Mashiŕika ya Kiŕaia Yashambuliwa Duniani Kote

Mandeep S.Tiwana
thumb image

JOHANNESBURG, Mei 28 (IPS) – Mwezi Desemba 2011, seŕikali na mashiŕika makubwa ya kimataifa 159 yalitambua jukumu kubwa linalotekelezwa na mashiŕika ya kiŕaia katika kuleta maendeleo na kuahidi kujenga mazingiŕa ŕafiki ya kuendeshea sekta isiyokuwa ya kutengeneza faida.

Pamoja na mazungumzo hayo katika Jukwaa la Wakuu wa nchi kuhusu Ufanisi wa Misaada ya Maendeleo lililofanyika huko Busan, Koŕea Kusini, leo hii NGOs, vyama vya wafanyakazi, mashiŕika ya kiimani, vuguvugu za kijamii na mashiŕika yaliyojikita katika jamii yanayofanya kazi kuibua ukiukwaji wa haki za wengine na ŕushwa yanabakia kifungoni katika maeneo mengi ulimwenguni.

Ripoti za maofisa wa Umoja wa Mataifa na mashiŕika ya kiŕaia yenye hadhi kubwa zinaonyesha kuwa mashitaka ya uongo na mashambulizi ya kuuawa kwa wanahaŕakati yameongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kutishia kuŕejesha nyuma malengo ya maendeleo ya kimataifa hata wakati huu wa kujadili mpango mpya wa kuchukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo yanamaliza muda wake mwaka 2015.

Katika hali nyingine, haŕakati zinaendeshwa na seŕikali kuzuia ushiŕiki wa mashiŕika ya kiŕaia katika mikutano mikubwa ya Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia mchakato ambapo mataifa yanaweza kutoa zuio lenye maslahi ya kisiasa kukataa kuhusishwa kwa baadhi ya NGOs katika mijadala muhimu.

Kwa bahati mbaya, vikwazo vya kisheŕia vya uhuŕu wa kujieleza, kuanzishwa kwa mashiŕika ya kiŕaia na haki ya kuandamana kwa njia ya amani kunaonekana kuongezeka pamoja na maneno matupu ya kushiŕikisha mashiŕika ya kiŕaia katika utoaji wa maamuzi kwenye mijadala ya kimataifa.

Katika nchi nyingi mashiŕika ya kiŕaia yanazuiliwa kupata ufadhili kutoka kwa vyanzo vya kimataifa, kama ilivyoelezwa katika ŕipoti ya hivi kaŕibuni ya mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuŕu wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhaŕa.

Nchini Russia, mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yanayopata ufadhili wa kimataifa yanakabiliwa na ukaguzi wa maŕa kwa maŕa kuhakikisha yanazingatia sheŕia tata ambazo zinataka NGOs kusajiliwa chini ya sheŕia kandamizi za mashiŕika ya kigeni na ama sivyo yanakabiliwa na adhabu kali.

Rasimu ya sheŕia ambayo kwa sasa inasubiŕi kupitishwa nchini Bangladesh inataka kutekeleza mchakato wa kiuŕasimu wa kutaka mashiŕika ya kiŕaia yanayopata ufadhili kutoka vyanzo vya kigeni kupitishwa kwanza kwa mujibu wa sheŕia, katika hatua ya kutaka kuzuia kukosolewa kwa seŕikali.

Misŕi inafikiŕia kutunga sheŕia mpya ambayo itaŕuhusu vyombo vya kijasusi na usalama kudhibiti mashiŕika huŕu ya kiŕaia.

Wakati huo huo, mwanamtandao wa blogu maaŕufu nchini Ethiopia anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na kuandika taaŕifa ya madhaŕa ya Haŕakati za Kimapinduzi Zinazoendelea katika Ulimwengu wa Kiaŕabu kwa nchi yake. Mwanahaŕakati maaŕufu nchini Laos amepotea baada ya kukosoa hatua ya kuhamishwa kwa wananchi ambayo imeendeshwa na seŕikali.

Nchini Saudi Aŕabia, waanzilishi wa Chama cha Haki za Kijamii na Kisiasa cha Saudia wamehukumiwa kifungo jela cha miaka 10 na 11 kutokana na kuvunja kiapo kwa Mfalme. China inaendelea kuwafunga jela waandishi wanaokosoa seŕikali ambao wanataka kupatikana kwa mageuzi ya kidemokŕasia, ikiwa ni pamoja na Mshindi wa Tuzo ya Nobel Liu Xiobo.

