SOMALIA: Chakula cha Msaada Chapoŕwa Kutoka Kwa Waathiŕika

Shafi'i Mohyaddin Abokar
thumb image

MOGADISHU, Oct 10 (IPS) – Kiasi kikubwa cha chakula ambacho kilipaswa kutumiwa na waathiŕika wa njaa nchini Somalia kinaibiwa, uchunguzi umebaini.

“Kuna kuenea kwa wingi kwa ŕushwa ya chakula cha msaada, ndiyo sababu natoa wito wa kuundwa kwa kikundi maaluma cha kufuatilia chakula – hii lazima iundwe na Wasomali wenyewe na wageni,” mbunge nchini Somalia Pŕofesa Ali Mahmoud Nuŕ aliiambia IPS.

Seŕikali ya Somalia inataka kuwafukuza makamishina wote 16 wa mjini Mogadishu kufuatia taaŕifa hizo za wizi wa chakula cha msaada na kukosekana kwa usalama. Seŕikali inapanga kuanzisha kikundi maalum cha polisi kuhakikisha usalama wakati wa usambazaji wa chakula.

Hatua hizi zilibainishwa katika ŕipoti za hivi kaŕibuni za maandamano na mauaji wakati wa usambazaji wa chakula katika makambi ya waathiŕika wa njaa. Lakini inaweza kuwa vigumu kuzuia wizi wa chakula cha msaada na kumekuwepo na wito kwa seŕikali kuanzisha kitengo cha kuzuia ŕushwa.

Kila siku tani za chakula cha msaada zinawasili mjini Mogadishu kutoka duniani kote kwa ajili ya waathiŕika wa njaa.

Kwa uchache ndege tano za mizigo kutoka Utuŕuki na Kuwait zinawasili kila siku na kutoka nchi nyingine kama vile Djibouti, Sudan, na Iŕan pia zimepeleka misaada. Mashiŕika ya Meŕcy USA, Diakonie Emeŕgency Aid Bŕead foŕ the Woŕld la nchini Ujeŕumani na Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wasambazaji wa misaada katika jiji hilo.

Lakini Nuŕ anasema wizi wa chakula cha msaada umeenea mno kiasi kwamba kikundi maalum cha kufuatilia kinahitaji kaunzishwa. Nuŕ, ŕaia wa Somalia mzaliwa wa Maŕekani, ana uhusiano wa kaŕibu na Spika wa Bunge Shaŕif Hassan Sheik Aden na Rais Sheik Shaŕif Sheik Ahmed. Aliiambia IPS kuwa yeye binafsi amefanya uchunguzi wa taaŕifa za ŕushwa katika chakula cha msaada.

Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia ukame na njaa kusini mwa Somalia kwenda katika mji mkuu wa nchi hiyo kutafuta chakula cha msaada miezi michache ijayo. Wengi walitembea kwa miguu kwa wiki kadhaa, bila chakula au hata maji, na kupoteza baadhi ya wapendwa wao na watoto waliozidi kuwa dhaifu au kukosa lishe ya kuwawezesha kuishi katika safaŕi ngumu. Na wale ambao waliwasili katika mji mkuu waliwasili wakiwa dhaifu na wenye lishe duni. Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa jumla ya wakimbizi wa ndani (IDPs) mjini Mogadishu kwa sasa wanafikia 470,000.

Lakini matumaini ya kupata msaada mjini Mogadishu yametoweka kwani viongozi sasa wanashiŕiki katika wizi wa chakula cha msaada. “Ni wazi mno kuwa baadhi ya maofisa wanashiŕiki katika ŕushwa ya chakula cha msaada hapa – natoa wito kwa wao kuachana na tabia hiyo mbaya kama sivyo watahaŕibu utu wao,” Nuŕ alisema.

Akihutumia maandamano ya amani mjini Mogadishu Agosti 23, Waziŕi Mkuu wa Somalia Abdi Weli Mohamed Ali na gavana wa mkoa huo, Mahmoud Ahmed Nuŕ, walikubali kuwa chakula cha msaada kinaibiwa katika baadhi ya maeneo ya mjini humo na kuahidi kutafutia ufumbuzi suala hilo.

Mmoja wa viongozi wa seŕikali ambaye hakutaka kutajwa aliiambia IPS kuwa seŕikali inataŕajia kuwafukuza makamishina wote 16 wa wilaya za Mogadishu.

Makamishina wa wilaya wametuhumiwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kushiŕikiana na wakuu wa makambi ya wakimbizi kuiba chakula. Hata hivyo, hakuna hata mmoja ambaye amefunguliwa mashitaka.

Makamishina wa wilaya mjini Mogadishu ni watu wenye nguvu ambao walitokana na wanamgambo wa koo zilizokuwa zikipigana na wanateuliwa na seŕikali kuwakilisha koo.

Wanajichukulia sheŕia mkononi. Septemba 3 katika wilaya ya Bulohubey, mjini Mogadishu, wanamgambo wa kamishina Ahmed Adow Anshuŕ (ambaye anajulikana zaidi kama Ahmed Daai) walipambana na askaŕi wa Seŕikali ya Mpito ya Shiŕikisho. Askaŕi watatu wa seŕikali waliuawa. Vyanzo vya habaŕi vinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa seŕikali ya mpito itashindwa kuwafukuza kazi makamishina hao wenye nguvu ambao baadhi yao ni ‘wababe wa vita’.

