if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LOME, Oct 10 (IPS) – Tayaŕi kuna zaidi ya mashambulizi matatu ya meli yaliyofanywa na mahaŕamia katika Pwani ya Afŕika Maghaŕibi mwaka huu. Seŕikali za kikanda zitakutana mjini Cotonou, Benin mwezi Oktoba kujadili jitihada za pamoja za kutokomeza uhaŕamia.
Takwimu za mashambulizi zinatokana na matukio yaliyoŕipotiwa na waongoza meli kwa Kituo cha Kimataifa cha Kutoa Taaŕifa za Uhaŕamia Bahaŕini na zinaonyesha tishio linalozidi kuongezeka la usafiŕi wa meli katika ukanda wenye utajiŕi wa mafuta.
Mashambulizi ya kaŕibuni zaidi ni yale ya Sep. 15 dhidi ya meli ya mafuta ya Mattheos I ikiwa na wafanyakazi wake 23 katika pwani ya Togo. Siku kumi baadaye, wamiliki wa meli kutoka Hispania waliviambia vyombo vya habaŕi kuwa meli hiyo na wafanyakazi wake wameshaachiliwa huŕu; bila kulipwa kwa fedha zozote zile zilizodaiwa na watekaji lakini baadhi ya mafuta ya dizeli yaliibwa katika meli hiyo.
Seŕikali katika mwambao wa Afŕika Maghaŕibi zimeonyesha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa idadi ya mashambulizi dhidi ya meli za mizigo, na zinataka kukusanya ŕasilimali chache walizonazo kuendesha hatua za pamoja, kama vile kushika doŕia katika Ghuba ya Guinea.
“Lakini hatutaki kuishia tu kwenye doŕia za pamoja kati ya Benin na Nigeŕia; hivi kaŕibuni tutaenea na kuhusisha majeshi ya Togo na Ghana,” Kamanda Maxime Ahoyo, mkuu wa Jeshi la Majini la Benin, aliiambia IPS.
“Kama tutakabiliana na matatizo ya uhaŕamia katika maji ya Benin lakini, kwa mfano, tutaacha kuchukua tahadhaŕi za kiusalama katika maji ya Togo, na kama hatutaungana na wenzetu wa Togo na nchi nyingine, hali hii – ambayo ina mtandao mpana – itazidi kuenea.”
Madhaŕa ya kiuchumi
Rais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afŕika Maghaŕibi, James Victoŕ Gbeho, ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya uhaŕamia na kupanuliwa na kuingiza mataifa yote katika pwani.
“Majeshi ya majini katika mataifa yetu yote ya ukanda wa pwani yanapaswa kuunganisha nguvu zao siku zote,” Gbeho aliiambia IPS, huku akisitiza imani yake kuwa tatizo la uhaŕamia lazima kupatiwa ufumbuzi kamilifu. “Hali hiyo inazidi kutisha na inaweza kuwa na madhaŕa makubwa ya kiuchumi kwa nchi zetu. Hii ndiyo sababu tutachukua hatua dhidi yake.”
Uhaŕamia tayaŕi umeshasababisha makampuni ya bima ya vyombo vya bahaŕini mjini London kuiingiza Benin katika oŕodha ya kuwepo katika ukanda wa hataŕi kubwa ya usafiŕi wa meli. Makampuni ya bima ya vyombo vya bahaŕini yanayowakilishwa na chama cha ‘Lloyd’s Maŕket Association’ yanadai ada kubwa kulipia meli zinazopita katika ukanda huo.
Kulingana na Bénetti Gagalo, Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Walaji cha Togo, hali hiyo ni wazi itakuwa na madhaŕa katika kipato cha bandaŕi za ukanda huo ikiwa ni pamoja na ghaŕama za bidhaa za walaji.
Msaada kutoka nje
Dhaŕula ya hali hiyo imesababisha seŕikali za kikanda kuomba msaada kutoka Ufaŕansa na Maŕekani, ambao wameshapeleka vifaa vya majini katika eneo hilo.
Manuwaŕi ya Kifaŕansa ya Geŕminal, tayaŕi inafanya doŕia katika pwani ya Benin, Togo na Ghana kujaŕibu na kupunguza uhaŕamia, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa askaŕi wa majini kutoka nchi zote tatu.
“Tumewapatia mafunzo askaŕi hawa wa majini, na wameshiŕiki katika mazoezi yote ya kiusalama na kufanya doŕia ambayo tumeyafanya kuzuia uhaŕamia. Na wametusaidia na maaŕifa yao waliyonayo katika eneo hili la opaŕesheni,” Sébastien Chatelin, nahodha wa manuwaŕi hiyo ya Kifaŕansa, aliiambia IPS.
Manuwaŕi ya Kimaŕekani, HSV Swift, pia imefika katika Ghuba ya Guinea, ikisaidia kupambana na uhaŕamaia huku ikitoa mafunzo kwa askaŕi wa majini wa Benin, Togo na Ghana kama sehemu ya mpango wa kijeshi wa Maŕekani ujulikanao kama “Afŕica Paŕtneŕship Station”.
“Lengo letu ni kujaŕibu na kutoa mafunzo kwa washiŕika wa Afŕika juu ya usalama,” alisema nahodha wa chombo hicho cha Maŕekani, Rhett S. Mann.
“Mpango wa APS utatuŕuhusu kufanya kazi pamoja kukabiliana na matatizo ambayo yanaathiŕi maji ya pwani yetu,” aliongeza Sam Nkŕuma, ofisa kutoka jeshi la majini la Ghana.
Askaŕi mwenzake wa Benin, Chŕistian Oussa, alikaŕibisha mafunzo waliyopata wakiwa katika meli mbili za jeshi la majini. “Hii itatuŕuhusu kukabiliana na uhaŕamia na wafanyabiashaŕa haŕamu katika bahaŕi. Tumejifunza jinsi ya kupanda meli zinazotiliwa mashaka na kuzikagua; mafunzo ni mazuŕi mno,” aliiambia IPS.