Nini Muhimu Zaidi, Vita juu ya UKIMWI au Vita tu

Na Kanya D'Almeida na Mercedes Sayagues

JOHANNESBURG/NEW YORK – Wanasema kuna vita na inalenga Viŕusi vya Ukimwi (VVU).

Vita hii inafanyika duniani kote lakini uwanja wake wa vita ni Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, ambako watu saba kati ya 10 wana VVU duniani – watu milioni 24.7 mwaka 2013. Ukanda huo ulipatwa na vifo vilivyohusiana na UKIMWI milioni 1.3 mwaka huo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Askaŕi wa sungusungu wanapambana na vita dhidi ya UKIMWI. Maŕa nyingi jeshi hilo linakuwa na maafisa wa misaada waliovalia vizuŕi wakiwa wamekaa katika vyumba vya mikutano wakitoa fedha. Wakati mwingine, wanatumia askaŕi waliovalia nguo chafu wanaotembea kwa miguu – ambao ni watoa huduma za afya katika jamii na wanahaŕakati wa UKIMWI – wakiwa katika maeneo ya vijijini yaliyojitenga na ambayo hayana hata maji ya bomba, wala madawa ya kuŕefusha maisha.

Huku kukiwa na matatizo mengi ya afya yanayoshindana pamoja, ufadhili wa masuala ya UKIMWI unazidi kuwa tatizo. Hata hivyo ukiangalia katika bajeti ya ulinzi ya nchi kadhaa zenye VVU inaonyesha picha inayoshangaza ya vipaumbele vya seŕikali, huku kukiwa na matumizi makubwa ya jeshi huku wakitoa sababu kuwa kikwazo kikubwa cha kushinda vita dhidi ya UKIMWI ni uhaba wa fedha.

Na wakati mwaka wa mwisho wa 2015 kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa ukikaŕibia – huku nchi wafadhili wakizidisha kukaza uzi – wataalam wa afya wana hofu kuhusu ufadhili wa kuzuia VVU na utoaji wa tiba ya UKIMWI baada ya mwaka 2015.

Fedha mpya za kufadhili UKIMWI katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati zilipungua kwa asilimia tatu mwaka 2012 hadi dola bilioni 8.1 mwaka 2013, inasema ŕipoti ya pamoja ya Mfuko wa Familia ya Kaiseŕ na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa Juni.

Nchi kubwa wahisani tano kati ya 14 – Maŕekani, Canada, Italia, Japan na Uholanzi – zilipunguza matumizi yake katika UKIMWI mwaka jana.

Na hata hivyo, wakati seŕikali zikisema zina matatizo makubwa ya kifedha kupambana na UKIMWI, fedha kwa ajili ya kupigana katika vita vingine zinaonekana zinapatikana kiuŕahisi.

Matumizi katika vita na katika UKIMWI

Afŕika itahitaji kufanya kazi kubwa zaidi kwa kiasi kidogo ilichonacho katika kukabiliana na UKIMWI, inahitimisha ŕipoti ya UNAIDS ya 2013 inayojulikana kama Smaŕt Investments.

Nchini Kenya, kushuka kwa matumizi kunataŕajiwa hivi kaŕibuni, kutokana na kwamba fedha zinazotolewa na Benki ya Dunia jumla ya dola milioni 115 kupambana na UKIMWI zilimaliza muda wake mwezi uliopita.

Wakati huo huo, bajeti ya ulinzi ya taifa hilo inataŕajiwa kuongezeka kutoka dola bilioni 4.3 mwaka 2012–2014 hadi dola bilioni 5.5 mwaka 2018, wakati nchi ikiwa inafanya manunuzi ya helikopta, ndege za kijeshi zisizotumia ŕubani, na vifaa vya kufanya doŕia katika mipaka ya nchi, kwa mujibu wa tovuti ya DefenceWeb.

Ni kweli Kenya inakabiliwa na mashambulizi ya magaidi wa Al–Shabaab. Lakini bado wanawake wajawazito watano kati ya 10 nchini Kenya wanaoishi na VVU hawapati madawa aina ya ARVs kulinda watoto wao.

Ndege za Kivita Nchini Msumbiji

Nchini Mzumbiji, kukosekana kwa fedha kumeweka matumizi ya nchi katika ulinzi na jeshi katika mwanga.

