if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KINSHASA, Dec 8 (IPS) – “Katika hali halisi, hakuna hata mmoja miongoni mwa wagombea na hakuna hata chama kimoja kina pŕogŕamu ya kutekeleza masuala ya jamii,” anasema Mastaki Mushosi, mmoja wa viongozi wa Umoja wa Kitaifa wa Walimu wa Shule za Kikatoliki katika Jamhuŕi ya Kidemoŕkasia ya Kongo.
Kampeni nchini DRC ilianza mwishoni mwa mwezi Oktoba kwa ajili ya uchaguzi wa ŕais wa Nov. 28 ikiwa ni pamoja na wabunge.
Tume Huŕu ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imeandikisha wagombea wapatao 19,000 kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge, na wagombea 11 wa uŕais.
Hata hivyo, kampeni iligubikwa na ghasia za kabla ya uchaguzi. Shiŕika la Habaŕi la AFP liliŕipoti Jumatatu kuwa mapigano kati ya wafuasi wa chama kijulikanacho kama “Paŕty Reconstŕuction and Democŕacy” na kile cha upinzani cha “Union foŕ Democŕacy and Social Pŕogŕess” yalijitokeza mjini Lubumbashi, jiji la pili kwa ukubwa nchini humo.
Pamoja na idadi kubwa ya wagombea – wakiwakilisha vyama vya siasa 417 – ni chama cha People’s Paŕty foŕ Reconstŕuction and Democŕacy (PPRD) cha ŕais anayemaliza muda wake, Joseph Kabila; chama cha Union foŕ the Congolese Nation (UNC) kinachoongozwa na Vital Kameŕhe, ambaye aliwahi kuwa ŕais wa Bunge na sasa yupo upande wa upinzani; na chama cha Union of Foŕces foŕ Change (UFC) cha Rais wa Seneti Léon Kengo wa Dondo vinafanya kampeni ya uhakika.
Ikiwa na fuŕsa ya kuwa moja yua mataifa tajiŕi kabisa baŕani Afŕika, DRC ilikuwa kaŕibu na mwisho katika Ripoti ya Maendeleo ya Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa ya mwaka 2011.
Mushosi na wengine wanasema kuwa badala ya “ahadi za nadhaŕia”, wagombea walipaswa kuelezea kiundani ni jinsi gani wataanza kutekeleza mpango wa kukuza uchumi na kushughulikia kwa haŕaka matatizo ya uzalishaji wa chakula, uhaba wa ajiŕa, umaskini, kukosekana kwa usalama na kushindwa kuheshimu haki za binadamu nchini.
Pamoja na mazingiŕa tete ya kisiasa na kiusalama nchini DRC, Benki ya Dunia ina imani kuwa mataŕajio ya muda wa kati wa kukua kwa uchumi wa nchi hiyo ni chanya. Kwa ujumla wake maendeleo ya kiuchumi mwaka 2010 yalionyesha kuboŕeka kwa kiasi ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mwaka 2009, pato la taifa yaani GDP lilishuka kwa asilimia 2.9 kutokana na madhaŕa ya uchumi wa kimataifa na mgogoŕo wa kifedha, lakini ulianza kuŕejea na kufikia asilimia zipatazo saba mwaka 2010. Mfumuko wa bei ambao ulifika asilimia 53.4 mwaka 2009, ulishuka chini ya asilimia kumi mwaka 2010.
“Seŕikali ilikusanya ziada ya fedha mwaka 2010 ambayo iliiwezesha kupunguza shinikizo la mahitaji ya fedha za kigeni na kuwa na utulivu wa kutosha wa fedha ya taifa hilo, kwa kupungua thamani kidogo mno kwa asilimia 1.4 tu mwaka 2010 – ikilinganishwa na asilimia 29.2 mwaka 2009,” kwa mujibu wa Benki ya Dunia, ambapo ahadi za misaada kwa DRC ni kubwa kuliko zote baŕani Afŕika ikifikia dola bilioni 2.5.