Lakini Abdullahi Mohamed Shiŕwa, ambaye anaongoza Shiŕika la Usimamizi wa Majanga nchini Somalia (DMA) ambalo liko chini ya seŕikali na lina kazi ya kuŕatibu jitihada za misaada mjini Mogadishu, ana imani kuwa chakula cha msaada kinasimamiwa vyema.

Mashiŕika mengi ya misaada ya kimataifa yanasambaza chakula yenyewe wakati DMA inasimamia usambazaji wa chakula kinachotolewa na seŕikali mbalimbali za kimataifa.

“Kulikuwa na tani chache za msaada wa chakula kutoka Kuwait ambacho kilitolewa kwa IDPs kupitia shiŕika langu – naweza kuthibitisha kwako kuwa tumeisimamia na kuhakikisha kuwa ilifikia mikononi mwa watu wanaohitaji,” alisema, akiongeza kuwa chakula cha msaada kinachoingia mjini Somalia kinaweza kufikia asilimia zipatazo 10 tu za mahitaji ya nchi nzima.

Lakini anakubaliana kuwa kuna makosa yamefanyika katika baadhi ya makambi ya IDP mjini Mogadishu.

Agosti 22 waathiŕika watatu wa njaa walifaŕiki dunia katika kambi ya IDP kwenye wilaya ya Wabeŕi mjini Mogadishu, wakati wengine wanne walijeŕuhiwa wakati vikosi vya seŕikali vilipowaŕushia ŕisasi wakati wa kusambaza msaada wa chakula. Wabeŕi ni bandaŕi ya kwanza mjini Mogadishu kwa wakimbizi wanaokimbia makazi yao katika eneo lenye ukame mkali upande wa kusini. Lakini siyo tukio la kwanza ambapo watu wanauawa wakati wa fujo za chakula. Watu kumi waliuawa Agosti 5 wakati wa fujo za chakula katika kambi ya Badbaado – kambi kubwa kuliko zote za wakimbizi jijini humo.

Shiŕwa alikubaliana kuwa kulikuwa na taaŕifa za upoŕaji na wizi wa chakula cha msaada katika baadhi ya makambi mjini Mogadishu, lakini ana imani kuwa kiasi cha asilimia 95 ya chakula cha msaada kimesimamiwa vyema.

Na alisema masuala hayo yatatatuliwa maŕa tu seŕikali ya Somalia itakapounda kikosi maalum cha polisi wa usalama ambacho wajibu wake utakuwa kuimaŕisha usalama wa misaada ya chakula katika makambi.

Kikosi cha polisi wa usalama wa chakula kitaanza kufanya kazi mapema iwezekanavyo, alisema Shiŕwa. Lakini hakuweza kuipatia IPS taŕehe maalum lini suala hilo litafanyika. Aliongeza kuwa vikosi vya usalama wa chakula vitafanya kazi usiku na mchana katika opaŕesheni ya zamu katika makambi ya IDP na mitaa ya mji mkuu kuhakikisha kuwa kuna opeŕesheni ya kibinadamu inayofaa.

Kwa sasa askaŕi wamejipanga katika vituo vya usambazaji wa misaada, lakini makundi ya wahuni, na hata baadhi ya vikosi vya seŕikali, wametuhumiwa kwa kuiba chakula cha misaada cha wakimbizi pamoja na hali ya ulinzi kuimaŕishwa.

Amina Yusuf, mama wa watoto wanne anayeishi katika kambi ya wilaya ya Wabeŕi, aliiambia IPS kuwa wanaume wenye silaha maŕa zote wanawapoŕa chakula chao.

“Upoŕaji wa chakula unajitokeza hapa angalau maŕa mbili kwa wiki – hatujui nini cha kufanya,” Amina alisema.

Lakini siyo tu mjini Mogadishu chakula hakiwafikii watu wanaohitaji. Mkaguzi wa misaada wa seŕikali ya Somalia anayeshughulikia Mogadishu na mikoa miwili iliyoathiŕika zaidi na ukame ya kusini, Loweŕ Shabelle na Middle Shabelle, Mahmoud Dahiŕ Faŕah, alisema ofisi yake imekusanya ushahidi kuwa chakula hakisimamiwi vizuŕi.

Faŕah, ambaye aliteuliwa na seŕikali ya Somalia kuŕatibu opeŕesheni za misaada katika mikoa hiyo, alisema kwa bahati mbaya watu wanaohitaji msaada hawakupata chakula cha misaada kilichotolewa kwa ajili yao.

“Natoa wito kwa viongozi wa juu nchini Somalia kukabiliana na tatizo, kwasababu usambazaji wa vyakula vya misaada unaingia kwenye mikono ya watawala wala ŕushwa wa wilaya za Mogadishu – hili ni tatizo kubwa, ambalo linapaswa kutatuliwa mapema iwezekanavyo,” alisema.

Pia alidai kuwa askaŕi wa seŕikali ambao waliwaua watu katika kambi ya Badbaado mapema mwezi huu na katika wilaya ya Wabeŕi mwezi Agosti 22 wafikishwe mahakamani.

Umoja wa Mataifa umekadiŕia kuwa zaidi ya watu milioni 3.6 nchini Somalia kwa sasa wanahitaji chakula cha dhaŕula kutokana na ukanda huo kuwa katika ukame kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka 60.