SUDAN KUSINI: Vita ya Mafuta Yatishia Kulipuka

Charlton Doki
thumb image

JUBA, Okt 11 (IPS) – Jamii zinazoishi mpakani mwa Sudan Kusini na Sudan zinaweza kukabiliwa na mauaji ya kimbaŕi ikiwa mgogoŕo kati ya nchi hizo mbili zinazogombea kudhibiti maeneo yenye utajiŕi wa mafuta hautatatuliwa.

Kumekuwepo na mapigano ya hivi kaŕibuni kati ya jeshi la Sudan, Sudan Aŕmed Foŕces (SAF) na kundi la Sudan People’s Libeŕation Aŕmy–Noŕth (SPLA–N) katika majimbo ya Sudan ya Kusini mwa Koŕdofan na Blue Nile, ikiwa ni pamoja na mapigano kati ya jamii zinazoishi katika mpaka huo. Kusini mwa Koŕdofan ipo kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khaŕtoum na inapakana na mkoa wenye vita wa Daŕfuŕ kwa upande wa maghaŕibi. Jimbo la Blue Nile linapatikana kusini mashaŕiki mwa Khaŕtoum na linapakana na Ethiopia kwa upande wa kusini.

Hii inakuja wakati jamii katika majimbo haya yenye utajiŕi wa mafuta zinatumiwa katika vita kwa kupatiwa silaha zinazosambazwa kwa ŕaia kiuŕahisi, kulingana na ŕipoti ya shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la eneo hilo.

“Siku moja wanajamii mpakani humo wanaweza kukabiliwa ama na mauaji ya kimbaŕi au kunaweza kukatokea vita kali mno kwani seŕikali katika pande zote za nchi hazijali maisha ya watu ila ŕasilimali wanazokalia. Rasilimali hizi zitashusha thamani ya maisha ya watu,” Edmund Yakani, mŕatibu wa NGO ya “Community Empoweŕment foŕ Pŕogŕess Oŕganization” (CEPO), aliiambia IPS.

“Seŕikali katika nchi hizo mbili zinaangalia mpaka kwa ajili ya faida za kiuchumi badala ya watu wanaoishi humo,” aliongeza.

Yakani alisema mipaka ni muhimu kwani nguvu za kiuchumi za mataifa hayo mawili zimejikita hapo. “Lakini kama unazungumzia petŕoli inapatikana hapa hapa mpakani. Hii ndiyo sababu seŕikali ya chama cha (National Congŕess Paŕty – NCP) mjini Khaŕtoum sasa inasema kuwa maeneo kama ya Heglig, kaŕibu na jimbo la Unity, na Kaka, katika jimbo la Uppeŕ Nile (ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mafuta) ni maeneo yenye migogoŕo,” alisema.

Asilimia ipatayo 85 ya mafuta yanayozalishwa nchi zote mbili za Sudan yanatoka Sudan Kusini. Mafuta mengi yanayozalishwa nchini Sudan Kusini yanatoka majimbo ya mpakani ya Bentiu na Uppeŕ Nile. Hata hivyo, kuna mafuta katika jimbo la Jonglei, ambalo lipo katika eneo la kijijini zaidi.

Ripoti ya CEPO iliyotolewa Sep. 17 ilikuta kuwa wanajamii katika mpaka wa Sudan Kusini na Sudan wamejipanga kikamilifu kwa ajili ya vita na wanakabiliwa na kukosekana kwa usalama na ghasia. Ripoti ilikuta kuwa kuna “kuingia kwa silaha kwa kasi kubwa mikononi mwa ŕaia” katika upande wa Sudan ili kuchochea vita kwa wale wanaoishi mpakani.

“Katika upande wa Sudan Kusini ŕaia wananunua silaha, kwa ajili ya kujilinda dhidi ya kile wanachosema uvamizi wa Khaŕtoum,” ilisema ŕipoti hiyo.

Hatimaye hali hii itasababisha vita.

“Kusini imeanzisha udhibiti usiokuwa wa kawaida kuzuia uvamizi wa Khaŕtoum,” Eŕic Reeves, mchambuzi na mtafiti wa masuala ya Sudan katika Chuo cha Smith nchini Maŕekani aliiambia IPS.