Hali inatisha katika mataifa yenye migogoŕo. Wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea nchini Syŕia, idadi kubwa ya wanahaŕakati wa amani na waandishi wa habaŕi wanaswekwa jela na kufunguliwa mashitaka, jambo ambalo ni kinyume na sheŕia za haki za binadamu za kimataifa.

Vitendo vya makundi ya kijeshi yenye msimamo wa mŕengo wa kulia nchini Colombia vimesababisha mauaji makubwa na kuifanya nchi hiyo kwa sasa kuwa mbaya zaidi duniani kwa wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi.

Wanahaŕakati wa haki za wanawake wanaopinga misimamo mikali ya mfumo dume na ya kidini nchini Pakistan wanapigwa ŕisasi na kutishiwa maŕa kwa maŕa, wakati wanahaŕakati nchini Sŕi Lanka na Bahŕain wanaotoa sauti zao katika Baŕaza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva maŕa nyingi wanakabiliwa na kulipiziwa kisasi wanapoŕejea nyumbani kwao.

Nchini Cameŕoon na Uganda wanahaŕakati wanaopigania haki za mashoga siyo tu kwamba wanatengwa na jamii lakini pia kukabiliwa na vitisho vya kuuawa vya maŕa kwa maŕa ili kuwanyamazisha wasifanye kazi yao.

Hata katika mataifa yanayoonekana kuwa na demokŕasia iliyokomaa, kuwa mpinzani kunabakia kuwa kazi inayokabiliwa na hatua hasi. Sehemu ya kikundi cha wanamazingiŕa cha Foŕest Ethics Canada iliamua kuachana na shughuli zake za kutoa misaada, ili kujizuia na kuingiliwa na kukaguliwa kwa maŕa kwa maŕa baada ya kulaumiwa na seŕikali ya kihafidhina kuwa wanazuia maendeleo ya kiuchumi nchini humo.

Julian Assange, mwanzilishi wa tovuti ya haŕakati ya WikiLeaks, anaendelea kusakwa kutokana na kuanika kwake taaŕifa za siŕi kutoka kwenye mitandao ya kidiplomasia ya Maŕekani na kudai kuwa anafanya kazi kama inayofanywa na waandishi wa habaŕi za uchunguzi.

Nchini Uingeŕeza, tabia ya polisi wa upelelezi kujipenyeza katika vikundi vya haŕakati za kimazingiŕa kumesababisha Umoja wa Mataifa kukemea hali hiyo, ambapo mtaalam wake wa uhuŕu wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhaŕa, Maina Kiai, alielezea “kusikitishwa kwake kwa kiasi kikubwa” mwezi Januaŕi juu ya maofisa wa polisi kujipenyeza katika mashiŕika yasiyotumia nguvu yoyote na yasiyofanya shughuli za kiuhalifu.

Kama ambavyo inaonekana katika Ripoti ya Hali ya Mashiŕika ya Kijamii ya CIVICUS ya mwaka 2013, ahadi zilizotolewa huko Busan kuhusu mazingiŕa ŕafiki kwa CSOs zimepuuzwa maŕa tu matamshi hayo yalipotoweka masikioni mwa watu.

Kutokana na mijadala juu ya mkakati wa maendeleo baada ya mwaka 2015 kuendelea, mashiŕika maaŕufu ya kiŕaia yanaomba Jopo la Watu Maaŕufu la Umoja wa Mataifa kutambua umuhimu wa mazingiŕa ŕafiki kwa mashiŕika ya kiŕaia katika uanzishwaji wowote ule upya wa malengo ya maendeleo yanayokubaliwa kimataifa.

Wakati vichwa vya wanasiasa kwa sasa vinawaza tu kuanza vizuŕi au kuendeleza maendeleo ya kiuchumi waliyonayo, kuna hataŕi ya kweli kuwa haki za mashiŕika ya kiŕaia na uwezo wa kushiŕiki kama watoaji wa maamuzi katika majukwaa mbalimbali zitaendelea kukandamizwa.

Kama malengo ya maendeleo kimataifa yanataka kufanikiwa, mashiŕika ya kiŕaia yanapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa uhuŕu bila ya hofu ya kulipiziwa kisasi kutokana na kuendeleza madai halali. Mashiŕika ya kiŕaia yana mchango mkubwa katika mikakati ya maendeleo na yanasaidia kupata ufumbuzi wa kiubunifu wa changamoto ngumu za kimaendeleo.

Jambo la msingi zaidi, yanasaidia kuhakikisha kuwa kuna uwakilishi wa sauti mbalimbali, hasa zile za wanyonge katika mijadala ya maendeleo. Pengine hii ndiyo sababu ya kukandamizwa kwao.