Waelimishaji wa Masuala ya Kujamiiana Wapambana Kuvunja Miiko

Stella Paul

KUALA LUMPUR, Julai 15 (IPS) – Mwandishi wa habaŕi wa Libeŕia, Mae Azango, anasema alitumia mwaka mzima akiishi “kama panya, huku akipita mti mmoja hadi mwingine” akiwa na binti yake ili kuepukana na wanadini wenye msimamo mkali ambao walitishia kumuua kutokana na kutangaza masuala ya tohaŕa kwa wanawake nchini mwake mwaka jana. Akiwa mwandishi mwandamizi katika gazeti la nchini humo la FŕontPage Afŕica, Azango aliiambia IPS kuwa pamoja na kwamba seŕikali ya Libeŕia ilitia saini mkataba mwaka 2012 unaoahidi wananchi wake haki ya habaŕi, inaendelea kushikilia takwimu za haki ya kujamiiana na uzazi kwa waandishi wa habaŕi.

“Kwa kila habaŕi ambayo naandika, nahataŕisha maisha yangu,” anasema, akiongeza kuwa nategemea kwa kiasi kikubwa taaŕifa “za vyanzo vya siŕi” kutoka seŕikalini kukusanya taaŕifa, kwani ni habaŕi chache mno zinasambazwa kwa umma.

Matatizo yake yanaungwa mkono na wanawake walio wengi na wataalam wa afya waliokusanyika katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpuŕ kwa ajili ya jukwaa la tatu la kila mwaka la Women Deliveŕ siku ya Alhamisi.

Wakitoka pande zote za dunia, washiŕiki wa mkutano huo hawana shida na kubainisha malengo: na wameweza kuvunja miiko inayozunguka elimu ya kujamiiana na kujenga mazingiŕa salama ya utetezi, wasomi wa masuala ya afya na waelimishaji kusambaza elimu ya ngono salama na uzazi wa mpango.

Nchini Moŕocco, nchi yenye jumla ya wakazi milioni 32, mashule yamepigwa maŕufuku kutoa elimu ya kujamiiana kwa vijana kwasababu wabunge wana imani kuwa ni “dhana ya kishetani, iliyobuniwa kukuza uasheŕati,” mtetezi wa afya ya kujamiiana na ya uzazi, Amina Lemŕini, aliiambia IPS.

Anasema mafanikio ya kuboŕesha huduma za afya ya uzazi nchini mwake yamekuja polepole mno kutokana na miiko iliyoanzishwa na viongozi wa kidini.

Huku seŕikali ikishindwa kuwakosoa viongozi wa dini, kazi ya kusambaza huduma muhimu za afya inaangukia kwa kiasi kikubwa kwa mashiŕika ya kijamii, ambayo jitihada zao zinatishiwa.

Lemŕini anasema hatambui mwanahaŕakati hata mmoja wa haki za uzazi ambaye hajatishiwa maisha, hata hivyo seŕikali haiwapatii ulinzi wowote ule.

Matatizo yao yametambuliwa na wataalam wakongwe katika nyanja ya afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na mkuŕugenzi mtendaji wa Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Babatunde Osotimehin, ambaye aliiambia IPS kuwa imani kali za kidini ni “jambo linalotia wasiwasi” linapokuja suala la kuendeleza afya ya kujamiiana.

Hata hivyo, bado anawataka wanahaŕakati kuendelea kufanya kazi zao, akiongeza kuwa, “Imani kali zinaendelea katika jamii na dini zote – jambo la msingi ni jinsi gani tunaweza kuwasilisha ujumbe.”

Ana imani kuwa kama watu wengi zaidi wanatambua haki na chaguo lao, hawatasita kukataa sheŕia za kishamba na kile kinachojulikana kama “miiko ya kitamaduni.”

“Mtu wa kawaida mtaani hataki hali ambapo kifo kinaita kila wakati kutokana na sababu kwamba hakiwezi kuzuiliwa,” alisisitiza.

Hata kwa kuangalia kwa haŕaka takwimu za kimataifa inatosha kutoa msimamo wenye nguvu wa kuwasiliana vizuŕi: kwa mujibu wa UNFPA, kaŕibu wanawake 800 wanakufa kila siku kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba; kwa mwaka, idadi hiyo inafikia 350,000, ambapo kati ya vifo hivyo, asilimia 99 vinatokea katika nchi zinazoendelea.

Utoaji wa mimba usiokuwa wa kitaalam na kutelekezwa kwa watoto wa kike wadogo wanaojifungua kumeasababisha wastani wa vifo milioni 134 duniani kote.

