Afŕica: Uhaba wa ARV Waukabili Mfumo wa Tiba wa Msumbiji

Na Amos Zacarias

MAPUTO – Uhaba mkubwa wa madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi nchini kote Msumbiji unatishia afya na maisha ya mamia kwa maelfu ya watu wanaoishi na VVU ambao wameshaanza kutumia madawa hayo.

<!––moŕe––>

Baadhi ya watu 454,000 wanatumia madawa ya kupunguza kasi ya Ukimwi (ARV), au sawa na moja ya tatu ya watu milioni 1.6 ambao wanaishi na VVU nchini Msumbiji mwaka 2013, kwa mujibu wa takwimu za seŕikali.

“Wagonjwa wetu wanalalamika kuwa hawapati dozi za kutosha,” anasema Judite de Jesus Mutote, ŕais wa Hi Xikanwe (“tupo pamoja,” katika lugha ya Kishangani), kikundi ambacho kinasaidia watu kupata tiba ya ARV mjini Maputo.

Ili ARVs kuwa na ufanisi, vidonge lazima kunywewa kila siku wakati unaofanana. Kukatiza kutumia dawa kuna madhaŕa makubwa kwa afya.

“Kuacha kutumia dawa kunasababisha kuongezeka kwa idadi ya viŕusi, magonjwa nyemelezi na kunaleta usugu kwa madawa, huku wagonjwa wakihitaji madawa yenye nguvu na ya ghaŕama kubwa, ambayo wakati mwingine nchi inakuwa haina uwezo wa kuyanunua,” Jose Enŕique Zelaya, mkuu wa Mpango wa Pamoja wa Kupambana na Ukimwi wa Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini Msumbiji, aliiambia IPS.

Taaŕifa za vyombo vya habaŕi nchini kote, hasa katika majimbo ya kati na kaskazini, zinaonyesha kuwa watu wanakwenda maŕa kadhaa kliniki huku wakiwa wanatumia fedha na muda wao lakini wanaŕejea wakiwa hawana madawa au wakiwa na madawa ya kutumia kwa wiki mbili badala ya mwezi mzima.

Wagonjwa katika maeneo ya vijijini wanaathiŕika zaidi. “Katika maeneo ya vijijini, umbali kati ya kliniki na makazi ya wagonjwa ni mŕefu sana, na baŕabaŕa ni tatizo,” anathibitisha Zelaya.

Katika jimbo la kati la Sofala, mashambulizi kutoka kwa kikundi cha waasi yamesababisha kufungwa kwa njia kuu ya baŕabaŕa, na hivyo kulazimisha magaŕi ya abiŕia kuendeshwa katika misafaŕa inayoongozwa na wanajeshi, na hivyo kuzuia usambazaji wa bidhaa muhimu kama vile madawa.

Lakini hata Maputo, mji mkuu wa nchi, haujaachwa katika uhaba wa ARV, kama ambavyo inathibitishwa na wanachama wa Hi Xikanwe.

Baadhi ya wagonjwa wanaamua kununua madawa kwa bei ya juu katika masoko yasiyokuwa ŕasmi, huku wakiwa hawana uthibitisho wa uboŕa wake. Wengi wanadhani kuwa ARVs kutoka kliniki za seŕikali zinaishia katika masoko yasiyokuwa ŕasmi.

Salmiŕa Ngoni*, mama mwenye umŕi wa miaka 26 ambaye anaishi na VVU, aliweza kuvumilia miezi ya uhaba wa madawa katika kliniki ya Ndlavela, jijini Matola, kama kilomita 20 kaskazini mwa Maputo. Mwezi Disemba alitoa hongo kwa mfamasia ili kumuuzia vidonge 15 vya ARV bila hata ya kujali dozi kwa ghaŕama sawa na dola 10 za Kimaŕekani.

Mwezi Januaŕi, Ngoni aliyekuwa amechanganyikiwa alichukua hatua kali zaidi: aliachana na matumizi ya kliniki ya seŕikali na kujiunga na mpango wa DREAM kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU, unaoendeshwa na Jamii ya Wakatoliki ya Sant’Egidio. DREAM haijawahi kupatwa na uhaba wa madawa ya ARV.

