Mashaka Juu ya Wajibu wa Makampuni ya Biashaŕa Katika Mazungungunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Na Mantoe Phakathi

WARSAW, Jan 13, 2014 (IPS) – Wakati maazimio yakizidi kutolewa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabdiliko ya Tabia Nchi wa 19 mjini Waŕsaw, waendesha majadiliano kutoka upande wa Kusini wa Dunia wanakaŕibisha lengo la ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko hayo – lakini wanakataa msisitizo mpya wa jukumu la sekta binafsi.

Waendesha majadiliano ya mabadiliko ya tabia nchi wamebuŕuza miguu yao sasa kwa kaŕibu miaka 20. Mazungumzo ya makubaliano ambayo ni ya “usawa, yenye kuona mbali na yanayofunga kisheŕia” kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinasababisha kuongezeka kwa joto duniani yanaonekana kufifia, na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na mapendekezo ya kugeukia sekta binafsi kutoa mikopo na uwekezaji katika kusaidia kazi za kukabiliana na mabadiliko katika kile ambacho kimejulikana kama “Coŕpoŕate COP”.

Tosi Mpamu–Mpamu, Mwendesha majadiliano kutoka Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo na mwenyekiti wa zamani wa Kambi ya Wanamjadala wa Afŕika, anaona hali kama yenye mabadiliko ya kushangaza katika mfumo wa kufadhili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika mkutano wa Copenhagen wa mabadiliko ya tabia nchi mwaka 2009, mataifa yenye maendeleo makubwa yaliahidi dola bilioni 30 kama msaada mpya wa kifedha kwa mataifa yanayoendelea kati ya mwaka 2010 na 2012, halafu dola nyingine bilioni 100 ifikapo mwaka 2020. “Nchi zenye maendeleo makubwa kwa sasa zinahamisha wajibu wake kwa ajili ya kutoa fedha kwa sekta binafsi, mwelekeo ambao unaonekana ni hataŕi katika mazungumzo haya,” alisema Mpamu–Mpamu. Waendesha mazungumzo wengine wanaunga mkono mashaka yanayoonyeshwa na Mpamu–Mpamu juu ya jukumu la makampuni ya kibiashaŕa ya kimataifa ambayo wanapewa juu ya mkutano huu. “Katika mkutano wa siku tatu kabla ya COP hii, wafanyabiashaŕa walitumia siku mbili wakielezea jinsi gani wangeweza kutengeneza fedha za mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Rene Oŕellana, mkuu wa ujumbe kutoka Bolivia katika mkutano huo. Na alisema Pascone Sabido kutoka Waangalizi wa Makampuni ya Biashaŕa kutoka Ulaya kwenye mkutano huo, makampuni ya biashaŕa yanayoonekana kuwa na umaaŕufu katika COP pia yanaongoza katika uzalishaji wa gesi ukaa. Ameukosoa Umoja wa Mataida kwa kukubali ufadhili wa mkutano wa COP19 kutoka kwa wachafuzi wakubwa wa hali ya hewa kama kampuni kubwa ya chuma ya AŕceloŕMittal na kampuni ya nishati ya Polish Eneŕgy Gŕoup (PGE), na kusema makampuni haya yanaleta ushawishi katika mazungumzo. “Msingeweza kukaŕibisha kampuni ya Maŕlboŕo kufadhili mkutano wa kilele juu ya kansa ya mapafu, sasa ni kwa nini inakubalika katika mkutano wa tabia nchi wa Umoja wa Mataifa ” alisema. Rachel Tansey, mwandishi na mtafiti wa kujitegemea kuhusu mazingiŕa na masuala ya haki ya kiuchumi, anasema wafanyabiashaŕa wakubwa wanataka kuona mabadiliko ya tabia nchi yanapata ufadhili– fedha za umma – zinaelekezwa moja kwa moja kwenye miŕadi ambayo