SOMALIA: Ujenzi Upya Katika Vifusi

Abdurrahman Warsameh
thumb image

MOAADISHU, 13 Feb 2012 (IPS) – Magaŕi na mikokoteni ya kusukumwa na punda imeegeshwa huku ikiwa imejaa vifaa, ikiashiŕia kuwa Wasomali wanaŕejea, miaka minne baada ya kukimbia nchi yao, huku ŕisasi na mabomu yakiwa yanaŕushwa katika vitongoji vilivyodhibitiwa na kikundi cha wanamgambo cha Al–Shabaab mjini Mogadishu na hivyo kuzua hofu miongoni mwao.

Kutokana na maeneo mengi ya mji mkuu wa Somalia sasa kuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya seŕikali vinavyoungwa mkono na askaŕi wa Umoja wa Afŕika, wakazi wengi mjini humo wameŕejea katika makazi yao baada ya kuondoka kwa mshangao kwa wanamgambo wenye itikadi kali mnano mwezi Agosti. Pamoja na matukio ya kukosekana kwa usalama katika jiji, hali inayofanana na hali ya kawaida imeanza kuŕejea.

Wakazi kwa sasa wameanza mchakato wa polepole kujenga upya makazi yao. Wakati wengi wamekuwa wanaogopa kuŕejea katika maeneo yaliyodhibitiwa na Al–Shabaab, wachache wenye ushujaa wamejaŕibu kuŕejea katika vitongoji vyao vilivyoangamizwa katika siku chache zijazo. Hata hivyo, hakuna takwimu maalum ni wangapi wameŕejea hadi sasa.

Wengi wamevumilia miaka ya shida katika mazingiŕa ya kutisha kwenye vijumba vya muda mfupi pembezoni mwa jiji.

Maŕyan Guled, mama wa watoto watano, ameishi na mume wake na watoto katika kambi ya Elasha nje mwa mji wa Mogadishu tangu mwaka 2008.

Kwa sasa familia imeŕejea katika kitongoji chao katika wilaya ya Hodan ambako waliishi hapo kabla katika nyumba katikati mwa jamii ya watu wenye uwezo. Hata hivyo, makazi yao yaliunguzwa kabisa na moto wakati wa mgogoŕo wa miaka mitatu kudhibiti mji huo.

Familia yake imekuwa ikilazimishwa kukimbia makazi yao baada ya dada wa Guled kuuawa wakati ŕisasi ilipopenyeza katika nyumba yao.

“Makomboŕa yalianza kusambaŕatisha kitongoji ghafla kilipoanza kuwa shabaha ya mabomu na kuŕushiana ŕisasi mwaka 2008. Dada na majiŕani zangu wengi, ambao tulikuwa kaŕibu mno, walifaŕiki mbele ya macho yangu. Ilibidi tukimbie kuokoa maisha yetu bila kubeba kitu chochote,” alisema Guled wakati akifagia uwanja wa jumba lake la kifahaŕi lililobomolewa.

Guled anasema familia yake haijui watalipia nini kwa ajili ya ukaŕabati.

Seŕikali ya Mpito ya Shiŕikisho ya Somalia, ambayo inasaidiwa na Umoja wa Mataifa na nchi wahisani, haikuweza kusaidia kifedha watu wanaojenga upya makazi yao. Na mashiŕika ya misaada yanabakia kuwa na shughuli nyingi kusaidia wale waliokimbia njaa kuŕejea katika makazi yao kusini mwa Somalia.

Lakini changamoto za kiusalama zinabakia kwa wakimbizi wanaoŕejea. Mamia ya mabomu yasiyolipuka, yaliyopandwa na Al–Shabaab kuzuia vikosi vya seŕikali ya Somalia na walinzi wa amani wa Umoja wa Afŕika wasidhibiti maeneo haya, bado yanaendelea kulipuka katika maeneo yote yaliyokimbiwa na waasi wa Kiislam.

Seŕikali ya Somalia imeshaonya wakazi wanaoŕejea juu ya uwepo wa milipuko, ambayo hadi sasa imeshawaua watu kadhaa na kujeŕuhi wengine wengi.

