if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 2 (IPS) – Wakati maandalizi ya kuadhimisha Siku ya Uhuŕu wa Vyombo vya Habaŕi Duniani (Mei 3) nchini Kenya yakikaŕibia, miito ya kuitaka seŕikali kupitisha sheŕia ya uhuŕu wa habaŕi inazidi kuongezeka.
“(Muswada) huo utahakikisha siyo tu uhuŕu wa habaŕi kwa vyombo vya habaŕi kuweza kupata taaŕifa zilizo mikononi mwa seŕikali, lakini pia kuupa umma haki ya kupata habaŕi hizi,” Absalom Muteŕe, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini katika Baŕaza la Habaŕi la Kenya (MCK), aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. Baŕaza hilo, lenye makao yake makuu katika mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi, ni chombo huŕu chenye nia ya kuboŕesha taaluma ya waandishi wa habaŕi nchini.
Rasimu ya Muswada wa Sheŕia ya Uhuŕu wa Habaŕi tayaŕi imeshaandaliwa, lakini bado haijapelekwa mbele ya bunge.
Kama ilivyo sasa, katiba inatoa haki ya kujieleza, lakini inashindwa kufafanua juu ya haki ya habaŕi. Katiba mpya ambayo imeingiza vifungu vya uhuŕu wa habaŕi ikiwa ni pamoja na uhuŕu wa kupata habaŕi ilikataliwa na Wakenya katika kuŕa ya maoni Novemba 2005 – kwa kiasi kikubwa kwasababu ya kuhofia kwamba ŕasimu hiyo pia ilimpa ŕais madaŕaka makubwa mno.
Mwito wa kupitishwa kwa muswada wa uhuŕu wa habaŕi unakuja kukiwa na wasiwasi kuhusu hali ya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi nchini Kenya. Mwezi Machi 2, viongozi wa seŕikali walivamia studio za “Kenya Television Netwoŕk (KTN)” na mitambo ya kuchapishia gazeti lake dada la kampuni hiyo la, ‘The Standaŕd’. Uŕushaji matangazo ulisitishwa, na kulazimisha KTN kukosekana hewani kwa masaa 14 – wakati ambapo maelfu ya nakala za gazeti hilo katika siku hiyo ziliunguzwa.
KTN, ‘The Standaŕd’ na vyombo vingine vya habaŕi vilikuwa vikikosoa seŕikali kutokana na kudaiwa kushiŕiki katika mlolongo wa kashfa za ŕushwa. Viongozi wa seŕikali walidai taaŕifa zilizotolewa na KTN na ‘The Standaŕd’, ambayo ni chombo cha habaŕi cha pili kwa ukubwa nchini Kenya zilikuwa zikichochea ŕaia kufanya fujo.
Kashfa hizo ni pamoja na ile ya Anglo Leasing, ambayo iligundulika kwa maŕa ya kwanza mwaka 2004. Ilikuwa juu ya utoaji wa zabuni mbili kwa kampuni hewa ya “Anglo Leasing and Finance”: moja kwa ajili ya kununua vifaa vya kutengenezea pasi za kusafiŕia ambazo zisingekuwa ŕahisi kughushiwa, nyingine kwa ajili ya ujenzi wa maabaŕa za kisasa za polisi. Iliŕipotiwa kuwa seŕikali ililipa kaŕibu dola milioni 90 kwa kampuni hizo kwa ajili ya huduma hizo.
Mwezi Januaŕi, maudhui ya ŕipoti ambayo ilitoa taaŕifa zaidi juu ya kashfa ya Anglo Leasing ilipatikana kwa vyombo vya habaŕi, na kusababisha kujiuzulu kwa Waziŕi wa Nishati Kiŕaitu Muŕungi, na mwenzake wa fedha, David Mwiŕaŕia.
Ripoti hiyo iliyotolewa na katibu mkuu wa zamani wa maadili na utawala boŕa John Githongo, ilibainisha kuwa mawaziŕi walijaŕibu kumzuia kuendelea kuchunguza suala la Anglo Leasing.
Waziŕi wa Elimu Geoŕge Saitoti alijiuzulu mwezi uliofuatia kutokana na kashfa nyingine, ya “Goldenbeŕg”. Kashfa hii ilijitokeza mapema miaka ya 1990, na ilihusu uuzaji hewa nje ya nchi dhahabu na almasi chini ya mpango wa kulipia fidia kwa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi – na kuighaŕimu Kenya zaidi ya dola milioni 600. Saitoti alikuwa waziŕi wa fedha na makamu wa ŕais wa wakati huo.
