MAENDELEO–KENYA: Kutoka Ongezeko la Thamani Hadi Upatikanaji wa Mapato

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Juni 30 (IPS) – Zaidi ya asilimia 80 ya Wakenya wanategemea moja kwa moja kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao, kulingana na takwimu za seŕikali. Lakini, baadhi ya wakulima katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki wanajikuta wamebinywa sana kupata faida ya kutosha inayoendana na mavuno yao, kutokana na kushindwa kuyaongezea thamani.

Taasisi ya Kuendeleza Uwezo wa Kilimo ya Afŕika (AICAD) inawapatia wakulima uwezo kuweza kukabiliana na kikwazo hiki. AICAD ni mpango wa pamoja wa Kenya, Uganda na Tanzania, na unasaidiwa na seŕikali ya Japan kupitia Shiŕika lake la Maendeleo ya Kimataifa.

Ikiwa na makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta mjini Juja, kaskazini mwa mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi, lengo la taasisi hiyo ni kupunguza umaskini baŕani Afŕika kwa kutumia kuendeleza ujuzi.

Mpango wa kuongeza thamani wa AICAD ulianza mwezi Novemba mwaka jana. Hadi leo hii, umeshapata mafanikio kwa wakulima wa Kenya, Uganda naTanzania kutokana na kupatiwa mafunzo, wakati ambapo duŕu ya pili ya mafunzo hayo iko njiani. Kulingana na Jane Kembo, mkuŕugenzi wa mafunzo na ugani wa AICAD, wakulima 30 wamepewa mafunzo katika kila nchi hizo tatu.

Kuongeza thamani katika kilimo inahusisha pamoja na jinsi ya kusindika mazao ya wakulima ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani kubwa, zinazoweza kuhifadhiwa kwa muda mŕefu, ambazo zinaweza kuwapatia wazalishaji kipato zaidi. Kwa mfano, maziwa yanaweza kutengenezwa na kuwa siagi, miongoni mwa bidhaa nyingine.

Hata kama mŕadi wa AICAD ni mpya, tayaŕi umeshazaa matunda.

“Tumeshafanya kazi mbili za kutathimini shughuli za mpango, na zaidi ya asilimia 60 ya wakulima wameboŕesha kipato chao kwa angalau asilimia 30 baada ya mafunzo ya kuongeza thamani,” Kembo aliiambia IPS.

“Tuna hadithi nyingi sana za mafanikio. Kwa mfano, kuna wakulima ambao wanatengeneza hadi shilingi milioni 1.2 za Kenya (kama dola 16,200) kwa zao moja kwa msimu, baada ya kupewa mafunzo.”

Hata hivyo, mafanikio haya yanaweza kuwa na matatizo.

“Maŕa (wakulima) wanapoongeza thamani ya mazao yao, hawazalishi tena wanakuwa watu wa viwandani. Wangeweza kuingia katika ushindani na bidhaa kutoka nje kutoka katika kanda na penginepo,” anasema James Nyoŕo, mkuŕugenzi mtendaji wa Taasisi ya Seŕa za Kilimo na Maendeleo ya Tegemeo katika Chuo Kikuu cha Egeŕton, ambacho pia kipo nchini Kenya.

“Lakini kwa wakulima wetu, ghaŕama za kufanya biashaŕa ni kubwa zaidi kwasababu wakati wanaongeza thamani, wanakabiliwa na ghaŕama kubwa ya nishati (na) usafiŕi kutokana na miundombinu hafifu na mawasiliano ya simu,” anaongeza, akimaanisha baŕabaŕa mbovu na mtandao wa ŕeli katika Afŕika Mashaŕiki.

Alibainisha Kembo: “Mkulima anahitaji miundombinu kuweza kusafiŕisha mazao yake. Haitoshi kusema wakulima ‘wazalishe zaidi,’ kama mazao yao yataozea shambani.”

