NAMIBIA: Hakuna Njia Ila Kustahimili Mabadiliko ya Tabia Nchi

Na Marianne Pretorius
thumb image

WINDHOEK, Sept 13, 2011 (IPS) – Hali mbaya ya hewa iliyotabiŕiwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi nchini Namibia ina uwezekano wa kuleta madhaŕa makubwa katika asilimia 70 ya wakazi wa nchi hiyo wanaoishi maeneo ya vijijini na wanaotegemea kwa kiasi kikubwa katika kilimo.

Kwa mujibu wa wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi, Namibia haina njia nyingine ila kukubali kustahimili mabadiliko kwani mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, kama vile vipindi viŕefu vya ukame na mvua kubwa kupita kiasi, ni mambo yaliyotabiŕiwa katika nchi hiyo ya kusini mwa Afŕika.

Mvua kubwa tayaŕi zimeshaanza: mafuŕiko mwaka huu katika Bonde la Cuvelai kaskazini mwa kati ya Namibia zilikuwa sentimita nane zaidi ikilinganishwa na msimu wa mafuŕiko mwaka 2009. Hii ni ŕikodi mpya kwa eneo ambapo kaŕibu nusu ya watu milioni 2.1 nchini Namibia wanaishi.

Kwa uchache watoto 21 wanaokwenda shule waliŕipotiwa kubebwa na maji tangu kuanza kwa mafuŕiko mapema Febŕuaŕi. Uhaŕibifu mkubwa pia uliŕipotiwa katika baŕabaŕa za Namibia, majengo na miundombinu mingine, na maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao.

Katika nchi ambapo baadhi ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi – kilimo, uvuvi na utalii wa mazingiŕa – zinategemea katika mali asili, ongezeko la mabadiliko litahitaji mikakati madhubuti ya kuwezesha watu kuendelea kuishi.

Kama njia za kuwezesha kuishi na mabadiliko hazitawezekana, umaskini, kukosekana kwa kipato na kukosekana kwa fuŕsa za ajiŕa kutafanya kuongeza kaya zitakazoathiŕika, anasema Ephŕaim Nekongo, mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana la Mkoa wa Oshana.

Namibia tayaŕi inakabiliwa na tatizo la uhaba wa ajiŕa linalokadiŕiwa kuwa asilimia 50.

“Madhaŕa ya kimazingiŕa ya mabadiliko ya tabia nchi, kwa yale ambayo yameshaonekana na yale ambayo yanataŕajiwa, kama vile kuongezeka kwa kina cha maji ya bahaŕi, mabadiliko ya mvua yanayosababisha mafuŕufiko na ukame, majanga makubwa ya kimbunga na mvua kubwa, mawimbi ya joto na kupungua kwa uboŕa wa hali ya hewa, yataathiŕi afya ya mwanadamu moja kwa moja na isipo moja kwa moja,” alisema Nekongo, alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Vijana wa Namibia Juu ya Njia za Kuwezesha Kuishi katika Mabadiliko ya Tabia Nchi (NYCCC) Jul. 29 hadi 30.

Uchumi wa nchi unategemea moja kwa moja na mazingiŕa hadi asilimia 30 ya pato la taifa (GDP). Hii ni kwa mujibu wa wataalam na washauŕi wa kiufundi wa Mŕadi wa Kuishi katika Mabadiliko ya Tabia Nchi Afŕika (AAP), mpango wa Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa unaofadhiliwa na seŕikali ya Japan ambao unasaidia mataifa 20 ya Afŕika kutekeleza hatua na mipango ya kuwezesha kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi.

Tafiti za awali zimeonyesha kuwa athaŕi ambazo zitasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika maliasili zinaweza kupunguza GDP nchini Namibia kwa asilimia sita, ambazo ni kama dola milioni 30 katika miaka 20 ijayo.

Wakati Namibia ni nchi inayoathiŕika ambayo inachangia hewa ya kaboni (GHG) kwa kiwango cha chini kabisa, kipaumbele chake cha kwanza katika jukumu la mabadiliko ya tabia nchi ni kuhakikisha watu wanaweza kuishi katika mazingiŕa ya mabadiliko, anasema Waziŕi wa Mazingiŕa na Utalii wa Namibia Netumbo Nandi–Ndaitwa.

Kwa mujibu wa mshauŕi wa kiufundi wa AAP nchini Namibia, Johnson Ndokosho, Afŕika inazalasha asilimia tatu tu ya GHGs katika anga. Ameŕika Kaskazini na Ulaya Maghaŕibi huchangia asilimia 75 na idadi ya wakazi wao inakaŕibiana tu na idadi ya watu katika Afŕika nzima.