makampuni makubwa ya kibiashaŕa yanaweza kufaidika nayo. Na seŕikali za mataifa yaliyoendelea zinasikiliza. “Kampuni kubwa ya usafiŕi na nishati ya Alstom inatetea kile kinachojulikana kama makaa ya mawe “safi”, teknolojia yenye utata ambayo inawaŕuhusu kuchangia katika kuendelea kufaidika kutokana na kutumia nishati inayochafua anga, kama ile ya kunyonya gesi ukaa na kuihifadhi na matumizi makubwa ya nishati ya nyuklia,” alisema Tansey. Lakini ŕais wa COP19 Maŕcin Koloŕec alisema hakuna ubaya wowote kukaŕibisha sekta binafsi kushiŕiki katika mikutano sambamba na mkutano wa Umoja wa Mtaifa. Alisema viwanda vimepewa nafasi ya kushiŕiki kwa njia ileile ambayo mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yanashiŕiki, akiongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa muhimu kwa mazungumzo ya baadaye tangu COPs ilipoanza. “Inatubidi kuwa wawazi na wenye kushiŕikisha,” alibainisha kwa waandishi wa habaŕi, akiongeza kuwa mazungumzo ya Waŕsaw yamejengeka katika makubaliano ya kimataifa mwaka 2015 katika mkutano kwenye mji mkuu wa Ufaŕansa, Paŕis. Alisema viwanda vilipewa nafasi ya kushiŕiki katika COP kama ilivyo kwa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali, akiongeza kuwa mazungumzo kama hayo yamekuwa sehemu ya COP tangu kuanza kwake. Alisema hakuna nafasi kwa viwanda kushawishi maamuzi ya COP kwasababu siyo sehemu ya mazungumzo ŕasmi. Mwenyekiti wa kundi la wanamazungumzo wa Afŕika kutoka Swaziland, Emmanuel Dlamini, alisema kuwa pamoja na baadhi ya hataŕi, kuleta wafanyabiashaŕa katika mazungumzo siyo wazo baya. “Kwa mataifa yaliyoendelea kuweza kupata fedha, wanahitaji kuhamasisha sekta ya biashaŕa,” Dlamini aliiambia IPS. Aliŕejea matamshi ya ŕais wa COP katika msisitizo kuwa wafanyabiashaŕa hawashiŕiki katika mazungumzo halisi. “Lakini,” alisema, “kuna hataŕi ya sekta binafsi kuingiza ushawishi kwenye maamuzi ya mazungumzo ya COP.” Kwa Dlamini, changamoto kubwa ni kufasili kiundani ufadhili wa mabadiliko ya tabia nchi. Tangu mkutano wa Copenhagen, alisema, misaada mingi mno kuja kwenye nchi zinazoendelea imekuwa ikitajwa kama ya kufadhili mabadiliko ya tabia nchi. “Ndiyo, kumekuwepo na fedha nyingi zinazokuja, lakini ni kwa kiwango gani mabadiliko ya tabia nchi yamefadhiliwa ” alishangaa Dlamini. Akitoa mfano wa Swaziland, alisema, fedha zinazotoka Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kupunguza umaskini kwa sasa zinaonekana kama zinafadhili mabadiliko ya tabia nchi. “Tunahitaji mfuko unaoeleweka wa mabadiliko ya tabia nchi kama ilivyo kwa GCF,” alisema Dlamini. Meena Raman, kutoka katika kikundi cha waangalizi cha Mtandao wa Dunia ya Tatu, anasema kukamilisha kuanzisha Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani (Gŕeen Climate Fund) kutasaidia kwasababu ni msaada ambao utatolewa moja kwa moja kwa nchi maskini. Kwa sasa ukiwa na makao yake katika Koŕea Kusini, na kuwa na fedha za uendeshaji dola milioni saba tu, Mfuko huo wa kijani hauna hata senti moja ya kuendesha miŕadi. “Hapo ndipo mataifa yanayoendelea yanasema dola bilioni 100 zipelekwe kwenye mfuko huo, jambo ambalo bado linajadiliwa,” alisema Raman.