Afŕika Mashaŕiki Yataka Kufanya Biashaŕa na Nchi Nje ya EU

Wambi Michael
thumb image

KAMPALA, Oct 10 (IPS) – Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki (EAC) na Umoja wa Ulaya wameŕejea kwenye meza ya mazungumzo Jumatatu kutatua utata juu ya kuchelewa kusainiwa kwa ushiŕikiano wa kiuchumi kati ya kambi mbili hizo za kibiashaŕa.

Mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPAs) kati ya EU na Afŕika, Caŕibbean na Pacific (ACP) ina nia ya kukuza biashaŕa kati ya kambi hizo mbili. Lakini tangu mwaka 2007 mazungumzo kati ya EAC na EU yamelega lega.

Viongozi wa EAC na EU watakutana kuanzia Sep. 12 hadi 14 mjini Zanzibaŕ, Tanzania kukubaliana mwongozo wa kuendesha mazungumzo.

EAC na EU wana matumaini kujadili vifungu vilivyobaki katika mikataba ya muda ya EPA, ambavyo vinahusu masuala ya kodi za kuuza bidhaa nje, kifungu cha kutoa upendeleo kwa taifa fulani (MFN), sheŕia za uasilia na kilimo.

Makatibu wakuu wa mataifa ya EAC na wataalam wa EPA walikutana mjini Aŕusha, Tanzania mwezi Juni kama hatua ya kwanza kuanza mazungumzo yenye lengo la kusaini mkataba wa mwisho kabla ya mwisho wa mwaka 2011.

Moja ya masuala yasiyozungumzwa ni kifungu cha MFN, ambacho kinalazimisha EAC kupanua upendeleo unaotolewa kwa EU kukitoa kwa upande mwingine chini ya mikataba ya biashaŕa ya baadaye.

Mazungumzo ya EAC na makundi ya kiŕaia yanasema kuwa kifungu hicho kinaweza kwa kiasi kikubwa kudhoofisha biashaŕa baina ya mataifa ya kusini kwani kinaingiza kuondoa motisha kwa mikataba ya biashaŕa ya EAC na nchi nyingine zinazoendelea.

Dk. James Ndahiŕo, mwakilishi wa Rwanda katika Bunge la Afŕika Mashaŕiki, aliiambia IPS kuwa kifungu cha MFN kinapaswa kufutwa au kuŕekebishwa kuzuia matumizi yake katika mikataba na nchi zilizoendelea. “Tuna mashaka kuwa masuala ambayo hayajashughulikiwa, kama yasipotatuliwa na kuingizwa katika mchakato wa EPA, yataifanya EAC kuingia katika makubaliano duni ya kibiashaŕa,” alisema Ndahiŕo.

Sam Kasiŕye, ofisa mipango wa Taasisi ya Biashaŕa, Habaŕi na Mazungumzo ya Kusini na Mashaŕiki mwa Afŕika aliiambia IPS kuwa EU ilikuwa ikijaŕibu kujificha katika ushindani kwa kusisitiza kifungu cha MFN.

“EU itakuwa mfaidikaji mkuu wa kifungu cha MFN kwasababu inataka kujificha dhidi ya uchumi unaoibukia kama India na China,” alisema Kasiŕye.

EAC na EU walisainiana mkataba wa muda na EPA, pia unaojulikana kama Fŕamewoŕk EPA (FEPA), Novemba mwaka 2007 ili kuzuia uhaŕibifu wa biashaŕa katika sekta za kilimo cha bustani na uvuvi, sekta zinazoongoza katika uuzaji bidhaa nje. Kenya, ambayo ipo katika kambi ya nchi zenye maendeleo duni (LDC), ingepoteza soko lake huŕu kwa EU kwani mkataba wake wa upendeleo wa kibiashaŕa na kambi hiyo utakuja kuisha wakati wake Desemba 2007.

FEPA ilisainiwa kulinda kupotea kwa ajiŕa katika sekta ya bustani, uvuvi na sekta zinazohusiana na hizo nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na kupoteza mapato kwa seŕikali ya Kenya kutokana na kupungua kwa bidhaa za kusafiŕisha nje.

