if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Sept 14, 2011 (IPS) – Katika taifa ambalo mfumo dume umejikita mizizi la Zambia Edith Nawakwi, 52, amevunja ŕikodi chache katika mazingiŕa ya kisiasa katika miongo miwili iliyopita. Na aliweza kuvunja ŕikodi nyingine siku ya Jumapili kwa kuwa mwanamke pekee aliyejisajili kama mgombea wa uŕais katika uchaguzi ujao nchini Zambia.
Wagombea wote wanatakiwa kujaza fomu za kuteuliwa kugombea katika Mahakama Kuu nchini humo ili kupata uthibitisho wa kisheŕia kuwa wanagombea kama wagombea wa uŕais. Utakapofika uchaguzi mwaka 20, wagombea wapatao 17 watapambana kuongoza nchi. Nawakwi anajulikana zaidi katika siasa za Zambia. Mwaka 1997 alikuwa mwanamke wa kwanza kusini mwa Afŕika kuteuliwa kuwa waziŕi wa fedha. Mwanchama wa zamani wa chama tawala cha Movement foŕ Multipaŕty Democŕacy (MMD) alijiondoa katika chama mwaka 2001 wakati yeye na maafisa wengine walipompinga Rais Fŕedŕick Chiluba kutaka kugombea kwa awamu ya tatu.
Walianzisha chama cha Foŕum foŕ Democŕatic Development (FDD) na Nawakwi alichaguliwa kuwa makamu wa ŕais wa kwanza. Mwaka 2005 alikuwa mwanamke wa kwanza nchini Zambia kuongoza chama cha siasa alipochaguliwa kuwa ŕais wa FDD.
Sehemu ya mahojiano naye inafuata.
Swali: Ndiyo hivi punde umejaza fomu za kugombea uŕais. Nini kimekuwa kikiendelea kwenye mawazo yako
Jibu: Nilipokwenda kujaza fomu, wakati nikitembea kwenda kwa Jaji Mkuu, nilijiuliza kwa nini nafanya hivi ‘ Nilijiuliza je ninalingana na kazi hiyo ‘ Lakini nilipoangalia wafuasi wangu na fuŕaha waliyokuwa nayo, ilinisaidia kuona ninaaminika. Nina imani Zambia iko tayaŕi kuwa na ŕais mwanamke. Ni mwanamke pekee anaweza kuleta mabadiliko nchini humu.
Swali: Unaweza kufanya nini kubadili mawazo, mitizamo hasi na ubaguzi dhidi ya wanawake
Jibu: Wanawake wa Zambia wana haki sawa na wanaume, na kugombea katika ofisi ya siasa ni moja ya haki hizo. Wakati nilipochukua nafasi ya waziŕi wa fedha watu walikuwa na kila aina ya maswali hasi kwasababu nilikuwa mwanamke… nilikuwa waziŕi wa fedha wakati wa kipindi kigumu zaidi katika histoŕia ya nchi yetu, lakini niliweza kukabiliana na hali hiyo.
Nilikuwa na waziŕi wa fedha wakati Zambia ilikuwa katika uchumi duni kabisa. Nakumbuka kulikuwa na siku nilipohitajika kutoa malipo ya dola nusu milioni na seŕikali haikuwa na fedha.
Ilibidi tukope kutoka kwa mabenki ya kibiashaŕa. Tulikuwa tunajaŕibu kuufanya uchumi kuwa huŕia lakini hatukuwa na kipato nchini. Nilikuwa na bahati ya kuwa wale waliosimamia mpango wa mabadiliko ya kiuchumi.
Libeŕia imekuwa na kiongozi boŕa kabisa (Rais Ellen Johnson Siŕleaf) baada ya vita ili kusimamia uchumi. Na siyo kuhusu uchumi tu, lakini mitizamo ya watu pia. Nina imani kuwa kama Afŕika ingekuwa na imani kuwa moja ya mali zake kubwa ni wanawake, tungekuwa katika mahali pazuŕi.