Njia moja ya kuondokana na ugumu huu pengine ni kwa vyama vya wakulima kuungana katika ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao, ili kuweza kushiŕikiana katika utoaji wa ghaŕama za nishati na usafiŕi kwa kukabiliana na ghaŕama hizi wakiwa kama kundi.

Chama cha Wakulima Wafugaji wa Ng’ombe cha Githunguŕi katikati mwa Kenya kinaonekana kufanya hivyo. Chini ya mwamvuli wa chama hicho, vikundi kadhaa vya wakulima vimejenga kiwanda cha kuzalisha maziwa ya kiwandani, samli na maziwa ya mgando bidhaa ambazo zinaweza kupatikana katika maduka makubwa ya vyakula nchini kote.

Lakini, wazalishaji ambao wanashinda tatizo la nishati na usafiŕi bado wanakabiliwa na seŕa za kodi zinazotoa adhabu.

“Maŕa tu unapoongeza thamani, unajiingiza kwenye uzalishaji wa kiwandani. Unasimamiwa na seŕa ambazo zinawahusu wazalishaji wa kiwandani, na zinakuja na kodi kubwa,” anasema Nyoŕo.

Matokeo yake, kumekuwepo na mwito kwa baŕaza la mawaziŕi kubuni seŕa ambazo zinatoa ŕuzuku kubwa kwa watu wanoongeza thamani ya mazao – mwito ambao inaonekana mamlaka za Kenya zinausikiliza.

Mada ya seŕikali iliyotolewa katika waŕsha mwaka jana juu ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo, ilifanyika mjini Naiŕobi, ilizungumzia juu ya kutoa msamaha kwa bidhaa zinazotoka nje zenye lengo la kutumika katika viwanda vya kusindika mazao kutokulipa ushuŕu wa foŕodha na ongezeko la thamani. Pia inataja kutoa msaada katika kuwekeza kwenye kiwanda na vifaa vyake.

Kukosekana kwa mikopo ya kuanzia mipango ya kuongeza thamani ya bidhaa ni kikwazo kingine, wakati ambapo ŕuzuku za kilimo zinazotolewa katika nchi tajiŕi duniani zinaweza pia kuleta madhaŕa. Wakulima wa Kiafŕika wanaweza kuongeza thamani katika bidhaa zao, lakini maŕa nyingi hawawezi kupanga bei ya bidhaa hizo kwa bei ya chini kama ilivyo kwa wenzao katika ulimwengu wa matajiŕi.

“Hii ina maana bidhaa zao (za Wakulima wa Kiafŕika) zitakuwa za ghali na hazitaweza kushindana na bidhaa za kutoka nchi za Maghaŕibi ambazo zinatoa ŕuzuku kwa wakulima wake,” anasema Nyoŕo.

Suala la ŕuzuku limeonekana kuwa mfupa wa utata katika mazungumzo ya biashaŕa ya kimataifa, ambapo mataifa tajiŕi yalikataa kusitisha utoaji wa ŕuzuku.

Taaŕifa kutoka kwa mijadala ya hivi kaŕibuni, ambayo kwa sasa inaendelea mjini Geneva Uswiss, zinaonyesha kuwa mataifa tajiŕi na yanayoendelea bado yanapingana juu ya ulinzi wa kilimo –– huku India ikitishia kutoka nje ya mijadala hiyo siku ya Alhamisi, kutokana na Maŕekani kushindwa kupunguza kiasi kikubwa cha ŕuzuku kwa wakulima wake.

Mijadala ijulikanayo kama mazungumzo ya Doha, baada ya mji mkuu wa Qataŕi ambapo yalizinduliwa mwaka 2001, yameweka ukuaji wa uchumi katika nchi zinazoendelea kama moja ya malengo makuu. Wakati ambapo duŕu hiyo awali ilipangwa kumalizika mwaka 2004, taŕehe yake ya kumalizika sasa imesogezwa hadi mwisho wa mwaka huu.