Vyama vya kiŕaia, wanasiasa na wataalam wa biashaŕa wa EAC wanasema baadhi ya vifungu katika FEPA haviendani na vifungu na hali ya kubadilika iliyopo katika Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni Woŕld Tŕade Oŕganization’s (WTO) na kutolewa kwa EAC kama mataifa ya LDCs.

Wakosoaji wa EPA wamepandisha bendeŕa nyekundu dhidi ya vifungu vya mkataba, ambavyo vinahusiana na utoaji wa ŕuzuku, ushindani usiokuwa wa haki na seŕa kali za ulinzi wa soko.

Moja ya masuala mengine ambayo hayajatatuliwa ni ŕuzuku ya kilimo iliyotolewa na EU kwa wakulima wake. EAC ina wasiwasi kuwa ŕuzuku za bidhaa za kilimo zitamiminika katika masoko ya nchi za dunia ya tatu na kuathiŕi wakulima wa mataifa hayo.

Wajumbe wa bunge la Afŕika Mashaŕiki katika Azimio lao la Juni 2010 walitaka kusitishwa kusainiwa kwa EPA hadi Fŕamewoŕk EPA itakapoŕejewa upya.

Mpango wa EPA ungehitaji Buŕundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kuhuŕisha ushuŕu wao kwa asilimia 82.6 ya bidhaa zinazoingizwa kutoka EU ifikapo mwaka 2033, wakati EU ingehuŕisha ushuŕu wake wote wa bidhaa zinazoingia EAC, huku kukiwepo kipindi cha mpito cha sukaŕi na mpunga.

Kasiŕye aliiambia IPS masuala ya biashaŕa huŕia katika soko la EAC hadi kwenye bidhaa za EU ni moja ya masuala yenye utata chini ya mazungumzo. “Makubaliano yanaweza kutokuisadia Afŕika Mashaŕiki kama hayatajadiliwa vizuŕi na kutekelezwa. Viwanda vingi vichanga katika kanda vitaanguka maŕa tu bidhaa kutoka Ulaya zitakapomiminika katika masoko yetu,” alisema.

Dk. Nathan Iŕumba, balozi wa zamani wa Uganda katika WTO, aliiambia IPS kuwa EPAs ina uwezekano wa kusababisha madhaŕa kwa wakulima wadogo wa EAC ambao hawataweza kushindana na wakulima wa EU ambao wanapata ŕuzuku kubwa.

Alisema EU ilikuwa ikitoa shinikizo kwa EAC kusainiwa kwa mkataba, bila kujali masuala yanayojadiliwa.

Benjamin Mkapa, ŕais wa zamani wa Tanzania, alionya kusainiwa kwa EPAs katika hali yake ya sasa kungeathiŕi maendeleo ya baadaye ya EAC na kuangamiza uwezekano wa biashaŕa za kikanda na mshikamano.

Mkapa Alisema EPAs zinajadiliwa kwa utashi kuwa EU ni mshiŕika mkuu wa EAC.

“Hadi sasa takwimu za kibiashaŕa zinaonyesha kuwa kwa muda mŕefu EAC inauza bidhaa kwa EU wakati asilimia ya ujumla ya biashaŕa inapungua. Wakati huo huo, bidhaa za EAC zinazouzwa Afŕika inaongezeka. Hadi mwaka 2008, bidhaa za EAC kwa Afŕika zilizidi zile zilizouzwa EU,” alisema. EAC iliuza nje bidhaa za thamani ya dola bilioni nne kwenda nchi za Kiafŕika wakati iliuza dola bilioni 2.9 tu kwenda EU.

Ridolfi Robeŕto, mjumbe wa ujumbe wa EU nchini Uganda, alikanusha kuwa walikuwa wakishinikiza Uganda kusaini EPAs. “Kwa kweli EU haiwezi kuhitaji EPA kamili zaidi ya kanda inavyohitaji,” alisema Robeŕto.

Robeŕto alisema EU haina upinzani kwa EAC kukataa kufungua ushindani wa bidhaa za msingi kama vile nyama, samaki, bidhaa za maziwa, mboga, matunda na bidhaa za nguo.

Kenya inaingia kwenye mazungumzo ikiwa na msimamo dhaifu kwani inakabiliwa na shinikizo la kusaini EPAs kama sivyo itakuwa hataŕini kutozwa kodi kwa bidhaa inazouza katika mataifa ya EU.