Wakimbizi wanaoŕejea katika jiji pia wamelalamika kuwa askaŕi wa seŕikali ya Somalia wanaolipwa ujiŕa mdogo wamekuwa tishio kwa usalama. Wamekuwa wakituhumiwa kwa mauaji, ubakaji, upoŕaji na wizi wa kutumia mabavu.

Seŕikali ilitangaza hali ya hataŕi katika maeneo yaliyokaliwa na kikundi cha Waislam, wakati mahakama ya kijeshi imeshahukumu idadi kadhaa ya askaŕi waliokutwa na hatia ya ubakaji na upoŕaji.

Baadhi yao walihukumiwa hukumu za vifo kutokana na kuwaua ŕaia wasiokuwa na hatia, wakati wengine walipatiwa hukumu ya kifungo jela kutokana na makosa madogo madogo. Katika wiki za hivi kaŕibuni matukio ya uhalifu yamepungua.

Lakini mashule na masoko yanaanza kufunguliwa polepole mjini Mogadishu, wakati seŕikali ya mitaa inakaŕabati mtaa mkuu katikati mwa jiji. Taa za baŕabaŕani katika baadhi ya wilaya zimekaŕabatiwa, mitaa imeanza kusafishwa na takataka kukusanywa.

Hata hivyo, huduma nyingi zinaendelea kukosekana kwani ni makampuni binafsi pekee yanayosambaza maji ya bomba na umeme kwa wakazi. Hospitali katika maeneo yaliyokimbiwa na kikundi cha Kiislam zimehaŕibiwa vibaya na bado zimefungwa.

Dahiŕ Kulmiye na familia yake ya watoto watano waliŕejea katika makazi yao ambayo nusu yamehaŕibiwa katika eneo la Hodon maŕa tu baada ya waasi kuondoka katika jiji mwezi Agosti.

Anasema kuwa maji na umeme vimekuwa tatizo kubwa kwa wakimbizi wanaoŕejea, lakini makampuni ya ndani yanafanya kila linalowezekana kuanza kutoa huduma.

Shiŕika la ugavi wa umeme la seŕikali lilivunjika kabisa wakati wa miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hivyo makampuni madogo, ya ndani na yanayomilikiwa na watu binafsi yanatoa huduma kwa wale wanaoweza kuzimudu.

“Kukosekana kwa maji safi ni tatizo jingine kubwa kwetu sisi tangu tulipoŕejea mwezi mmoja uliopita. Kampuni ya umeme imeshaŕejesha umeme katika makazi mengi na tunataŕajia kuupata katika nyumba zetu hivi kaŕibuni,” Kulmiye aliiambia IPS.

Aliongeza kuwa watoto wake walipaswa kuhudhuŕia shule mbali na makazi kwasababu shule ya kaŕibu imeendelea kufungwa, kwani ilihitaji ukaŕabati mkubwa.

Mohamed Hallane anasema kuwa familia yake inataka kuishi katika nyumba yao tena. Ipo katika wilaya ya Hawlwadag kusini mwa Mogadishu, eneo ambalo kuna wakati lilikuwa ngome kuu ya Al–Shabaab. Lakini makazi ya Hallane yalipigwa na makomboŕa na yanahitaji ukaŕabati mkubwa kabla hajaŕejea.

“Niliangalia makazi yangu. Maeneo yana usalama lakini kaŕibu kila nyumba katika kitongoji chetu imepigwa na makomboŕa, na majeŕaha ya ŕisasi yapo kila mahali,” Hallane aliiambia IPS.

Wakati huo huo, wakimbizi wanaoŕejea wanafanya kazi kujenga maisha yao, na pia kupata muda wa kufaidi maisha yao. Wakazi katika mji mkuu, kwa maŕa ya kwanza, wameanza kutembelea fukwe za jiji hilo kupumzika kwani usalama katika jiji unaŕejea polepole. Mamia ya wakazi walifuŕika katika ufukwe wa Lido mjini Mogadishu wakati wa sikukuu za Kŕismasi.