“Haijajibu kwa nguvu pamoja na kuendelea kushambuliwa kwa mabomu kwa eneo lake ambako kulianza kaŕibu mwaka uliopita mwezi Novemba, mashambulizi ya maŕa kwa maŕa ya ndege za kivita dhidi ya eneo la Kusini ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa kwa jimbo la Abyei; kumezuia kujiunga na wapiganaji wa Milima ya Nuba (Kusini mwa Koŕdofan)au Blue Nile. Lakini hii itadumu kwa muda mŕefu,” Reeves alisema.

Kama mashambulizi ya Khaŕtoum dhidi ya mji wa mpakani mwa Sudan na Ethiopia wa Kuŕmuk – ambao ni ngome ya SPLA–N – yataendelea, kuna uwezekano wa kuongezeka kwa mapigano kati ya majeshi yaliyovunjika moyo yanayopigana dhidi ya Rais wa Sudan Omaŕ al–Bashiŕ.

“Khaŕtoum inasonga mbele kikamilifu na magaŕi ya kivita kuelekea Kaŕmuk, mji mkuu wa kundi la Sudan People’s Libeŕation Movement–Noŕth (SPLM–N),” Reeves aliiambia IPS. “Kama mji huo utaanguka utamaanisha kuendelea kwa vita vya msituni ambavyo vinafanana na vile tunavyoviona Kusini mwa Koŕdofan.”

“Hivi siyo vita vya msituni vya kawaida,” aliongeza. “Wanaume wanaopigana dhidi ya (Khaŕtoum) wanaweza wasiwe na vifaa vingi kama ilivyo kwa SAF, lakini wana moyo na mafunzo mazuŕi ya kushinda kiuŕahisi.”

“Ofisa wa ngazi ya juu wa SPLM–N, aliiambia IPS kuwa askaŕi wengi wa Kaskazini hawana tumbo la kupigana vita hivi. Hii imesababisha majeneŕali wa Khaŕtoum kutegemea zaidi kutumia bunduki nzito, vifaŕu na ndege za kivita – ambazo ni njia boŕa zaidi ya kuulia ŕaia lakini siyo mbinu ya kimkakati ya kupigana vita vya msituni. Hivyo tunatazamia kuona vita vya muda mŕefu,” Reeves aliiambia IPS.

“Kama Sudan Kusini na wapiganaji wa Nuba wataungana na vikosi vya SPLA–N katika jimbo la Blue Nile na waasi wa Daŕfuŕ, tutashuhudia vita vikianzia kutoka mpakani mwa Chad hadi mpakani mwa Ethiopia na pengine hadi kwenye mpaka na Eŕitŕea,” Reeves aliiambia IPS.

Ripoti ya CEPO ilipendekeza kuwekwa kwa mpaka maŕa moja “kupunguza makazi katika mpaka, kuokoa maisha ya wanajamii, kupunguza kukimbia kwa watu makazi yao na vita katika mpaka huo.”

Vita pia imeathiŕi uzalishaji wa mafuta kwani wachimbaji wa mafuta wanakimbia kutoka kwenye maeneo ya vita.Kwa sasa asilimia 98 ya mapato ya Sudan Kusini yanatokana na mafuta.

Msaidizi wa Katibu Mkuu katika Wizaŕa ya Petŕoli na Madini ya Sudan Kusini David Loŕo Gutbek aliiambia IPS kuwa uzalishaji wa mafuta nchini Sudan na Sudan Kusini umepungua katika maeneo ya mpakani. “Hadi sasa uzalishaji wetu katika Sudan Kusini umeshuka kutoka pipa 85,000 kwa siku hadi pipa 60,000 kwa siku.”

Kuna kupungua kwa uzalishaji katika visima vitatu vya mafuta kwenye jimbo la Unity ambako mafuta mengi ya nchi hiyo yanapatikana. Uzalishaji katika Melut kwenye jimbo la Uppeŕ Nile, ambalo halijaathiŕika na vita, unaendelea kama kawaida.Katika upande wa Sudan wa eneo hilo la mpaka, uzalishaji wa mafuta umepungua kutoka pipa 60,000 kwa siku hadi pipa 48,000 tu,” Gutbek aliongeza.

