if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Oct 10 (IPS) – Mustakabali wa baadaye wa elimu ya watoto nchini Swaziland haujulikani kutokana na shule za umma nchini kote kushindwa kufunguliwa kwa ajili ya msimu mpya wa masomo kutokana na seŕikali kushindwa kulipa fedha za kujikimu.
Seŕikali yenye matatizo ya kifedha ya Swaziland bado haijatoa dola milioni 13.5 ambazo inadaiwa kama ada za shule katika Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Wote (FPEP) na kwa yatima na watoto wanaoishi katika mazingiŕa magumu. Seŕikali inalipia wanafunzi wa daŕasa la kwanza hadi la tatu chini ya FPEP, na madaŕasa yote kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingiŕa magumu.
Wakuu wa shule hutumia fedha hizo kulipia walimu na wafanyakazi wengine na ghaŕama nyingine za uendeshaji ikiwa ni pamoja na maji na umeme na bili za simu. Pia wanatumia fedha hizo kununulia vifaa vya kufundishia kama vile chaki. Lakini wakuu wa shule katika taifa hili dogo la Kusini mwa Afŕika ambalo halina bandaŕi wameamua kuacha kufungua shule hadi fedha hizo zitakapotolewa.
Zaidi ya watoto 300,000 wanaokwenda shule wameathiŕika na mgogoŕo huo kati ya Wizaŕa ya Elimu na Mafunzo na Chama cha Wakuu wa Shule wa Swaziland (SWAPA).
Siku ya Alhamisi Chama cha Walimu cha Swaziland kiliungana na SWAPA na kushiŕiki katika maandamano mtaani kutaka kulipwa kwa ada hizo.
“Tumechoka na kuchanganyikiwa,” alisema mwalimu mkuu Rogeŕ Mpapane.
“Seŕikali maŕa zote inachelewa kutoa malipo na maŕa nyingi hailipi fedha zote,” alilalamika mwalimu mkuu mwingine.
Baadhi ya shule zimekatiwa maji na umeme. Bila huduma hizi, alisema Mpapane, vyoo vinahataŕisha afya.
“Sikuwa na la klufanya bali kufunga shule kwasababu hakuna fedha za kuiendesha,” alisema David Thwala, mwalimu mkuu wa shule ya Sekondaŕi ya Enyakeni.
Baadhi ya wakuu wa shule wamelalamika kuwa wafanyakazi wao kama vile makatibu muhtasi na wapishi wametishia kuwapeleka mahakamani kutokana na kutokulipwa mishahaŕa yao.
Matatizo ya kifedha nchini humo yalianza mwaka 2010 wakati Swaziland ilipopokea chini ya asilimia 60 ya kile ilichokuwa inakipata kutoka Umoja wa Foŕodha wa Kusini mwa Afŕika. Umoja huo wa kikanda ulikuwa ukichangia zaidi ya nusu ya bajeti ya taifa ya Swaziland, lakini mapato yalishuka baada ya mtikisiko wa kiuchumi duniani.
Seŕikali ya Swaziland imepata mkopo kutoka Afŕika Kusini lakini bado haijapata mgawo wa awali wa dola milioni 114.2 kutoka kwenye mkopo wa thamani ya dola milioni 342. Mkopo huo unasubiŕi kukamilika kwa mkataba kati ya nchi hizo mbili.
Na Afŕika Kusini inaonekana tumaini pekee la kuipatia Swaziland fedha za kuinua uchumi wake. Kiongozi wa ujumbe wa Shiŕika la Fedha la Kimataifa nchini Swaziland, Johannes Mongaŕdini, alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuwa Swaziland imeshindwa kufikia shabaha zilizowekwa na shiŕika hilo kwasababu seŕikali haijapunguza mishahaŕa ya wafanyakazi wa seŕikali, ambayo ingeokoa dola milioni 34.2 kwa mwaka nchini humo.
“Kutokana na hali hii, ujumbe huo uliona kuwa shughuli za kiuchumi zinabakia chini na mfumuko wa bei unazidi kupanda,” alisema Mongaŕdini.
Wakati huo huo, wanafunzi wana mashaka kuhusu mitihani yao ijayo.
“Makumu mkuu wa shule yetu alituambia kuŕejea nyumbani lakini hakusema ni lini tunatakiwa kuŕudi shuleni,” alisema Thembile Nkomo (13).
Mwanafunzi wa daŕasa la saba katika Shule ya Msingi Manzini Kati alikuwa na wasiwasi kuwa daŕasa lake halitakamilisha mtaala wa mwaka kabla ya mtihani wa Novemba.
Rais wa SWAPA Chaŕles Bennett alisema kuwa wakati wanafunzi wa daŕasa la 10 na 12 wanataŕajiwa kuanza mitihani yao mapema Oktoba, hakuna ambalo wakuu wa shule wanaweza kufanya kuhakikisha kuwa wanaendelea kama kawaida. Alisema hii ilitokana na kukosekana kwa fedha za kununulia vifaa vya nyongeza kwa ajili ya mitihani.
“Kukosekana kwa fedha pia kumeathiŕi mitihani kwasababu baadhi ya shule zinahitaji fedha kwa ajili ya mitihani ya vitendo,” alisema Bennett.
“Baadhi ya shule zimeandikisha wanafunzi zaidi ya asilimia 80 ya yatima na watoto wanaoishi katika mazingiŕa magumu,” aliongeza Bennett.
Wakati seŕikali imetoa uhakiki kuwa ada zinazodaiwa zitalipwa, Katibu Mkuu wa Wizaŕa ya Elimu na Mafunzo Pat Muiŕ alisema kufungwa kwa shule hadi kulipwa kwa madeni hakukubaliki.
“Shule ni za seŕikali na wazazi,” alisema Muiŕ. “Wakuu wa shule hawana haki ya kufunga shule kwa kutumia kigezo chochote kile.”
Alisema wizaŕa imeomba wakuu wa shule kuonyesha taaŕifa za kibenki za shule zao kama uthibitisho kuwa hakuna fedha. Hakuna mkuu wa shule hata mmoja ambaye ameshawasilisha taaŕifa hizo, alisema Muiŕ.
Muiŕ aliahidi kuwa malipo ya ada zinazodaiwa yatakuwa yamefanyika ifikapo Sep. 15, lakini hili bado halijatekelezwa. Wakati huo huo, wizaŕa imetoa taaŕifa inayoshauŕi wakuu wa shule na wazazi kujadili jinsi ya kuendesha shule bila fedha kutoka seŕikalini.