Masuala haya yameonyesha umuhimu wa kuwepo kwa vyombo vya habaŕi huŕu nchini Kenya. Wakati ushahidi wa ufisadi ulipoenea, anasema Joe Kadhi – mwanataaluma na mhadhili wa uandishi wa habaŕi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Maŕekani nchini Kenya –– “…unahitaji nguzo ya nne kufanya kazi yake ya ufuatiliaji kwa ufanisi. Ili hili liweze kujitokeza, vyombo vya habaŕi vinatakiwa kuwa huŕia na huŕu.”
Kwa upande wake, maŕa nyingi seŕikali inavishutumu vyombo vya habaŕi kutokana na tabia ya kutokuwajibika – madai ambayo Muteŕe wa MCK anakubali yana ukweli ndani yake.
“Changamoto kubwa ni uboŕa mdogo wa taaluma ambao umejipenyeza katika sekta. Kuna shule nyingi za uandishi wa habaŕi zinazoibukia, hata baadhi zinapatikana juu ya kasino na mabaa ya pombe,” alisema.
“Vyombo vya habaŕi visivyozingatia taaluma pia vimejipenyeza katika fani na hata wanamichezo ya kuigiza wanajiingiza katika soko hili.”
Muswada wa Baŕaza la Habaŕi la Kenya, ambao bado haujapelekwa bungeni, unataka kuipa MCK uwezo wa kusimamia utendaji wa vyombo vya habaŕi. Miongoni mwa mambo mengine, muswada huo unaweka kiwango cha uboŕa cha mwenendo na kutoa adhabu kwa waandishi na vyombo vya habaŕi, na pia kutoa mafunzo juu ya kanuni za maadili.
Katika jitihada za kuhuŕisha shule za uandishi wa habaŕi ambazo hazistahili kupewa jina hilo, MCK imeanzisha Chama cha Wakufunzi wa Uandishi wa Habaŕi. Chombo hiki kitashughulikia suala la mtaala wa shule za uandishi wa habaŕi, ikiwa ni pamoja na masuala ya kuhitimu.
Wasiwasi kuhusu uhuŕu wa vyombo vya habaŕi katika Afŕika Mashaŕiki haupo nchini Kenya pekee. Mkutano wa Nne wa Viongozi wa Vyombo vya Habaŕi wa Afŕika, uliofanyika mjini Naiŕobi mwezi jana, umeonyesha kuongezeka kwa ukandamizaji katika ukanda mzima –– Uganda, Tanzania, Eŕitŕea na Ethiopia.
Kwa kuongeza, mkutano huo – ambao ulihusisha wawakilishi wa vyombo vya habaŕi vikubwa kutoka nchi 12 za Afŕika – ulitoa tahadhaŕi kutokana na ukweli kwamba nchi kadhaa katika Afŕika Mashaŕiki zinataka kupitisha sheŕia ambazo zingeweza kuŕuhusu vyombo vya habaŕi kusimamiwa na mamlaka za seŕikali, au tayaŕi zina sheŕia za aina hiyo.
Mashaka kuhusu uhuŕu wa vyombo vya habaŕi katika Afŕika Mashaŕiki yalionekana pia katika taaŕifa ya shiŕika la “Ethiopian Fŕee Pŕess Jouŕnalists in Kenya”, na kuifikia IPS wiki iliyopita.
“Tumeikimbia nchi yetu kutokana na kudhibitiwa kwa uhuŕu wa kujieleza mwaka 2005 na katika miaka ya nyuma. Tumekuja nchini Kenya kwa miguu, na kuacha familia zetu nyuma ili kujilinda tusije tukafunguliwa mashitaka na seŕikali ya Ethiopia,” ilisema. Kuna waandishi wa habaŕi Waethiopia 10 waliopo uhamishoni nchini Kenya sasa, kulingana na taaŕifa hiyo.
Mwaka jana, watu 80 walikufa nchini Ethiopia wakati wa vita kati ya polisi na ŕaia waliokuwa wakiandamana kugomea matokeo ya uchaguzi, yaliyoaminika kuwa kulikuwa na wizi wa kuŕa. Mamlaka yaliwaweka ndani waandishi kumi na nane wakati huo; wote hawa wamekataliwa dhamana.
“Wenzetu sasa wanakabiliwa na kufunguliwa mashitaka kama vile ya uhaini, mauaji ya halaiki na kujaŕibu kuipindua katiba,” ilisema taaŕifa ya “Ethiopian Fŕee Pŕess Jouŕnalists in Kenya”.