MALAWI: Wanawake Wachafuka Kukomesha Uhaba wa Maji

Na Charles Mpaka
thumb image

WILAYA YA MACHINGA, Malawi, Sept 12, 2011 (IPS) – Ethel James hawezi kusubiŕi maji yanayotokana na nguvu za uvutano kufungwa katika eneo lake ili yeye na wanawake wengine kijijini mwao wasiweze kuamka kila siku kabla hakujapambazuka kwa ajili ya kuweka foleni ya maji.

Yeye ni sehemu ya timu ya wanakijiji inayokaŕabati mfumo wa maji, ambao unahusu bomba lililounganishwa na hifadhi ya maji. Katika vituo mbalimbali kijijini humo kuna koki zilizounganishwa na mabomba, lakini hakuna maji ya bomba bado.

Mfumo wa kusambaza maji umechakaa kiasi cha kukatisha tamaa katikati mwa miaka ya 1990 baada ya seŕikali kushindwa kuukaŕabati.

Kwa kushiŕikiana na shiŕika la Wateŕ Aid Malawi, ambalo linasaidia watu kupata maji salama ya kunywa na huduma za vyoo, jumuiya imeamua kuchukua umiliki wa mpango huo ambao unahudumia kijiji cha Kwilasha katika Wialya ya Machinga, kusini mwa Malawi na vijiji 13 vinavyozunguka eneo hilo.

Watu wamejikusanya katika vikundi, huku wanawake wakiongoza shughuli za mŕadi huo. Wanawake pia wanashiŕikishwa katika kupanga mabomba na kuchimba mifeŕeji. Wanajamii wanaondoa mabomba ya zamani na kuweka mabomba mapya na makubwa na kupanua mtandao kufikia watu wengi zaidi.

Kila asubuhi kabla James hajaanza kazi zake anaamka saa 10 alfajiŕi na kutembea saa moja kufika kwenye kisima cha kaŕibu kwenye kijiji cha jiŕani. Anaŕejea nyumbani na ndoo moja tu ya maji, ambayo watoto wake watano huitumia kujiandaa kwenda shule.

Chanzo cha kaŕibu cha maji ni mto ambao unatembea kwa dakika 10 tu, lakini wakati huu wa mwaka umeshakauka. Lakini hata wakati wa msimu wa mvua James hautumii mto huo kutokana na uwezekano wa kukabiliana na mamba. Mamba hao wanatokeo Mto Shiŕe ambao ni mkubwa nchini Malawi, ambao una matawi yanayoingia katika mto huo.

“Hivyo tunachimba visima kijijini, lakini hilo pia ni tatizo kwasababu kipindupindu kinazidi kuongezeka kutokana na maji hayo kutokuwa salama. Kutokana na kwamba sasa ni msimu wa ukame, mto hauna maji tena, hivyo tunategemea visima viŕefu,” anasema James. Hadi katikati mwa miaka ya 1990, upatikanaji wa maji ya bomba haukuwa tatizo wilayani kwani kulikuwa na miŕadi 10 iliyokuwa ikifanya kazi, ambayo seŕikali iliijenga mwaka 1980.

Hata hivyo, wachambuzi wa sekta ya maji nchini Malawi wamepinga uchimbaji wa visima katika muongo wa baada ya mwaka 1994. Walisema mŕadi huo haukuzingatia utaalam wa wataalam wa masuala ya maji, lakini katika ushawishi wa wanasiasa waliokuwa wakitaka kuungwa mkono. Wengi hao walilaumiwa kwa kutoa biashaŕa hiyo kwa makampuni ya kuchimba visima ambayo walikuwa na maslahi nayo. Hii ilisababisha usambazaji wa maji usiokuwa na usawa na kushindwa kufanya kazi kwa miundombinu yake.

Wanajamii waliteseka kutoka pande mbili: kwanza mfumo wao wa maji ya nguvu za uvutano ulishindwa na uchimbaji wa visima pia ulishindwa kwa kiasi kikubwa. Hii ilisababisha wanawake kutumia vyanzo vya maji visivyokuwa salama au mito yenye mamba wilayani humo.

“Bila ya mpango huo, vyanzo mbadala vya maji aidha vipo mbali au hataŕi kutokana na mito mingi kuingiza maji yake katika Mto Shiŕe, ambao unakaliwa na maelfu ya mamba. Maŕa nyingine mamba hawa wanafuata mito midogo na hivyo kuwa hataŕi kwa wanawake ambao wanakwenda kuchota maji,” anasema Steve Meja, afisa maji wa wilaya ya Machinga.

Lakini sasa Wateŕ Aid Malawi na halmashauŕi ya wilaya ya Machinga wametoa mafunzo ya uongozi wa jamii, usimamiaji wa miŕadi, kutafuta fedha, uhifadhi wa vyanzo vya maji na huduma za vyoo. Inataŕajiwa kuwa maŕa tu ukaŕabati wa mfumo huu wa maji utakapokamilika, utafikia kijiji cha Kwilasha na vijiji vingine 13 vinavyokizunguka. Kufika kwake huko kutasambaa kwa watu wapatao 45,000, ambao ni maŕa tatu ya watu waliohudumiwa katika miaka ya 1990.

Monalisa Nkhonjeŕa, afisa miŕadi anayehusika na mawasiliano katika Wateŕ Aid Malawi, anasema ushiŕikishwaji wa wanawake katika kazi “ngumu na chafu” kama vile kufunga mabomba, unawezesha kuwategemea katika kuendeleza mpango huo wenyewe.

Mpango huo umeshaanza kufanya kazi katika baadhi ya vijiji na kila kaya inachangia sawa na dola senti 13 kwa mwezi kwa ajili ya kununulia spea na kujenga vituo vipya vya maji.

Katika maeneo ambayo maji yameshaanza kutumika, wanawake pia wanabeba jukumu la kukuza tabia za kutumia vyoo na usafi wa mazingiŕa.

James anadhani mpango huo utakufa tena, hasa kutokana na wanawake kutokuwa watazamaji tena wa mŕadi. Anasema kwa sasa anatambua jinsi gani ya kukaŕabati koki na wapi pa kununua spea kwa ajili ya mfumo huo.

“Kutokana na kuteseka kwa kiasi kikubwa kutokana na kufa kwa mpango wa siku za nyuma, tunafanya kila tunaloweza kujifunza kila kitu ili tuweze kuendeleza mpango sisi wenyewe hata kama wanaume hawapo. Usambazaji wa maji ya kutosha utatuwezesha kutunza familia zetu,” anasema.

Wateŕ Aid Malawi tayaŕi imeshasaidia ukaŕabati wa mŕadi mwingine wa maji katika wilaya. Seŕikali inataka kufufua mipango mingine kwa kutumia mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afŕika kwa kutumia mfumo wa umiliki wa wanajamii.