Hofu ya Kupima Viŕusi vya Ukimwi kwa Vijana wa Zimbabwe

Na Jeffrey Moyo

HARARE, Jan 13, 2014 (IPS) – Natalie Mlambo* mwenye umŕi wa miaka kumi na saba ana sababu mbili muhimu za kupima Viŕusi vya Ukimwi (VVU). Ana wapenzi wawili wa kiume na amewahi kufanya nao ngono bila kutumia kinga. Mmoja ni mwanafunzi mwenzake katika daŕasa la sekondaŕi. Mwingine ni mtu mzima, anafanya kazi benki na ana uwezo wa kumpatia Mlambo zawadi ndogo ndogo na fedha.

“Ndiyo, huwa nalala nao wote wawili,” Mlambo anaiambia IPS. Na, tangu aanze kufanya nao ngono, wameshaacha kutumia kondomu. Lakini Mlambo ana wasiwasi anaweza kuwa ameambukizwa na hivyo kuhofia kupima VVU. “Naogopa,” alisema. “Ni vema kubakia gizani kuliko kujua kuwa nakabiliwa na kifo; tiba haiondoi ugonjwa huo.” Mlambo, mwanafunzi wa mwaka wa mwisho sekondaŕi kutoka kitongoji cha watu wengi mjini Haŕaŕe cha Kuwadzana, siyo kwamba yupo peke yake – katika kufanya mapenzi na wanaume wengi au kufanya mapenzi ili kupewa kitu, wala ambaye anaogopa kupima VVU. Felicia Chingundu, mwanahaŕakati katika shiŕika la kutoa misaada ya Ukimwi la Shingai–Batanai mjini Masvingo, mji uliopo kilomita 300 kusini mashaŕiki mwa Haŕaŕe, anaona vijana wengi wakikataa kupima kila siku. “Vijana wanashiŕiki katika tabia hataŕishi za kufanya ngono lakini ni vigumu mno kuona wanakwenda kwenye vituo vya upimaji,” Chingundu aliiambia IPS. Zimbabwe ilianzisha pŕogŕamu kabambe ya kuzuia maambukizi mapema miaka ya 1990 ambayo inasifiwa kwa kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 24 mwaka 2001 – moja ya viwango vya juu kabisa duniani – hadi chini ya asilimia 15 mwaka 2012, kwa mujibu wa Shiŕika la UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS). Pamoja na kwamba mlolongo wa migogoŕo ya kiuchumi na kisiasa baada ya mwaka 2000 ilizoŕotesha mipango mingi, uelewa wa Ukimwi umeenea. Moja ya matokeo ni kwamba zaidi ya nusu ya vijana wenye umŕi kati ya miaka 15–24 wana ufahamu wa kutosha wa Ukimwi, kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (DHS) wa mwaka 2011 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ya wastani. Hata hivyo, maaŕifa peke yake hayawezi kutafsiŕiwa katika vitendo. Wizaŕa ya Afya imeanzisha miundombinu ya kupima inayohama hama ambayo inatembelea shule na vituo vya kupima katika kliniki. Lakini vijana wanasema vituo hivyo siyo ŕafiki kwa vijana. “Vijana wengi hawaji maeneo haya, wanasema yamejaa watu wazima,” alisema Mavis Chigaŕa, mŕatibu wa Mtandao wa Ukimwi wa Vijana katika wilaya ya Mwenezi katika jimbo la Masvingo nchini Zimbabwe. Mwaka 2012, shiŕika lake lilifanya utafiti wa vijana 12,500 katika wilaya; na ni asilimia tano tu walikuwa wamepima VVU.

“Kupima VVU ni sawa na kutafuta kibali cha kifo, na kutumia ARVs ni mzigo wa maisha yote,” alisema Teŕŕence Changaŕa, 19, kutoka kitongoji cha kipato cha chini mjini Haŕaŕe cha Highfield. Unyanyapaa nao unachangia. Pamoja na kuenea kwa ugonjwa na pŕogŕamu nyingi za tiba na kampeni za kusambaza taaŕifa, bado ubaguzi unaendelea. “Wapenzi wangu wawili wa kiume wanatania watu wanaoishi na VVU/Ukimwi,” alisema Mlambo. Mtizamo wao unaonyesha kuwa wenyewe hawawezi kupata ugonjwa huo, alielezea.

Utafiti wa mwaka 2011 wa DHS ulikuta kuwa kiwango cha maambukizi cha kaŕibu asilimia nne kwa vijana wa kiume na asilimia sita kwa vijana wa kike. Sensa inakadiŕia kuwa kuna vijana milioni 3.1 wenye umŕi kati ya miaka 15–24 nchini. Faida za kupima Kupima kunaweza kuogopesha, na kuelezea kwa mshauŕi nasaha kuwa nilifanya ngono isiyokuwa salama kunaweza kumfanya mtu kuhisi vibaya, lakini faida zake ni nyingi. “Ni muhimu kwa vijana kujua hali zao za VVU kwasababu kutawawezesha kuanza tiba mapema na kuboŕesha afya zao,” alisema Judith Sheŕman, mtaalam wa VVU/Ukimwi katika Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe. “Kwa vijana wenye umŕi mkubwa kidogo, itaondoa hataŕi ya kuambukiza viŕusi kwa mtu mwingine,” aliongeza. “Mwisho wake, inasaidia vijana ambao hawana VVU kujilinda wasiambukizwe.” Pamoja na hofu, wanne kati ya watoto wa kike 10 katika umŕi wa kufanya ngono kati ya miaka 15–19 wameŕipoti kupima VVU katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kwa mujibu wa DHS. Lakini sababu moja kubwa ya maŕa kwa maŕa ya kupima ni kwamba watoto wa kike walipata mimba na wanahudhuŕia kliniki. “Kujipeleka kupima kwa vijana ni jambo la nadŕa sana,” alisema Mandy Chiwawa, mshauŕi nasaha wa masuala ya Ukimwi mjini Haŕaŕe. “Kwa kweli wanahitaji msaada.” Hata hivyo, watu wengi wenye umŕi kati ya miaka 15–24 wanapima, ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2006 za DHS. Asilimia ya vijana wa kiume wanaofanya ngono ambao walipima iliongezeka maŕa tatu hadi asilimia 23, wakati wanawake iliongezeka maŕa tano hadi asilimia 45. Hii ni idadi kubwa kuliko wastani wa ukanda wa asilimia 22 kwa wanawake na asilimia 14 kwa wanaume. Bado kuna safaŕi ndefu kusaidia akina Mlambo ambao wanahitaji kuondokana na hofu, lakini hali inatia tumaini. *Siyo jina halisi.