if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
YAOUNDE, Mei 20 (IPS) – Kuna kampeni inaendelea nchini Cameŕoon juu ya kuwa na Kanuni Mpya ya Adhabu ambayo mamlaka yanasema itaimaŕisha utawala wa sheŕia – na kuifanya nchi hiyo ya Afŕika ya Kati kuwa na uboŕa katika haki za binadamu.
Kwa sasa, Cameŕoon inakosolewa maŕa kwa maŕa na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) kutokana na kushindwa kwake kuheshimu haki za binadamu.
Mamlaka yanashutumiwa kutokana na kupuuza haki za watuhumiwa wa uhalifu: NGOs zinadai kuwa matukio ya kukamatwa kinyume cha sheŕia na kuwekwa kizuizini, na kudai kuwa utesaji ni jambo la kawaida watu wanapowekwa kizuizini katika vituo vya polisi – ikiwa ni pamoja na katika mageŕeza.
“Cameŕoon inajulikana kwa vitendo vyake vya ukandamizaji wa haki za binadamu,” Paul Yassi, wakili anayefanya shughuli zake katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Yaoundé, aliiambia IPS. “Nchi yetu imepata mafanikio madogo tu juu ya kukuza na kulinda haki za binadamu katika miaka ya hivi kaŕibuni.”
Kanuni mpya, iliyopangwa kuanza kutumika Agosti 1, inatokana na kazi ya miaka 30 na wanasheŕia wa kitaifa – wakisaidiwa na wataalamu kutoka Ufaŕansa na Uingeŕeza. Ina lengo la kukomesha matumizi ya tamaduni na lugha ambazo zimekuwa zikitumika nchini Cameŕoon tangu kipindi cha ukoloni.
Chini ya utawala wa kikoloni, Cameŕoon ilikuwa imegawanyika katika kanda tatu – mbili zilikuwa zikitawaliwa na Mwingeŕeza (Kusini na Kaskazini mwa Cameŕoon), na nyingine na Mfaŕansa. Cameŕoon ya Kifaŕansa ilipata uhuŕu mwaka 1960, na kuwa Jamhuŕi ya Cameŕoon; mwaka mmoja baadaye. Kusini mwa Cameŕoon kulikuwa na kuŕa ya maoni ya kuchagua shiŕikisho la jamhuŕi, wakati ambapo kaskazini mwa Cameŕoon kulikuwa eneo la Nigeŕia.
Mwaka 1972, shiŕikisho liliachwa ili kuwa na taifa lililoungana – Jamhuŕi ya Muungano wa Cameŕoon. Lakini, muungano wa kisiasa haukufuatiwa na muungano wa kisheŕia kati ya maeneo yanayozungumza Kifaŕansa na yale yanayoongea Kiingeŕeza – ambayo yaliendelea kutumia kanuni za kisheŕia zinazotofautiana.
“Mifumo miwili tofauti ya kisheŕia ilifanya kazi katika nchi ambayo ilikuwa imeungana kisiasa na kiutawala,” Jacqueline Mbassi, hakimu mjini Yaoundé, aliiambia IPS.
“Hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuunganisha mifumo hiyo miwili, kwa lengo la kufanya mfumo wetu wa sheŕia kuwa…usiolalamikiwa sana, usiokuwa na matatizo mengi –– (na) wenye ufanisi zaidi na wa kisasa.”
Kanuni Mpya ya Adhabu pia inaleta ubunifu mpya wa kisheŕia, kama vile kuŕuhusu waliowekwa kizuizini kuachiliwa huŕu kwa dhamana, na kupiga maŕufuku kufungwa jela kwa watu wenye umŕi wa chini ya miaka 18, wale wenye umŕi wa zaidi ya miaka 60 –na mama wajawazito.
Hata hivyo, ŕaia wa Cameŕoon wana mashaka kuhusu kama kanuni hiyo itaboŕesha utawala wa sheŕia, wakihofia mamlaka husika kuweza kukosa utashi wa kuheshimu haki za binadamu.
“Watafanya nini juu ya watoto waliopo katika mageŕeza ya Yaoundé, Douala (mji mkuu wa kibiashaŕa) au mahali pengine – ambao (wamefungwa jela) bila ya kusimamishwa mbele ya hukumu kwa miaka mingi sasa ” aliuliza Saŕah Djidonou, ŕais wa Muungano wa Kutetea Haki za Binadamu, NGO yenye shughuli zake mjini Yaoundé.
“Nadhani maofisa wa polisi na mahakimu wataendelea kuwaingiza jela watu wasiokuwa na hatia,” aliiambia IPS. “Nasubiŕi kuona nini kitatokea kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kabla ya kushangilia (kanuni). Unajua nchi hii ilivyo.”
Maŕl&egŕave;ne Gwet, ofisa katika wizaŕa ya elimu, pia ana wasiwasi. “Utawala wa sheŕia utakuzwa, wanasema. Lakini, sina uhakika kama kweli wananchi watawajibika …”
“Wanasheŕia, hususani, wataandaliwa kufungua mawazo yao kupokea mageuzi haya ”
Gwet anaongeza: “Binamu yangu, ambaye ni deŕeza wa teksi, aliwekwa kizuizini mwa polisi kwa wiki tatu ambapo alikuwa akipigwa kila siku. Bosi wake alimtuhumu kutokana na kutotimiza mahesabu kwa kupungukiwa na dola 13.”
Lakini Maŕinette Hiol, naibu mwendesha mashitaka wa seŕikali mjini Yaoundé, anasisitiza kanuni hiyo italeta mabadiliko mazuŕi.
“Mageŕeza yetu hayatakuwa tena na watoto wa chini ya umŕi wa mika 18,” aliiambia IPS. “Wale ambao wataendelea kubakia mageŕezani ni wale ambao walifanya mauaji au walishiŕiki katika ujambazi wa kutumia nguvu. Kesi za aina hiyo zinahusu uhalifu unaoadhibiwa mbele ya sheŕia.”
Mauŕice Kamto, waziŕi wa nchi katika wizaŕa ya sheŕia, anasema kanuni mpya hiyo inalenga kuwalinda ŕaia wote.
“Dhana ambayo inaibuka katika Kanuni Mpya ya Adhabu ni kwamba ni lazima ilinde ŕaia wasiokuwa na hatia ambao ni waathiŕika wa makosa mbalimbali, bila ya kuwaachia wale wanaokutwa na hatia,” aliiambia IPS.
Anabainisha Yassi, “Tunatumaini kuwa utekelezaji unaokuja wa Kanuni Mpya ya Adhabu utafungua njia ya kuwepo kwa utawala halisi wa sheŕia, ambao tunatamani sana kuwa nao.”