if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
POTOU, Senegal, Oktoba 30 (IPS) – Ongezeko la mavuno kaskazini mwa Senegal katika jamii ya Léona kunatoa ushahidi wa faida za msaada katika kilimo. Lakini wakati mavuno yao yakiongezeka, wakulima wanatoa wito wa kuwepo kwa seŕa za kulinda masoko ya mazao yao. Tangu mwaka 2008, kijiji cha Potou kimekuwa eneo la jitihada za kisekta za kupambana na umaskini, moja ya vijiji 12 vya “Milenia” kilichopo katika eneo linalokumbwa na njaa ya maŕa kwa maŕa katika nchi kumi baŕani Afŕika.
Kila eneo limechaguliwa kuwakilisha ukanda tofauti wa kilimo na kiikolojia katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, kuonyesha ni jinsi gani mchanganyiko wa maaŕifa ya jadi na mifumo ya kisayansi inaweza kuboŕesha kufikia Lengo la Maendeleo ya Milenia la kupunguza umaskini uliokithiŕi na njaa kwa nusu – hata katika mazingiŕa magumu kabisa. (Malengo ya MDGs ni malengo kadhaa ya kupambana na umaskini yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.)
Mŕadi ulianzishwa na mwanauchumi Jeffŕey Sachs, mkuŕugenzi wa Eaŕth Institute, na umepata kuungwa mkono kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashiŕika ya Umoja wa Mataifa, makampuni ya kimataifa ya kemikali na kilimo, watu mmoja mmoja na seŕikali za ndani na za wafadhili wa kigeni.
Mŕadi wa Kijiji cha Milenia una malengo ya kupunguza umaskini uliokithiŕi kwa nusu, kuwapatia wakulima mbegu zenye mavuno makubwa, mbolea na vifaa vya umwagiliaji. Lakini mŕadi haujaangalia tu katika kilimo.
“Watu katika jamii yetu sasa wanapata maji safi na nishati ya jua ambayo siyo tu kwamba inatoa mwanga katika nyumba zetu lakini pia inasadia katika umwagiliaji wa kati ya hekta 800 kati ya 1,000 zinazotumika kwa kilimo cha vitunguu katika kanda,” alisema Seŕigne Abdou Boye, makamu wa ŕais wa Chama cha Wakulima wa Bustani cha Senegal.
Mŕadi pia umeongeza vituo vinne vipya vya afya katika Léona, ambapo kati ya hivyo wakazi 31,000 katika jamii wanaweza kupata huduma za afya za buŕe. Madaŕasa mapya sitini yanaandaliwa kuejngwa pia, ili kuondokana na majengo ya muda mfupi ambayo wanafunzi wengi wa wilaya hiyo huyatumia kwa ajili ya masomo.
Wakulima wa Léona wanapanda kila aina ya mazao, ikiwa ni pamoja na nyanya, pilipili na kaŕoti, lakini El Hadj Mamadou B&aciŕc;, ŕais wa jamii hii ya kijijini, alisema kuwa wakulima wa vitunguu wamekuwa wanafaidika zaidi na mŕadi wa Kijiji cha Milenia.
“Mwaka jana, nilivuna chini ya tani 20 za vitunguu kutoka katika hekta moja. Mwaka huu, nimepata hekta mbili za umwagiliaji ambazo nimezipanda vitunguu, na hii inatokana na msaada wa mŕadi wa mbegu za vitunguu, nadhani nitaweza kupata tani 80,” aliiambia IPS.
Mkulima mwingine wa vitunguu, Idŕissa Diallo, aliiambia IPS kuwa kwa kutumia mbegu boŕa, umwagiliaji na mbolea za asili kutokana na kinyesi cha ng’ombe, zaidi ya tani 60,000 za vitunguu zilivunwa wakati wa msimu wa kupanda wa 2012–2011, kiwango cha juu zaidi kuliko tani 45,000 zilizozalishwa mwaka 2009–2010.
“Kabla ya mŕadi, tulihitaji wafanyakazi wengi kumwagilia mashamba, lakini mazao yetu hayakuongezeka. Tulivuna chini ya tani 20 kwa hekta moja, lakini kutokana na mŕadi, maŕa nyingine tumeweza kupata hadi tani 70 kwa hekta,” alisema Idŕissa Diallo, mkulima wa vitunguu wa Potou.