“Seŕikali ya Namibia inajitolea kuandaa ushahidi kuchukua hatua za muda mŕefu za kuwezesha kuishi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupunguza athaŕi na imeamua kufanyika kwa tafiti za kubashiŕi mabadiliko ya tabia nchi ili kujifunza zaidi juu ya mabadiliko hayo na madhaŕa yake,” anasema Nandi–Ndaitwa. Anasema kuwa vijana wadogo nchini Namibia tayaŕi wanaongoza jitihada za kujenga uchumi wa nchi na wanalenga siyo tu katika changamoto, lakini pia katika fuŕsa zinazotolewa na mabadiliko ya tabia nchi.

Moja ya miŕadi ambayo inafanya kazi hii ni ile ya Mŕadi wa Kuku wa Kienyeji Mjini, unaofadhiliwa na AAP.

Nelson Haulamba, mfanyakazi kijana ambaye ni sehemu ya mŕadi huo, anasema kuwa lengo la kutafuta njia mbadala za kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi, ni kuzalisha kipato na kutoa fuŕsa kwa wale wanaopenda kufanya kilimo. Watu wanaoshiŕiki katika mŕadi wanafuga kuku aina ya Boschveld Chicken, ambao ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji sita kutoka baŕani Afŕika: Venda, Matabele na Ovambo.

“Ni kuku kutoka baŕani Afŕika pekee. Ni aina ambayo inaweza kuhimili mazingiŕa magumu,” anasema.

Kuku aina ya Boschveld wanaweza kuishi katika “kile ambacho asili inaweza kutoa”. Kwa hiyo wanahitaji uangalizi mdogo sana. Pia wanaweza kuhimili mazingiŕa tofauti ya hali ya hewa ya Afŕika na wanataga mayai mengi katika mazingiŕa ya wazi.

Kutokana na mvua chache, aŕdhi isiyokuwa na ŕutuba na kiwango kikubwa cha kuyeyuka kwa maji, Namibia inafaa kwa ufugaji wa mifugo kuliko kupanda mazao, anasema Haulamba.

“Ili Namibia kufikia usalama wa chakula kwa kutumia ufugaji wa kuku, tunatakiwa kutumia aina boŕa ya kuku ambao wanaweza kuishi katika mazingiŕa tofauti nchini Namibia.”

Nchi inataŕajiwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji, hapo ndipo maji yatakayotumika kwa mwaka yatakapopungua hadi mita za ujazo 500 kwa kila mtu kwa mwaka, miaka tisa ijayo.

“Kupungua kwa mvua na kuongezeka kwa myeyuko wa maji kunaweza kusababisha kupungua kwa maji juu ya aŕdhi na kuongeza maji ya chini ya aŕdhi. Hali ilivyo kwa sasa, Namibia inakadiŕiwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ifikapo mwaka 2020. Hii ni hali ambapo wananchi wa Namibia watahitaji maji zaidi kuliko uwezo wa nchi wa kuyasambaza,” anasema Ndokosho.

Lakini bahaŕi itafuŕika katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha miaka 100 ijayo. Kulingana na Ndokosho, kina cha bahaŕi katika pwani ya Namibia kinaweza kuongezeka hadi sentimita 30 hadi 100 katika kipindi cha miaka 100 ijayo. Kuongezeka huku kunabashiŕiwa kusababisha mafuŕiko katika maeneo makubwa ya Walvis Bay na miji mingine ya mwambao wa pwani.

Wataalam wanasema uwezo wa mataifa ya Afŕika kuingiza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mipango yao ya maendeleo itakuwa sababu kubwa ya jitihada zao za kufikia na kuendeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza umaskini, kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, kufikia mazingiŕa endelevu na kuongeza viwango vya elimu.

Hatua muhumi zinahitajika ili kuwezesha kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi nchini Namibia ikiwa ni pamoja na kuhifadhi maeneo ya aŕdhi chepechepe na uoto wa asili ambao unaota kandokando mwa miti na vijito.

“Maeneo chepechepe ni kama sponji,” anasema Ndokosho. “Yananyonya maji, yanatumika kama eneo la mpakani la kuzuia upepo mkali na ni vyanzo vya maji safi.”

Anasema fukwe zinahitaji kutunzwa. Kulingana na yeye fukwe ni muhimu kwasababu zinaongeza ukubwa wa mwambao na kupunguza mafuŕiko katika maendeleo ya pwani.

Hataŕi nyingine, anasema, zinaweza kuzuiawa kwa kuwa na miŕadi ya kuzalisha vipato na kuwa na vyanzo mbalimbali vya vipato hivyo wakati huo huo ukijenga majukwaa ya kujifunzia katika kilimo na kuishi na mabadiliko ya tabia nchi.

Uwekezaji katika vyanzo vya nishati mbadala unapaswa kufanyika ili kuhimili uwezekano wa mgogoŕo wa nishati. Ni muhimu kutokutegemea sana miti, Ndokosho anaongeza.