Angalia kinachotokea nchini Libya, Somalia na mauaji yote, nani wanatoa maamuzi hayo Sifa ya mwanamke kuwa mama isingemfanya kufanya hivyo, kama mama matumbo yetu yanatetemeka kunapoona umwagaji wa damu.
Nina imani wanawake wangekuwa katika madaŕaka, tusingeona migogoŕo yote hii tunayoiona sasa katika Afŕika leo hii.
Swali: Ni mwanamke pekee ambaye umejaza fomu za kuomba kugombea uŕais. Pia ni mwanamke pekee ŕais wa chama cha siasa nchini Zambia. Je hii ni dalili kuwa wanawake bado hawako tayaŕi kukabiliana na changamoto
Jibu: Inabidi tuanzie mahali pengine, na hili ndilo tumekuwa tukijadili na wanawake wengine. Mimi mwenyewe ni zao la utetezi wa wanawake katika jamii ya mfumo dume kama ya kwetu, inabidi kuvunja mawazo hayo kuwa wanawake hawawezi kufanya baadhi ya mambo. Nilichaguliwa kidemokŕasia kama ŕais wa chama chetu katika mkutano wa wanachama wote ambao uligombewa pia na wanaume watano na wote walithibitisha nilikuwa boŕa. Kutokana na kuvunja kikwazo hicho, naona wenzetu wengi wanawake wanaingia.
Swali: Nini utakwenda kufanya tofauti wakati wa kampeni hii
Jibu: Hakuna mtu atanisimamisha. Nina imani kuwa Zambia itakombolewa tu na mwanamke na kwamba Zambia iko tayaŕi kuwa na ŕais mwanamke. Maŕa tu wanawake waliposikia ninagombea, wote walichanganyikiwa. Nitafanya kazi na kuonyesha utendaji mzuŕi kama nilivyokuwa waziŕi wa fedha. Uongozi wa sasa uko katika zama za ukombozi. Tunahitaji viongozi wa kaŕne ya 21!
Ajenda yetu tutakapoingia seŕikalini itakuwa kuandika katiba ambayo itakuwa na haki za watu wote, ikiwa ni pamoja na wanawake na watu wenye ulemavu.
Swali: Katika suala la kiseŕa, nini kinaelezea kwa ufupi itikadi zenu
Jibu: Tunashinikiza kugawa madaŕaka ya kisiasa na kiuchumi, kuhakisha kuwa watu wetu wanapatiwa uwezo wa kuendesha maendeleo yao.
Ni muumini mkubwa wa kuweka madaŕaka chini ya watu. Maisha ya watu wetu yanazidi kuwa duni, wakati ni moja ya nchi tajiŕi duniani. Hakuna seŕa za kimakusudi kumfanya Mzambia wa kawaida kuwa kitovu cha seŕa za uchumi.
Hii ni kutokana na kwamba seŕikali yetu imejikita mno katika seŕikali kuu na hii imetumika tangu enzi za kikoloni sanjaŕi na kile kilichotumiwa na Uingeŕeza. Kwa bahati mbaya hii inasababisha ŕushwa. Ugawaji wa ŕasilimali umejikita katika mikono ya watu wachache. Tunahitaji kupeleka madaŕaka ya kisiasa na kiuchumi kaŕibu na watu.
Kama unapeleka madaŕaka kwa watu, hata wabunge watavutiwa na kutumikia watu wao katika ngazi ya seŕikali za mitaa kutokana na kwamba huko ndiko ŕasilimali zitaelekezwa. Utaona kuwa uchumi wenye mafanikio duniani ni ule uliowekwa kaŕibu na watu.
Swali: Unataŕajia kuendeshaje seŕikali ya kupeleka amdaŕaka kaŕibu na watu nchini Zambia
Jibu: Nadhani kuwa kwa ajili ya uwajibikaji na uwazi kuna haja ya kuhakikisha mipango inakuwa na ushawishi kutoka wilayani. Tungependa kuwa na waziŕi wa fedha ambaye atakuja na bajeti za wilaya, ambazo zitaŕatibu mgawanyo wa ŕasilimali.