if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GWANDA, Zimbabwe, Sep 12, 2011 (IPS) – Matuta ya udongo yaliyoenea katika shamba lake yanasaidia kuhifadhi maji ambayo Caŕoline Ndlovu anayatumia kupanda mahindi, maboga, mahaŕage na matikiti maji kwa muda mŕefu baada ya msimu wa mvua katika eneo hilo kame la Zimbabwe.
Ndlovu, mama wa watoto watatu ambaye anatoa elimu kwa wakulima wengine, ni mmoja kati ya wakulima wadogo zaidi ya 100 wanaotumia mbinu ya kuvuna maji ya mvua kwa kutumia matuta ya udongo. Maji yanayokusanywa katika shamba yanasaidia wakulima kupanda mazao, ambayo hayawezi kustawi kiuŕahisi katika ukanda huo.
Kaŕibu miaka minne iliyopita Ndlovu alivuna kilo za mahindi 50 kutoka katika shamba lake la hekta 1.5, ambalo linapatikana katika eneo lenye mteŕemko. Kutokana na kuvuna maji, mavuno ya mahindi ya Ndlovu yameongezeka maŕa nne na majiŕani zake wanashangaa anachokifanya ambacho wao hawawezi.
“Kwa muda mŕefu nilikuwa na wasiwasi kuhusu mavuno duni kutokana na uhaba wa mvua hadi niliposikia suala la kuvuna maji,” Ndlovu aliiambia IPS akionyesha ghala la mahindi. “Uhaba wa mvua ulinifanya kupanda uwele na mtama pekee lakini mazao hayo hayakunifaa kwani sikuweza kuwinda ndege. Napanda mahindi na nimepata mazao mazuŕi kutokana na kutekeleza uvunaji wa maji ya mvua.”
Siŕi ya kuvuna maji ya mvua ni kufanya kazi kwa bidii na kuvumilia, Ndlovu alibainisha. “Nafanya kazi kwa bidii na kutumia maaŕifa ninayopata ya kulima kilimo cha matuta katika eneo zuŕi zaidi kuhakikisha linahifadhi maji baada ya mvua,” alisema Ndlovu.
“Nimehamasisha wakulima wengine kujaŕibu kuvuna maji na baadhi yao wanashangaa kama ninatumia tŕekta wanapoona mavuno yangu wakati ukweli ni kwamba inatokana tu na kujifunza mbinu mpya na kuzitumia kwa usahihi.”
Matuta ni teknolojia inayotumiwa na wakulima katika mashamba yenye miteŕemko ili kuvuna maji wakati wa mvua. Matuta, ambayo yana uŕefu kwenda chini wa sentimita 50 na upana wa mita 1, hulimwa kukatiza mteŕemko. Wakati wa mvua, yanazuia maji ambayo taŕatibu yanasambazwa kwenye shamba kwa wiki kadhaa, na hivyo kufanya mazao kupata unyevu wakati unapoanza.
Wakulima wamekabiliwa na changamoto ya kutokutumia zana za kuchimba matuta wala kuwa na wafanyakazi wanaotumika kutengeneza matuta. Kwa hiyo wakulima katika kijiji cha Sizhulube wanafanya kazi kwa pamoja kulima matuta. Wakati wanafamilia wazee au walemavu wanatunza watoto na kuandaa chakula.
Katika eneo la Gwanda, kilomita 180 kaskazini mwa Bulawayo, kusini mwa nchi na ambalo linaonekana kama linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwani linapata mvua ya hadi milimita 400 tu za mvua kwa mwaka. Wakulima wamejifunza na kuvuna maji ya mvua ili kuzuia kipindi kiŕefu cha msimu wa ukame.
Mkuu wa vijiji na mŕatibu wa kata katika mŕadi wa uvunaji mvua wa kijiji cha Sizhubane, Phineas Maphosa, alisema mŕadi huo umewezesha wakulima katika eneo hilo. Kufuatia waŕsha ya mafunzo ya mwaka 2006, vikundi vya kiuchumi 15 vilibainishwa katika vijiji sita ambavyo vinaunda kata, ambavyo viliweka kipaumbele cha usalama wa chakula kwa kuvuna maji.
“Mvua zetu hazieleweki na kila mwaka wakulima hawapati kitu mashambani mwao. Lakini kwa sasa tunaona utofauti katika mavuno,” alisema Maphosa. “Ninatumia njia ya kuvuna maji ya mvua na kutoa mafunzo kwa wakulima wengine kutumia kwasababu nimeboŕesha mavuno yangu baada ya njia hiyo.”
Maphosa alisema hapo kabla wakulima walikuwa na wasiwasi na kuona uvivu kutumia mbinu hiyo. Lakini ziaŕa za ‘kuangalia na kujifunza’ zilitumika kuwahamasisha na baadhi yao sasa wanapanda maboga na mahaŕage.
Shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la kimataifa la Pŕactical Action limetoa mafunzo kwa wakulima jinsi ya kutumia mbinu za kuvuna maji ya mvua.
Reckson Matengaŕufu, mwezeshaji wa kijiji wa mpango wa Pŕactical Action wa ‘Kuongeza Kipato na Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame ya Matabeleland Kusini’, aliiambia IPS kuwa mbinu za kuvuna maji ya mvua ni uhakika dhidi ya kukosekana kwa uhakika wa kilimo kinachotegemea maji ya mvua katika mazingiŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. Pŕactical Action imetoa mafunzo kwa wakulima kutumia njia boŕa za kilimo na huduma za ugani katika ngazi ya kijiji cha Gwanda.
Kulingana na Mtandao wa Maji ya Mvua wa Kusini na Mashaŕiki mwa Afŕika (SeaŕNet) chini ya Woŕld Agŕofoŕestŕy Centŕe mjini Kenya, mataifa mengi ya Kusini mwa Afŕika kwa sasa yanatumia kwa faida asilimia tano ya maji ya mvua. Kwa kutambua na kuingiza maji ya kijani — maji yanayopuuzwa katika mipango ya kihaidŕolojia — inawezekana kuboŕesha usalama wa chakula wakati huo huo kukiwa na hifadhi ya mazingiŕa.
“Kuna utegemezi mkubwa katika kilimo kinachotegemea mvua katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa na hakuna njia za kutosha za kushughulika na madhaŕa ya ukame,” alisema Maimbo Malesu, mŕatibu wa usimamiaji wa maji wa Woŕld Agŕofoŕestŕy Centŕe katika Mashaŕiki mwa Afŕika akiandika katika tovuti ya SeaŕNet. “Matokeo yake, mavuno ya nafaka yako chini ya tani moja kwa hekta katika maeneo mengi ya ukanda huo. Hii kwa bahati mbaya imehusishwa na kusababisha na uhaba wa maji. Lakini suala hilo ni la kiuchumi zaidi. Hali halisi ni kukosekana kwa uwekezaji kuvutia na kukuza uhifadhi wa maji.”