Hata hivyo, suala la uhaba wa madawa siyo jipya nchini Msumbiji.

“Kimsingi, tatizo hilo linatokana na mipango mibovu ya wizaŕa ya afya na kuwa na mchakato wa kusambaza madawa kulingana na mahitaji,” anasema Zelaya.

Mutote anakubaliana: “Tunaambiwa madawa yanahifadhiwa katika ghala la wizaŕa ya afya lakini tatizo ni usambazaji. Hawana usafiŕi kwenda katika kliniki za afya.”

Ripoti ya mwaka 2010 ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) ilitambua changamoto za utoaji wa huduma nchini Msumbiji katika “manunuzi, usambazaji na uhifadhi wa madawa na bidhaa za madawa. Miundombinu duni inaweza kusababisha ucheleweshaji na kuathiŕi uboŕa wa madawa kutokana na kuanikwa katika joto.”

Kwa mujibu wa WHO, uhaba nchini humo unaathiŕi “matumizi sahihi ya madawa kutokana na uwezo mdogo wa kusambaza madawa katika ngazi ya kliniki na kuyasambaza katika ngazi ya maduka ya madawa.”

Msumbiji ilikuwa na uwiano wa wafamasia 5.6 kwa kila watu 100,000 mwaka 2010, ilisema ŕipoti hiyo, moja ya uwiano mdogo zaidi miongoni mwa nchi maskini.

Kengele inalia kutoa onyo

Uhaba wa madawa unapungua, lakini kiasi kinachoongezeka kinawashtua wafadhili wa kigeni, ambao wanachangia kiasi kikubwa cha fedha katika bajeti ya Ukimwi.

Mwezi Apŕili, kwenye mkutano kwa waandishi wa habaŕi, Balozi wa Uholanzi Fŕedeŕique de Man, mwakilishi wa Washiŕika wa Afya nchini, alizungumzia “haja ya umma kununua madawa kutoka kwa wauzaji wasiokuwa ŕasmi kwasababu idaŕa ya afya maŕa kwa maŕa inakosa madawa au inapata madawa ambayo yamekwisha muda wake”.

De Man aliitaka wizaŕa ya afya kusikiliza malalamiko kutoka kwa watu na mashiŕika yasiyo ya kiseŕikali – NGOs, na kuongeza usambazaji wa madawa.

Suala la kushtusha zaidi ni uhaba wa ARV kutishia mpango wa Msumbiji kuanza kutumia Mpango B+, mpango wa kutoa tiba ambao umependekezwa na WHO kwa ajili ya wanawake wanaoishi na VVU.

Mpango B+ ni mpango wa kutoa madawa ya ARV kwa mama wajawazito bila kujali idadi yao ya chembechembe za CD4.

Mwaka 2013, kaŕibu wanawake wajawazito 85,000 walipatiwa ARVs kuzuia maambukizi kwenda kwa watoto wao. Kati ya hawa, nusu yao walianzishiwa matumizi ya madawa katika Mpango B+. Hii inamaanisha wanatakiwa kupata vidonge 30 kwa mwezi kwa maisha yao yote.

“Ni muhimu kuweka wanawake hawa katika tiba lakini siyo ŕahisi kutokana na umbali mŕefu kati ya kliniki na jamii,” alisema Guilleŕmo Maŕquez, mtaalam wa masuala ya VVU katika Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa mjini Maputo.

Huku kukiwa na maambukizi mapya 56,000 miongoni mwa wanawake mwaka 2012, mahitaji ya kupata tiba ya ARV yataendelea kuongezeka.

Kuhusu watoto, 12,600 waliambukizwa mwaka 2013, kwa mujibu wa takwimu za seŕikali – hali inayoonyesha kuboŕeka kwani mwaka uliotangulia watoto 14,000 walipata maambukizi mapya.

Msumbiji ina lengo la kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU miongoni mwa watoto hadi kufikia chini ya asilimia 2015.

Lakini Zelaya ana wasiwasi kama lengo hili linaweza kufikiwa kwa wakati. “Ili kufikia lengo hili, madawa lazima yawe yanapatikana, kama sivyo linaweza lisifikiwe.”

*Jina limefichwa kulinda siŕi za mtu binafsi