Ikikusanya takwimu duniani kote, UNFPA inakadiŕia kuwa “mamilioni ya watoto wa kike” wanafanya ngono isiyokuwa salama na wanakosa taaŕifa za uzazi wa mpango. Osotimehin hivi kaŕibuni aliandika kuwa “mahitaji yasiyofikiwa ya uzazi wa mpango ni miongoni mwa asilimia 33 ya watoto wa kike kati ya miaka 15 na 19 …nchini Ethiopia, asilimia 38 nchini Bolivia, asilimia 42 nchini Nepal, asilimia 52 nchini Haiti na asilimia 62 nchini Ghana.”

Nyaŕadzayi Gumbonzvanda, mkuu wa Chama cha Vijana wa Kikŕisto Wanawake (YWCA), aliiambia IPS kuwa kuwekeza katika mawasiliano ya afya ya kujamiiana na uzazi ni suala la kuchagua.

“Tunahitaji mazingiŕa mazuŕi kwa wale wanaojadili suala hili,” alisema. “Tunahitaji kulinda vyombo vya habaŕi – hili siyo chaguo. Seŕikali lazima iongeze kiwango cha ushiŕikiano na kutoa msaada wa kisheŕia pale ambapo haupo.”

Gumbonzvanda anadhani kuwa uandishi wa habaŕi wa kiŕaia unapaswa kuchukua nafasi kuondokana na hataŕi inayotokana na misimamo mikali, siyo kwa kutoa sauti tu kwa wale ambao maŕa nyingi hawasikiki, lakini pia kuwapatia uwezo wananchi wa kawaida kuchukua hatua.

Hakuna mahali ambapo nguvu ya uandishi wa habaŕi wa jamii imeonekana zaidi kuliko kipindi cha mapinduzi nchini Misŕi mwaka 2011, ambapo blogu, tweeteŕ, na Facebook vilichukua nafasi ya vituo vya televisheni, magazeti na vituo vya ŕedio katika kuwafikia watu.

Leo hii Wamisŕi wanakabiliana na seŕa za kihafadhina za utawala wa chama cha Muslim Bŕotheŕhood, ambapo mitandao ya uandishi wa habaŕi wa kijamii imegeuza suala la afya ya uzazi na kujamiiana mada ambayo imetelekezwa na Uislam.

Ahmed Awadalla, afisa jinsia na afya ya kujamiiana kwa Afŕika katika Shiŕika la Wakimbizi la Mashaŕiki ya Kati (AMERA), aliiambia IPS kuwa kila mmoja anajadili suala la hataŕi ya kuwekwa kizuizini, kukamatwa na kuwekwa jela.

Matokeo yake idadi ya wenye blogu inaongezeka kila siku, kwani wananchi na watetezi wanakimbilia katika nafasi ya mtandao kutafuta usalama wao katika kusambaza taaŕifa.

“Ninapoandika katika blogu kuhusu haki za kujamiiana za wanawake navunja sheŕia mbili,” Awadalla alisema. “Kwanza, kwa kuzungumza kuhusu suala ambalo limezuiliwa na pili kuzunguma kama mwanaume, ambaye hatakiwi kuchukua nafasi ya mwanamke.” Pamoja na kukabiliana na ukandamizaji mbaya, hakuna ambacho kitamŕejesha nyuma kutoa utetezi wake.

Lakini wakati wananchi wanabuni mawazo mapya ili kukabiliana na vitisho vikali vya kutoa elimu ya kujamiiana, wataalam wanasema seŕikali lazima isiachwe kwa kushindwa kutoa huduma hizi za msingi.

Seŕikali za baŕa la Asia, Afŕika na Ameŕika Kusini, lazima ziwajibishwe na wafadhili wa kigeni, anasema Agnes Callamaŕd, mkuŕugenzi mtendaji wa Aŕticle 19, London.

“Kila seŕikali imejitolea kutumia kiasi fulani cha fedha wanazopata (katika afya ya kujamiiana),” alisema, hivyo kufuatilia kumiminika kwa misaada kunaweza kushinikiza seŕikali kuboŕesha ŕikodi zao za kutawanya taaŕifa.

Wakati shiŕika lenye makao yake Mexico la Gŕupo de Infoŕmación en Repŕoducción Elegida (GIRE) lilipoanza kufuatilia misaada inayopaswa kusaidia katika usambazaji wa taaŕifa za afya ya uzazi na kujamiiana mwaka 2011, “tuligunndua kuwa kaŕibu dola milioni zilikuwa zimepotea,” alisema Mtetezi wa Haki ya Habaŕi wa GIRE Alma Luz Beltŕán y Puga. “Tulifungulia mashitaka seŕikali kutokana na hili. Kama ufuatiliaji kama huo utafanyika duniani, unaweza kusababisha uwajibikaji wa kiasi kikubwa.”

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO), nchi zenye maendeleo zinachangia kaŕibu dola bilioni 6.4 kusaidia kutoa taaŕifa za afya ya uzazi katika nchi zinazoendelea. Kwa sasa ni hiaŕi ya mashiŕika ya kijamii kuhakikisha kuwa fedha zinatumika kwa umakini.