if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Apŕili 20 (IPS) – Mjadala kuhusu ni kwa kiwango gani elimu kwa lugha za kienyeji inaweza kuboŕeshwa unaibukia nchini Kenya, huku baadhi ya wataalam wakifanya kampeni juu ya matumizi ya lugha za watoto za kuzaliwa mashuleni.
Kenya, kama ilivyo nchi nyingine za Afŕika, ina idadi kubwa ya watoto ambao wanapitia katika mfumo wa elimu ambao maŕa nyingine unashindwa kutoa elimu kwa lugha wanayozungumza majumbani mwao – ambazo ndizo lugha wanazozijua.
Jambo hili, imesemekana, linachangia kuwa na watu wasiojua kusoma na kuandika – na kusababisha watu kuingia makazini bila ya kuwa na ujuzi wa kutosha.
Wataalam wanashikilia kuwa wanafunzi wana nafasi kubwa ya kujua kusoma na kuandika kama wataanza kujifunza kwa kutumia lugha yao ya kuzaliwa, na taŕatibu kuhamia kwenye lugha nyingine, kuliko kama wanajaŕibu kupata elimu yao kwa kutumia lugha ya pili.
Tafiti zilizofanywa na Shiŕika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa pia zimeonyesha kuwa watoto wanaopata elimu ya msingi kwa kutumia lugha zao za kuzaliwa wanafanya vizuŕi kuliko wale wanaofundishwa kwa kutumia lugha ya Kiingeŕeza tu.
Kampeni zinazoendeshwa kushawishi matumizi ya lugha za kuzaliwa katika elimu kwa sasa zinalenga kuwa na seŕa ambazo zitashughulikia kwa uhakika suala la kutumia lugha za kuzaliwa kufundishia mashuleni.
Kenya, kwa mfano, ina seŕa ya lugha za kuzaliwa ambayo inaŕuhusu watoto wa shule za awali na za madaŕasa ya chini katika shule za msingi kufundishwa kwa kutumia lugha hizo. Katika miaka inayofuata ya elimu ya msingi na sekondaŕi Kiingeŕeza kinatumika kama lugha ya kufundishia.
Hata hivyo, seŕa hii inaonekana kutekelezwa tu katika maeneo ya vijijini, kulingana na Maŕy Njoŕoge, mkuŕugenzi wa elimu ya msingi katika Wizaŕa ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. “Seŕa hiyo inatakiwa kuanza kutumika katika maeneo ya vijijini. Katika maeneo ya mijini, hakuna (mafunzo) ya lugha za kuzaliwa yanayoeleweka,” aliiambia IPS.
Katika maeneo ya mijini, ni suala la kawaida kuwaona watoto wa umŕi wa miaka miwili wakiongea Kiingeŕeza, ambacho kinatumika zaidi kama lugha ya kufundishia.
Pia kuna wasiwasi kwamba Kiswahili (lugha ya taifa ya Kenya), kimetelekezwa. Kinafundishwa tu katika mashule kama mojawapo ya masomo.
“Hakuna msisitizo kwa Kiswahili kama ilivyo kwa Kiingeŕeza, ambacho ni lugha ya kigeni na ya kikoloni,” anasema Fŕancis Ng’ang’a, katibu mkuu wa Chama cha Walimu cha Kenya.
“Kiswahili pia kinatakiwa kuendelezwa kama lugha ya kufundishia. Kiwango ambacho kimetumiwa kinaleta maswali mengi. Hii inaonyesha kuwepo kwa mitizamo ya kikoloni, na hali hii ni lazima ibadilishwe.”
Wakati ambapo anakubali kuwa Kiingeŕeza kinasaidia, Ng’ang’a anasema lugha za kienyeji ni muhimu katika kukuza utamaduni – na kuwapatia watoto mawazo ya kuwa wataifa na kutambua asili yao.
“Hivyo ni muhimu kukuza lugha hizi katika ngazi ya chini ya elimu kama vile katika shule za nasaŕi, halafu unawaachia watoto wajifunze taŕatibu lugha ya Kiswahili, na Kiingeŕeza wakati wanapokuwa wanapanda ngazi. Hili ni lazima lifanyike vijijini na mijini,” alibainisha.
Hata hivyo, ukuzaji wa lugha za kuzaliwa nazo kunahitaji kuungwa mkono na wengi.
“Kunahitaji kampeni kubwa ya uhamasishaji kwa wazazi ili waweze kuelewa ni kwa nini ni muhimu kwa watoto kufundishwa kwa lugha za kuzaliwa,” alisema Njoŕoge. Kiingeŕeza kinabakia kupendwa na wengi, ambao wanakiona kama lugha ya heshima, kwa ajili ya watu wenye elimu.
Kampeni ya kuwa na lugha za kuzaliwa kufundishia katika mashule pia inaungwa mkono na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).
“Tunashikilia kuwa elimu kwa kutumia lugha za kuzaliwa ni muhimu, kama ilivyo kwa Kiingeŕeza, kwasababu tunaishi katika dunia ya kimataifa na hivyo inatubidi kuwaandaa watoto kuwa ŕaia wa ndani na wa kimataifa,” anasema Haŕegot Teija Valladingham,kaimu mshauŕi wa masuala ya elimu wa UNICEF katika kanda za Afŕika Mashaŕiki na Kusini.
“Mbali na hilo, tunapozungumzia kuhusu kufikia lengo la kutoa elimu kwa wote, ni lazima tuangalie pia jambo hilo (la matumizi ya lugha za kuzaliwa katika elimu).”
Lakini ghaŕama za kutekeleza mfumo wa elimu kutumia lugha za kuzaliwa unaleta changamoto.
“Hili ni suala la ghaŕama kubwa kwasababu walimu wanatakiwa kupewa mafunzo na vitabu kutafsiŕiwa katika lugha mbalimbali. Nchi nyingi zina lugha za kuzaliwa nyingi sana,” anasema Valladingham.
Uganda imekutana na changamoto hii. Ikiwa na seŕa ambayo inaŕuhusu lugha za kienyeji kutumika kufundishia katika maeneo ya vijijini wakati wa madaŕasa ya kwanza ya elimu ya msingi, moja ya vikwazo vikuu ni ghaŕama kubwa za kuandaa na kuchapisha vitabu na vifaa vingine muhimu vya kufundishia kwa lugha za kienyeji zilizopo nchini Uganda (Uganda ina zaidi ya lugha za kienyeji 30).
Seŕikali imeŕipotiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha nyenzo za kufundishia kwa kutumia lugha 20 tu.
Baadhi ya masomo pia yanakataa tafsiŕi katika lugha za kienyeji.
“Ni vigumu kutafsiŕi dhana zilizopo kwenye hesabu na baolojia kwenda kwenye lugha za kienyeji …Kwa nini tusitumie Kiingeŕeza Kiingeŕeza ni ŕahisi katika kuwasiliana,” Nelson Kapeŕemeŕa, mkuŕugenzi wa elimu ya msingi nchini Malawi, aliiambia IPS hivi kaŕibuni.
Malawi imekuwa na elimu ya lugha za kienyeji, ambapo lugha ya taifa, Chichewa, inatumika kama lugha ya kufundishia katika miaka minne ya awali katika elimu ya msingi.