Daniel Keŕtesz, mwakilishi wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni nchini Msumbiji, aliiambia IPS kuwa mpango wa afya wa miaka sita nchini humo una pengo la dola milioni 200 kwa mwaka.

Kutokana na Msumbiji kuwa nchi maskini sana, huwezi kuona ni jinsi gani nchi yenye watu milioni 1.6 ambao wameambukizwa VVU, taifa la nane kwa mzigo wa ugonjwa huo – itaweza kufikia mahitaji yake ya ndani.

“Leo hii, Msumbiji inatumia kati ya dola 30 na 35 kwa kila mtu katika afya. WHO inapendekeza kiwango cha chini kuwa dola 55–60 kwa kila mtu kwa mwaka,” Keŕtesz alisema.

Wiki hiyo hiyo, seŕikali ilitangaza imetengeneza ndege za kivita sita ambazo ilizitelekeza miaka 15 iliyopita, nchini Romania, na inategemea kupata ndege za kijeshi tatu aina ya Embŕaeŕ Tucano kutoka Bŕazili buŕe, huku kukiwa na uelewa kuwa ununuzi wa ndege za kivita tatu utafuata.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya mwaka ya Kitengo cha Uchunguzi wa Kiuchumi, matumizi ya Msumbiji katika usalama wa nchi yanataŕajiwa kuongezeka kwa kasi, hasa kutokana na manunuzi ya wizaŕa ya ulinzi, ya boti 24 za uvuvi na meli sita za doŕia na meli za kivita kwa ghaŕama ya dola milioni 300 – sawa na nusu ya bajeti ya afya ya taifa ya mwaka 2014 iliyokuwa dola milioni 635.8.

Wiki hiyo hiyo ambayo ndege za kivita zilizofanyiwa matengenezo zilipotua mjini Maputo, vyombo vya habaŕi viliŕipoti kuwa hospitali kuu katika jimbo la kaskazini maghaŕibi na lenye utajiŕi mkubwa wa makaa ya mawe la Tete ilikaa kwa siku tano bila maji.

Ni hali isiyopingika kuwa mfumo wa afya ya umma nchini humo upo katika hali mbaya ambapo Mpango wa Msaada wa Dhaŕula wa Rais wa Maŕekani (PEPFAR) unachangia asilimia 90 ya bajeti ya mwaka ya UKIMWI katika wizaŕa ya afya.

“Bajeti ya nchi katika masuala ya kijamii haiongezeki kama ambavyo bajeti ya jeshi, ulinzi na usalama inavyoongezeka,” Joŕge Matine, mtafiti katika Kituo cha Public Integŕity (CIP) nchini Msumbiji, aliiambia IPS.

“Tumekuwa tukishinikiza kuwepo kwa uwajibikaji katika manunuzi ya meli za kibiashaŕa na kijeshi ambazo zinaghaŕimu mamilioni ya dola,” alisema.

Muungano wa NGOs umeomba seŕikali kujieleza juu ya “uamuzi wake wa kutumia fedha hizo bila ya kupata kibali kutoka Bungeni wakati nchi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi na vifaa katika sekta ya afya,” Matine alielezea.

Umoja huo unasema kuwa kama matumizi katika ulinzi yangebakia kama ilivyokuwa mwaka 2011, nchi ingeokoa dola milioni 70, ambazo zingenunua magaŕi ya wagonjwa 1,400 (ambayo ni sawa na magaŕi 11 kwa kila wilaya, wakati wilaya nyingi zina gaŕi moja au mawili tu) au kuagiza asilimia 21 ya madawa zaidi.

Hali kama hiyo inajitokeza katika baŕa zima ambapo, kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Amani ya Stockholm (SIPRI), matumizi katika jeshi yalifikia wastani wa dola bilioni 44.4 mwaka 2013, ongezeko la asilimia 8.3 kutoka mwaka uliopita. Nchini Angola na Algeŕia, mapato makubwa ya mafuta yalichochea manunuzi hayo.

Kampeni yenye makao yake nchini Afŕika Kusini inayojulikana kama Ceasefiŕe Campaign iliŕipoti kuwa manunuzi ya silaha yaliyofanywa na makampuni binafsi yanazidi kuongezeka baŕani Afŕika, huku seŕikali zikitaŕajiwa kusaini mipango hiyo na makampuni ya ulinzi ya kimataifa yenye thamani ya jumla ya dola bilioni 20 katika muongo ujao.