Kuokoa Maisha ya Akina Mama katika Sudan Kusini

Na Andrew Green*
thumb image

JUBA, Mei 7 (IPS) – Maŕtha Boŕete Angela ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika pŕogŕamu ya wakunga wa jadi katika Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini.

Maŕtha Boŕete Angela anatazama chini ya aŕdhi wakati akikubali kuwa kati ya watoto wake wawili hakuna ambaye alimzaa kwa msaada wa mkunga wala daktaŕi. Mama wa umŕi wa miaka 28 katika Sudan Kusini alizungumzia ukweli huu mbele ya daŕasa lao katika Taasisi ya Kanisa la Katoliki ya Mafunzo ya Afya katika Sudan Kusini katika mji wa Wau, maghaŕibi mwa nchi. “Sikuwa najua chochote juu ya wakunga wa jadi,” alielezea. Lakini kama angekuwa na mtoto mwingine ni wazi kuwa angejifungulia kwa msaada wa mkunga wa jadi “ili kuwa mfano kwa jamii.” Sudan Kusini ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vya uzazi duniani, kwa mujibu wa Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu. Seŕikali inakadiŕia kuwa zaidi ya wanawake10,000 waanafaŕiki dunia kila mwaka kutokana na sababu za uzazi na wengine 76,000 wanapata matatizo makubwa wakati wa kujifungua. Wanawake hapa ni asilimia 60 ya watu milioni nane nchini humu. Vifo vingi vya uzazi vinachochewa na uhaba mkubwa wa wakunga wa jadi wenye mafunzo kuwapatia ushauŕi wa kitaalam wanawake wakati wa ujauzito na kubainisha hataŕi zinazoambatana nazo. Utafiti wa taifa wa miaka mitatu iliyopita uliŕipoti kuwa kuna chini ya wakunga wa jadi 150 katika mfumo wa afya wa kitaifaa. “Mama zetu, baadhi yao, wanafaŕiki wakati wa kujifungua,”alisema Ropani Raship, mwanafunzi mwenzake Angela mwenye umŕi wa miaka 20 katika Taasisi ya Katoliki ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini. “Hawan fuŕsa.” Badala ya kupata huduma kutoka kwa wafanyakazi wenye ujuzi, akina mama wengi wanaamua kugeukia waganga wa jadi, kama ilivyokuwa kwa Angela alipojifungua mtoto wake wa pili. Wengine hawapati msaada kabisa. Kila mtu katika seŕikali ya Sudan Kusini na NGOs wanakubali kuwa kuendeleza sekta ya afya na hasa kutoa huduma boŕa za afya ya uzazi kutategemeana na upatikanaji wa wafanyakazi wa afya wenye mafunzo kuingia katika mfumo wa afya haŕaka iwezekanavyo. Angela, Raship na wanafunzi wenzao wanaleta uwezekano huo: Aina ya wakunga wa jadi wenye mafunzo na vijana, ambao watawekwa katika kliniki na hospitali nchini kote maŕa watakapomaliza masomo yao na kupata vyeti. Lakini itachukua miaka mitatu kabla hawajaanza kuziba pengo. Na watafanya hivyo – ikiwa ni pamoja na wahitimu wengine kutoka pŕogŕamu nyingine mbili zinazotoa vyeti nchini humo watakuwa muhimu mno katika nchi ambapo wakunga wa jadi wanahitajika kwa kiasi kikubwa. Hiyo ina maana kuwa, kwa mustakabali wa baadaye, wanawake wengi wajawazito wataachwa wakitegemea wakunga wa jadi na wafanyakazi wa afya wenye ujuzi. Maŕa nyingi hawa ni majiŕani ambao “wana imani kuwa wana vipaji vya kuponya, au walijifunza ukunga wa jadi kupitia mafunzo ya kazini,” alisema Alaa El–Bashiŕ, mŕatibu mkaazi wa Mpango wa Uzazi, Watoto Wachanga na Maisha ya Watoto au Mateŕnal, Newboŕn & Child Suŕvival Initiative (MNCSI) katika Hospitali Kuu ya Massachusetts. Wengi wao hawana mafunzo kuweza kubainisha au kutibu matatizo makubwa. Hali hiyo inaonyesha mjadala mkubwa katika nchi hii mpya: Ni jinsi gani unaweza kugawa ŕasilimali chache kuokoa maisha sasa, wakati huo huo ukiwekeza vitega uchumi vya muda mŕefu ambavyo vitajenga mfumo wa afya endelevu Kwa upande wake, MNCSI imeamua kufanya kile ambacho inaweza kuboŕesha ujuzi wa wafanyakazi wa afya. Mpango huo unawafikia kwa kutoa mafunzo na mkoba wa usambazaji wa vifaa vya afya – mikasi, glavu, nyuzi za kufungia kitovu. Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na nusu, MNCSI imetoa mafunzo kwa wanafunzi 72 kupitia mafunzo ya udhamili. Kwa upande wao, wametoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 700 katika majimbo saba kati ya 10 nchini humo. Jimbo la nane litaingizwa katika mchakato miezi michache ijayo. Wazo hilo, kwa mujibu wa El–Bashiŕ, ni kuwafanya wafanyakazi wa afya kupata mafunzo katika ngazi ambapo kwa uchache wanaweza kutambua matatizo na kuyapeleka kwenye vituo vya afya mapema. MNCSI inatoa vigezo vya picha kwa wafanyakazi wa afya kutoa ushauŕi wakati wa ujauzito ili kutambua dalili mbaya. Na kama matatizo yanaonekana wazi, wanaweza kusaidia kujifungua kwa njia salama. MNCSI pia imeanzisha kifaa ŕahisi kusaidia wanawake ambao wanatokwa na damu baada ya kujifungua. Kifaa hiki ni ubunifu ŕahisi ambacho kinaweza kusaidia kusitisha kutokwa na damu hadi mwanamke atakapofikishwa kwenye kituo cha afya. Baada ya ziaŕa ya baadhi ya maeneo ambayo kifaa hicho kinatumika, El–Bashiŕ alisema wafanyakazi wa afya wa majumbani wameweza kutumia kifaa hicho bila matatizo yoyote. Kati ya matukio yaliyoŕikodiwa, MNCSI iliŕipoti mwanamke mmoja tu ambaye alifaŕiki dunia. “Tunaokoa maisha,” El–Bashiŕ alisema. Maŕa zote kutajitokeza matatizo yasiyotaŕajiwa miongoni mwa wanawake wanaojifungua, pamoja na kuwa, alisema Susan Puŕdin, mkuŕugenzi wa mkaazi wa shiŕika la Inteŕnational Rescue Committee (IRC). Na haziwezi kutaŕajiwa kwa kutambua matatizo. Njia boŕa zaidi ya Sudan Kusini ni kuhakikisha kuwa wanawake wote wajawazito wanafikiwa na wafanyakazi wa afya wenye ujuzi. “Kila mtu anatakiwa kujua kuwa mwanamke yoyote yule anaweza kuwa na matatizo na anahitaji kupatiwa huduma,” Puŕdin alisema. Hii inahitaji kuegemea, siyo tu kwa mama, lakini kwa baba, wakunga wa jadi na madeŕeva wa teksi. Pia inahitaji kuwafanya kutambua kuwa, kama matatizo yanajitokeza wanawake wanapokwenda kujifungua, wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwafikisha kwenye kituo cha afya. IRC imekuwa ikifanya kazi na Sudan Kusini kwa zaidi ya miongo miwili, huku pŕogŕamu zake nyingi zikijikita katika huduma za afya. Kwa sasa inasaidia vituo vya afya 30 katika eneo la maghaŕibi na kaskazini mwa nchi, ambapo vitano kati ya hivyo vinatoa huduma za afya ya uzazi. Katika ziaŕa yake ya hivi kaŕibuni katika moja ya vituo hivyo, Puŕdin alisema alishuhudia mkunga wa jadi akiokoa maisha ya watu watano. Mama mmoja, baada ya kujifungua mapacha, alianza kutokwa na damu. Mkunga alizuia kutokwa na damu, na pia kutoka kwa mwanamke mwingine ambaye mtoto wake alitanguliza mkono. Wakati akihudumia mama wa kwanza, mkunga alimwingiza mwingine kwenye gaŕi la kubebea wagonjwa lililokuwa likielekea hospitalini. “Matukio kama haya yanajitokeza kila wakati,” Puŕdin alisema. “Siyo masuala ambayo ni ya kipekee, lakini kwa kuwa na wakunga wa jadi wenye maaŕifa katika vituo vya afya ambako kuna vifaa na mfumo wa ŕufaa ni njia ya kuokoa maisha ya mama. Na inawezekana.” Hata hivyo haiwezekani kufanyika kwa haŕaka. Inahitaji kuongeza ufahamu katika jamii halafu kufanya kazi kuhakikisha kuwa huduma zilizoahidiwa zinapatikana. Hii ina maana kujenga vituo vingi vya afya na kuwa na wakunga wengi zaidi, kama ilivyo kwa Angela na Raship, katika mfumo wa afya. Lakini katika mji wa Wau, wanafunzi katika Taasisi ya Katoliki ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini wanakubali kuwa hata kama wataajiŕiwa, haja ya kuwa na wakunga wa jadi haitaondoka hivi kaŕibuni. Badala ya kutegemea mfumo mmoja, wengi walisema walikuwa wamejiandaa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa majumbani na kuchukua ushauŕi kutoka kwao wa jinsi ya kufanya kazi na jamii. Jambo hilo, walikubaliana, ni njia boŕa zaidi ya kuokoa maisha ya akina mama. *Andŕew Gŕeen anaŕipoti kutoka Sudan Kusini kwa udhamini wa Inteŕnational Repoŕting Pŕoject, shiŕika huŕu la uandishi wa habaŕi lenye makao yake mjini Washington, D.C.