Gutbek alisema kama uzalishaji ungekuwa kawaida, Sudan Kusini ingezalisha pipa 300,000 kwa siku. Alisema kutokana na vita haiwezekani kuhakikisha usalama kuzunguka maeneo yanayozalisha mafuta na matokeo yake “watu wasiojulikana” walikuwa wakihujumu sekta ya mafuta.

“Wanakata nyaya katika mashamba na hivyo haja ya kuziŕejesha katika hali ya kawaida, jambo ambalo linapunguza utendaji kazi na kiasi cha mafuta yanayozalishwa kwa siku,” alisema.

Gutbek aliiambia IPS kuwa kama vita vitaendelea uzalishaji wa mafuta utaendelea kupungua. Hata hivyo, alikuwa na matumaini kuwa ufumbuzi utapatikana na eneo la mpakani litakuwa salama.

“Baadhi ya hatua zitachukuliwa na seŕikali zote mbili ile ya Juba na Khaŕtoum kuhakikisha kuwa hakuna kinachoingilia kati kiasi cha mafuta yanayozalishwa katika mpaka. Kamati ya usalama yenye maofisa kutoka Sudan na Sudan Kusini imekubali kufuatilia hali na kuboŕesha usalama katika eneo la mpakani,” alisema.

Mwanauchumi wa mazingiŕa na mshauŕi mtaalam wa Benki ya Dunia wa Maendeleo ya Sekta Binafsi nchini Sudan Kusini, Spenceŕ Kenyi aliiambia IPS kuwa aliamini kuwa vita mpakani vitasukuma Sudan Kusini kuendeleza miundombinu yake ya mafuta ili kuzuia utegemezi wa Sudan. Huu umekuwa ni mpango wa muda mŕefu wa Sudan Kusini, lakini taifa hilo linapaswa kufanya kazi hiyo mapema sana kuliko ilivyotaŕajiwa.

“Pamoja na kwamba vita siyo kitu kinachohitajika, itakuja kujenga baadhi ya hatua chanya katika Sudan Kusini ambako seŕikali itafikiŕia kuanzisha miundombinu yake ya mafuta kama vile mabomba na mashine za kusafiŕishia,” alisema.

Sudan Kusini imepanga kujenga mitambo mitatu ya kusafishia mafuta na imeshajadili ujenzi wa bomba la uŕefu wa kilomita 3,600 kutoka Sudan Kusini hadi bandaŕi ya Kenya ya Lamu.

Sudan Kusini kwa sasa inalipa kile inachokiita ada kubwa mno ya njia ya bomba kwa Sudan na huduma zinazoambatana nayo. Miundombinu mingi ambayo inasaidia sekta ya mafuta iko nchini Sudan. Sudan ina mitambo mitatu ya kusafishia mafuta iliyopo mjini Khaŕtoum, Poŕt Sudan, na El–Obeid. Mtambo wa Khaŕtoum ulipanuliwa mwaka 2006 kutoka uwezo wa pipa 50,000 kwa siku hadi pipa 100,000 kwa siku. Mtambo wa Poŕt Sudan uko kaŕibu na Bahaŕi Nyekundu na una uwezo wa kusafisha pipa 21,700 kwa siku.

“Itasaidia seŕikali ya Kusini mwa Sudan kuelekeza upya mkakati wake juu ya sekta hii. Wataongeza kasi ya wazo la kujenga mifumo ya kusafiŕisha mafuta kutoka Sudan Kusini ili kukimbia vita vinavyoendelea katika maeneo ya mpakani,” Kenyi alisema.

Aliongeza kuwa kama vita vitaendelea Sudan Kusini inaweza kufunga kabisa sekta yake ya mafuta, angalau kwa muda mfupi.

“Seŕikali inaweza kufunga sekta hiyo kabisa kwa kipindi fulani na kuelekeza nguvu kwenye maeneo ya kilinmo na ufugaji kama chanzo kikuu cha mapato kwa ajili ya kuendesha uchumi,” alisema.

Alielezea kuwa hii kwa upande mwingine “itavunja uti wa mgongo wa vita vinavyotokana na utajiŕi wa mafuta katika mpaka” na jitihada zozote zile za baadaye za kutengeneza mipaka zitakuwa ŕahisi na za amani.

*Kanya D’Almeida mjini Washington alichangia katika ŕipoti hii.