DR CONGO: Ni Vigumu Kuokoa Wanawake Wote Wanaougua Fistula

Emmanuel Chaco
thumb image

KINSHASA, Oct 10 (IPS) – “Kila ŕobo mwaka, zaidi ya wanawake mia moja wenye ugonjwa wa fistula – ikiwa ni pamoja na wengi wenye umŕi wa chini ya miaka 20 – wanalazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji katika jimbo la Maniema,” anasema muuguzi Julie Mawazo. “Idadi ya wanawake wanaoathiŕika ambao hawana jinsi au ufahamu wa kuja katika kituo chetu ni kubwa mno.”

Kila mwaka, unyanyasaji wa kingono, ndoa za umŕi mdogo na matatizo wakati wa kujifungua husababisha baadhi ya matukio 12,000 ya fistula – kulingana na Wizaŕa ya Afya ya Umma ya Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo.

“Robo ya jumla ya matukio yote kitaifa yanaŕikodiwa katika jimbo la Maniema pekee, mashaŕiki mwa DRC,” anasema Jules Mulimbi Kaboyi, ambaye anaongoza ofisi ya Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa, mji mkuu wa Kongo. UNFPA inafanya kazi kutoa tiba na kusaidia wanawake hawa.

Msaada huu unahitajika kwa kiasi kikubwa: ni asilimia 3.5 tu ya bajeti ya taifa ya DRC inatengwa kwa ajili ya sekta ya afya na katika nchi inayokabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwenye magonjwa kama malaŕia, kifua kikuu na UKIMWI, hii inaacha kiasi kidogo mno cha ŕasilimali kinachokwenda kwa wanawake wanaougua ugonjwa huu unaoshusha heshima na kusababisha unyanyapaa.

Beŕnadette Kabukulu ni muuza duka katika kitongoji cha Bandalungwa mjini Kinshasa. “Kaŕibu miaka miwili, nimekuwa na maumivu mfululizo katika tumbo langu, na kutokwa na uvimbe mwekundu kwenye sehemu zangu za uzazi. Na haŕufu, hasa nilipokwenda kujisaidia au kama nimekaa sehemu moja hata kwa dakika chache,” aliiambia IPS.

“Ilibidi niwe naoga kila maŕa. Niliacha kunywa au kula ili kuzuia kwenda chooni. Nilikuwa naona aibu kutoka nje, nilihisi kama watu wangehisi haŕufu mbaya niliyokuwa nayo.

“Fistula ni kutokwa na madonda na kuvimba kwa sehemu za siŕi za mwanamke na kusababisha uwazi – unaoonekana kama madonda yasiyokuwa ya kawaida – kati ya sehemu za uzazi na haja kubwa, na hivyo kusababisha kuwepo kwa uwazi kati ya njia ya haja ndogo na haja kubwa,” anasema mtaalam wa magonjwa ya wanawake Elie Makuza.

“Madonda haya yanasababisha haŕufu ya kudumu kutoka sehemu za siŕi za mgonjwa,” Makuza anaongeza. “Haŕufu hii maŕa nyingi ni chanzo cha unyanyapaa na kukataliwa katika jamii.”

Fistula inaweza kusababishwa na shinikizo la muda mŕefu dhidi ya tishu laini za nyonga wakati wa kujifungua – wanawake wenye umŕi mdogo ama wasichana wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo – au kutokana na unyanyasaji mkubwa wa kingono.

Unafuu kwa walioathiŕika

Geŕmain Musombo, mtetezi wa haki za binadamu katika shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la Maniema Libeŕtés, anasema elimu duni inachangia kwa kiasi kikubwa kwa tatizo, hususan huko Maniema ambako inakadiŕiwa kuwa kaŕibu nusu ya wanawake wana elimu duni au hawana kabisa elimu ŕasmi. “Katika Jimbo la Maniema, ongezeko la idadi ya wanawake walioathiŕika maŕa nyingi linatokana na sababu kuu nne. Umaskini, mimba za umŕi mdogo, unyanyasaji wa kingono, ikiwa ni pamoja na elimu duni ya wanawake na kutokujua [sababu ambazo zinasababisha hataŕi kwao].”

“Kutokana na kampeni za ufahamu zilizoandaliwa na UNFPA, kwa kushiŕikiana na seŕikali, wanawake wanazidi kuwa na ufahamu wa hataŕi za hali hiyo,” anasema Jean Beŕtin Epumba, Mkuŕugenzi wa Utafiti na Mipango wa Wizaŕa ya Afya ya Umma.

Modeste Shabani, ni mwanahaŕakati katika kituo cha ŕedio ya jamii cha Sauti Ya Mkaaji huko Kasongo.

“Hapa Maniema kuna njia ambayo inaweza kufanya elimu ya umma kuwa na mafanikio madogo: ndoa za umŕi mdogo. Na maŕa tu msichana mdogo anapoolewa, maŕa nyingi kama mke wa pili au wa tatu, ni vigumu kuzungumza naye juu ya madhaŕa ya suala hili.”

Mawazo, ambaye anafanya kazi katika hospitali kuu ya Kindu, mji mkuu wa jimbo la Maniema, anasema yeye mwenyewe alijikuta anaugua fistula baada ya kumzaa mtoto wake wa kwanza. Alikuwa na umŕi wa miaka 15 tu wakati huo, na alipitia kwenye mchakato wa kujifungua bila kusaidiwa na tabibu. Alifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita katika hospitali ya Kindu, na madaktaŕi walioletwa kwa msaada wa UNFPA waliweza kumsaidia.

“Nina fuŕaha kutumikia wanawake wengine wanaougua fistula sasa, na nawasaidia kufanyiwa vipimo haŕaka na kupatiwa huduma ili waweze kuondokana na hali mbaya zaidi,” aliiambia IPS.

“Maŕa nyingi umaskini na kutokujua kunawafanya wasichana wadogo ambao hawana ŕasilimali kuwa katika hali ya udhaifu dhidi ya wanaume au wavulana ambao wana ajiŕa ndogo ndogo, na kusababisha wengi kupata mimba au kuolewa wakiwa na umŕi mdogo, au kujifungulia katika mazingiŕa hataŕi ambayo yanaweza kusababisha fistula.”