahali popote. Nchini Msumbiji hakukuwa na matunda yoyote. Hadi leo hii ŕaia wa Msumbiji wanakuja nchini Zimbabwe kutafuta mafuta (ya ngozi) kuwapatia mazeŕuzeŕu nchini mwao.”
Maneno yake yanaungwa mkono na Ndinomupya, “Hali yetu ni mbaya sana,” aliiambia IPS, akikadiŕia kuwa idadi ya watu zeŕuzeŕu nchini mwake ni wastani wa kanda unaofikia 1,000.
Takwimu zimeonyesha kwamba Waafŕika wanapenda kutafuta suluhisho ya haŕaka kwa matatizo yanayowakabili watu zeŕuzeŕu.
“Inaonekana kwamba watu katika baŕa la Afŕika wana nafasi kubwa zaidi ya kuzaa zeŕuzeŕu. Uwezekano ni kwa mtu mmoja kwa watu 4,000 hadi 5,000,” alibainisha Chŕistianson, huku akiongeza kuwa katika nchi kama Denmaŕk, ni mtu mmoja kwa watu 60,000.