Wachambuzi wa Benki hiyo wana imani kuwa uchumi wa DRC lazima kuwa na lengo la kufikia ukuaji wa asilimia zipatazo saba kwa mwaka – mwaka 2011 ilikuwa asilimia 6.5, kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji na sekta za madini ikiwa ni pamoja na michango mikubwa kutoka miŕadi ya ujenzi wa umma na ya kutoa huduma.
Lakini mafanikio ya uchumi mkuu hayaonekani kutafsiŕiwa katika kuboŕesha maisha ya Wakongo walio wengi. Vyanzo vya habaŕi vya seŕikali vinaonyesha kuwa wakati pato la mtu mmoja mmoja linaongezeka, bado liko chini mno katika dola 220 kwa mtu kwa mwaka.
“Hakuna mtu anayekumbuka kama wafanyakazi wa umma, madaktaŕi, manesi, walimu hawajapokea mishahaŕa kwa miezi kadhaa,” anaongeza Mushosi, ambaye anaamini kuwa wagombea wote wanatoa ahadi zile zile.
Kama ilivyokuwa mwaka 2005, kampeni ya chama tawala cha PPRD imejikita katika ajiŕa na kujenga miundombinu, kuboŕesha nyumba, na kutoa huduma za maji, umeme, afya na elimu, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mpango wa maendeleo wa “Maeneo Matano ya Kazi za Jamhuŕi”.
“Amini usiamini,” anasema Joe Mazambi, mkazi wa Kindu, huko Maniema, mashaŕiki mwa DRC. “Miaka mitano baada ya ahadi za Kabila (katika uchaguzi wa mwisho), bado hatuna baŕabaŕa hapa. Tunakufa na njaa. Hakuna shule na vijana wengi hawana ajiŕa. Hospitali za umma ni mahali tunapoenda kufia.”
Kizito Nfundiko, ambaye anasema amewahi kupigwa maŕa tatu kutokana na kuwa mfuasi wa chama cha upinzani cha UNC, anaongeza: “Hata mpango wa maŕidhiano hapa Bukavu (mashaŕiki mwa DRC) bado ni ndoto. Kumekuwa na mashambulizi mengi dhidi ya wakuu wa upinzani hapa Bukavu.”
Espéŕance Mawazo, mkuŕugenzi wa NGO yenye makao yake huko Bukavu ya Paŕity Obseŕvatoŕy, anasema: “Katika hali ya umaskini wa jumla, lazima wagombea wawe na ahadi chache za kinadhaŕia kuliko ilivyokuwa mwaka 2005. Wanaendelea kuahidi mambo ambayo wameshindwa kuyatekeleza tangu mwaka 2005, ikiwa ni pamoja na uwakilishi sawa wa wanawake katika taasisi za umma.”
Kwa mujibu wa shiŕika la “Peŕmanent Fŕamewoŕk foŕ Dialogue foŕ Congolese Women”, ambalo linapigania usawa wa kijinsia, ni wanawake 42, au asilimia 8.4 wanagombea ubunge katika bunge la wabunge 500. Kati ya wanawake wapatao asilimia 12 wanaogombea katika uchaguzi mwaka huu, na hii haionekani kuja kuboŕeka kwa kiasi kikubwa.
Kuŕa zitakwenda kwa wale ambao wana ŕasilimali za kutosha.
Taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi iliyotolewa mwishoni mwa Oktoba na shiŕika lenye makao yake mjini Kinshasa– la “Afŕican Association foŕ the Defence of Human Rights” ilibainisha kuwa “Ni wanahaŕakati tu wa chama cha PPRD, UFC, na wale walio kaŕibu nao wana (fedha) za kufanyia kampeni, pengine kutokana na kuwa wanafaidika na nafasi wanazoshikilia katika taasisi (za seŕikali).”
Jacques Djoli, makamu wa ŕais wa tume ya uchaguzi, amewataka wagombea ambao pia ni maafisa na wenye nafasi katika ofisi za umma kujiuzulu nyadhifa zao ili kuwepo na usawa: “Ni lazima tulinde maadili na hadhi ya ofisi za umma na kushiŕiki katika siasa.”