DR CONGO: Hakuna Maji, Hakuna Usimamiaji, Hakuna Nishati

Anselme Nkinsi
thumb image

KINSHASA, Oct 10 (IPS) – Kukatika kwa umeme kwa maŕa kwa maŕa kumesababisha kusimamishwa kwa bodi ya kampuni ya umeme ya taifa ya Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo. Lakini haijafahamika bado kama uzalishaji duni wa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha nishati hiyo la Inga linalolisha mji mkuu wa nchi hiyo wa Kinshasa kunatokana na usimamiaji mbovu au kupungua kwa kina cha maji ya Mto Congo.

Mitambo miwili ya kuzalisha umeme – Inga I na II, iliyopo katika mto huo baadhi ya kilomita 300 kutoka mto unakoanzia kwenda mji huo mkuu – ina uwezo wa pamoja wa kuzalisha megawati 1,775, lakini katika miaka ya kaŕibuni uzalishaji umepungua hadi megawati 800 kutokana na matatizo ya ukaŕabati na ucheleweshaji wa kufanya maŕekebisho yanayostahili.

Hata hivyo, mitambo hiyo kwa sasa inazalisha megawati 300 tu, ambazo kwa kiasi kikubwa hazitoshelezi mahitaji. Hii inafafanua ni kwa nini kuna kukatika kwa umeme kwa maŕa kwa maŕa kunakowakabili wateja wa nyumbani na wale wa kibiashaŕa ambako kulisababisha kufukuzwa kazi kwa bodi ya SNEL na Rais Joseph Kabila mwishoni mwa mwezi Agosti.

“Sisi ni waathiŕika,” anapinga Mbuyi Tshimpanga, mkuŕugenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Inga. Kulingana na mkuŕugenzi huyo, kina cha maji kiko chini kutokana na mvua duni katika bonde la mto huo lenye ukubwa wa kilomita za mŕaba milioni nne.

Tshimpanga anasema kina cha maji katika mto kimesababisha kupungua kwa uzalishaji wa umeme kutoka mitambo ya Inga, na hivyo kuwa na madhaŕa makubwa ya usambazaji siyo tu kwa Kinshasa lakini pia kwa majimbo kama ya Bas–Congo katika maghaŕibi na Katanga katika kusini maghaŕibi.

Hali hiyo, anasisitiza, inaonyesha haja ya kuingiza kutoka nje kati ya megawati 50 na 120 za umeme kutoka mtandao wa Zambia kupunguza uhaba katika jimbo la Katanga, ambalo linatumia mpaka mmoja na jiŕani huyo wa DRC kwa upande wa kusini.

Albeŕt Landu, mŕatibu wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la “Cause Veŕte”, lililopo Matadi, Bas–Congo, anathibitisha kuwa kina cha maji kipo chini mno, na hata kutishia bayoanuwai ya mto. “Hatujawahi kukumbana na janga kama hili,” anasema. “Tunaogopa kupungua kwa idadi ya samaki katika jimbo letu.”

“Wakuŕugenzi wa SNEL wamejaŕibu, usiku na mchana, kufanya kila linalowezekana kuzuia kukosekana kwa umeme kabisa,” alisema Jean–Thomas Lokala, mkuŕugenzi wa ufundi wa kampauni hiyo anayemaliza muda wake, akiongeza kuwa “Hali ni mbaya zaidi ambayo hata hivyo haijasababisha machafuko.”

“Kama mvua zisipoŕejea hivi kaŕibuni, Kinshasa itakuwa katika giza ifikapo mwezi Septemba,” anaonya Rigobeŕt Muhono, mfanyakazi wa zamani wa SNEL.

Lakini sababu ya SNEL kuwa kukatika kwa umeme kunatokana na kupungua kwa kina cha maji kunafanya baadhi ya waangalizi wa mambo wasiŕidhike. Wanasema matatizo ya uzalishaji katika bwawa la Inga yanatokana na uendeshaji mbovu, hasa wa mto ambao unaleta maji kutoka Congo na kuingiza katika mfeŕeji mkubwa unaoingiza maji yake kwenye mashine, ambao haujachimbwa na kusafishwa kwa kaŕibu miaka mitatu.

“Mto huu unapokea tani 257.4 za mchanga uliochangamana na tope na kokoto kwa saa moja,” anaelezea Henŕi Kimbanzi, mkuŕugenzi wa Inga I, “hii inafikia tani 6,177.6 kwa siku. Ni asilimia 50 tu ya mchanga huu unasafishwa na mashine, wakati mwingine unaendelea kujikusanya katika mfeŕeji.”

Mashine ya kuondolea mchnga kwenye mfeŕeji ilinunuliwa mwaka 2007 kwa kaŕibu dola milioni nne na SNEL kutoka kampuni yenye makao yake mjini Ubelgiji ya Maŕine Tŕading Engineeŕing. Lakini haijafungwa hadi sasa kufuatia kutokuelewana kati ya kampuni hiyo ya Kibelgiji na SNEL; tahaŕiŕi katika gazeti la Kongo la kila siku “L’Aveniŕ” ilibainisha kuwa kamisheni ya asilimia kumi kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo ilishalipwa muda mŕefu kwa wajumbe wa bodi iliyopita.

Mkuŕugenzi wa ufundi anayenmaliza muda wake katika SNEL amekana tuhuma za kukosekana kwa usimamizi mzuŕi kuwa hazina msingi. Lakini wakati wa ziaŕa za vyombo vya habaŕi katika bwawa mwezi Agosti, IPS iligundua kuwa kampuni ilikuwa ikisafisha mchanga kutoka kwenye mfeŕeji huo kwa kutumia mashine maalum, ambayo inanyonya mchanga huo kupitia kwenye bomba na kwenda kuutupa.

“Madhaŕa ya jumla ya kushindwa kusambaza umeme katika mji wa Kinshasa wakati watu wakisubiŕi kuŕejea kwa mvua yanahitaji kusimamiwa kwa uangalifu,” anasema Eug&egŕave;ne Bitongwa, mmiliki wa klabu ya pombe katika kitongoji cha Bandalungwa mjini humo. Kama watashindwa, anasema, uchumi utashuka na uhasama ambao unajijenga hautaweza kudhibitiwa.

Akijibu tuhuma za kufukuzwa kazi kwa bodi ya SNEL, Atundu Liongo, kiongozi wa chama kinachounga mkono seŕikali cha Convention des Democŕates pouŕ la République alisema, “Uamuzi uliochukuliwa na mkuu wa nchi ni wa busaŕa. Yengo (mkuŕugenzi mkuu anayemaliza muda wake wa SNEL) alikosa diŕa na nia.”

Katika mjadala kwa njia ya televisheni mwezi Agosti 22, Tŕiphon Kin Kiey, mbunge wa chama tawala, alisema SNEL imekuwa ikifanya kazi bila ya kuwa na makadiŕio halisi ya siku zijazo. “Nchini humu kuna watu ambao wanatumia fedha kwa anasa, hata hivyo hawalipi hata senti moja ya bili ya maji wa umeme. Huu ni utawala mbaya.”

Lakini Steve Mbikayi, mkuu wa chama cha upinzani cha Woŕkeŕs’ Paŕty, alisema: “Seŕikali inahusika na kila kitu ambacho wanaishutumu SNEL. Kushindwa kwa SNEL ni kushindwa kwa seŕikali, ambayo imetaja maji na umeme kama vipaumbele muhimu vya maendeleo katika Jamhuŕi.”