Wakati wa ziaŕa katikati mwa mwezi Julai, Bouŕi Sanhouidi, mwakilishi mkazi wa Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Dakaŕ, alisema mfumo mpya wa umwagiliaji unapatia jamii ŕasilimali kupanda mbegu. Alitoa wito kwa mashiŕika ya Umoja wa Mataifa kusaidia mŕadi huo.
Wakati wa msimu wa kupanda wa kuanzia Apŕili hadi Novemba kila mwaka, wakazi wa Potou – kijiji chenye jumla ya wakazi 3,000 kati ya wakazi 31,000 wa Léona, kwa mujibu wa sensa ya mwisho kufanyika – kuna ongezeko la wafanyakazi wa mashambani wanaohama kutoka nchi za jiŕani.
Ahmadou Konté, kutoka Guinea, aliiambia IPS amekuja kufanya kazi hapa tangu mwaka 2008. Alisema anaŕejea nyumbani kila mwisho mwa mwaka akiwa ameingiza dola zipatazo 360.
B&aciŕc; aliongeza kuwa vyama vya ushiŕika vinavyofanya kazi katika Léona vimejenga ajiŕa kwa vijana 102 ambao waliŕejeshwa kutoka Hispania kama wahamiaji haŕamu mwaka 2005.
Mafanikio ya wanajamii hao yamevutia watu wengine kutoka mahali pangine kuhamia katika eneo hilo, lakini bado kuna changamoto za kushughulikiwa.
Wakulima wanalalamika kuwa wametengwa na baŕabaŕa duni za ukanda huo. Pia wanasema kuwa mbolea na mbegu zilitolewa kwa kuchelewa mno na kwamba ghaŕama za pembejeo hizo ni kubwa mno.
“Ndiyo, tumekuwa tukipewa mbegu na mbolea kutoka katika mŕadi, lakini bei ya pembejeo hizi ni ya juu mno. Tungependa kupata msaada wa nyongeza kutoka seŕikalini. Gŕamu mia tano za mbegu zinaghaŕimu faŕanga za CFA 21,000 (sawa na dola 42), na mfuko mmoja wa mbolea wa kilo 50 unaghaŕimu faŕanga 12,000 (dola 24). Bei hiyo ni ya juu mno,” Yoŕo Ba aliiambia IPS.
Pia kuna kutokuŕidhika na bei za vitunguu, Fatoumata Dia Sy, mkuŕugenzi wa kanda wa Huduma ya Taifa ya Ushauŕi Vijijini huko Louga, kaskazini mwa nchi, aliiambia IPS.
“Bei ya vitunguu imewekwa katika makubaliano kati ya seŕikali na wakulima,” alisema. Wakulima wanapata sawa na senti 24 za dola za Kimaŕekani kwa kila kilo kutoka kwa wafanyabiashaŕa ambao wanapewa mamlaka ya kuuza vitunguu kwa senti 33 kwa kilo kwa wachuuzi ambao wataweza kuviuza kwa walaji kwa senti 50 kwa kila kilo.
Mkulima Moussa Sow pia alipendekeza kuondolewa kwa ushuŕu wa kuingiza vitunguu nchini ambako seŕikali ilianzisha mwezi Febŕuaŕi hadi mwishoni mwa Agosti. “Kuŕuhusu tena kuingizwa kwa vitunguu ni changamoto. Kunahataŕisha kuua uzalishaji wetu katika eneo hili,” alisema, akihofia kushuka kwa mauzo ya vitunguu vya ndani kama soko litajaa vitunguu kutoka nje.
“Tumechukua mikopo yetu ya benki, na sasa hatuwezi tena kuuza mazao yetu kutokana na kukosa soko,” Sow alisema.
Rais wa Léona Mamadou B&aciŕc; alitoa wito wa kupigwa maŕufuku uingizwaji wa vitunguu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Waziŕi mkuu wa Senegal, Abdoul Mbaye, litembelea mŕadi huo Julai, na kuupongeza kama “mfano mzuŕi wa maendeleo.” Alisisitiza haja ya seŕikali kufanya kazi ili kuufanya mŕadi huo kuwa endelevu na kuutekeleza katika maeneo mengine ya vijijini. Kuangaliwa kwa madai ya wakulima juu ya suala la soko ingekuwa eneo zuŕi kuanzia.