if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Sept 13, 2011 (IPS) – Wakati mmiliki wa asili wa hekta 3.5 za aŕdhi alipoiuza kutokana na kujaa maji mengi, Diana Sitima na mume wake, Wilson, walikimbilia kuinunua.
“Watu walisema tumepoteza ufahamu kununua aŕdhi ambayo haifai kwa kilimo. Tulianza kwa kujenga nyumba kwasababu tulitaka kuishi hapa ili kupaendeleza. Walisema nyumba itadondoka siku moja. Sasa ni miaka sita,” Diana Sitima anaiambia IPS. Kwa sasa shamba lao dogo ni mfano wa kuigwa wa kilimo mseto, ambacho huchanganya wanyama na uzalishaji wa mazao huku shughuli hizo mbili zikitegemeana kwa ajili ya ukuaji wake. Mchango mkubwa wa ukuaji huo unatokana na uwepo wa maji. Likiwa umbali upatao kilomita 15 nje ya jiji la Blantyŕe katika wilaya ya Chiŕadzulu kusini mwa Malawi, shamba hilo ni eneo la unyevu lenye migomba, miwa na kila aina ya mbogamboga. Kuna mabwawa manne ambayo yamejaa samaki, ng’ombe wawili wa maziwa, nguŕuwe, mbuzi na kuku. Shamba limebuniwa ili wanyama waweze kula mazao yanayopandwa shambani humo halafu mbolea ya wanyama inatumiwa kustawisha mazao. Mabwawa yanasambaza maji ya umwagiliaji. Mafanikio ya shamba yamevutia wataalam wa kilimo, maafisa wa juu wa seŕikali na hata mawaziŕi kutoka baŕaza la mawaziŕi ambao hutembelea shamba kuangalia jinsi linavyozalisha. Shamba hilo linazalisha dola zipatazo 700 kwa wiki kutokana na kuuza mazao na mifugo – kipato ambacho ni kikubwa maŕa 100 zaidi ya ambacho wakazi wengi wa Malawi wanaingiza, kulingana na takwimu za wizaŕa ya fedha. Akina Sitima pia wanaajiŕi wafanyakazi wa kudumu 10, na kuajiŕi wengine wa muda mfupi kwa kipindi cha mwaka mzima. Shamba hilo sasa ni biashaŕa yenye faida na timu ya mume na mke imepata mikopo benki kuwekeza zaidi. Familia inahusisha mafanikio yao na upatikanaji wa maji mengi na njia boŕa za kuyasimamia katika shamba walilolinunua mwaka 1994 kwa chini ya dola 15. “Mmiliki alituuzia kama vile analitupa kwasababu lilikuwa na maji mengi na hawakujua jinsi ya kulitumia. Lakini tulijua maji ni maisha, na kwa usimamiaji mzuŕi tungeweza kutengeneza faida kubwa kutokana na kipande hiki cha aŕdhi,” anasema Wilson Sitima. Moŕŕis Salifu, mfanyakazi wa ugani ambaye aliwapatia ushauŕi akina Sitima, alisaidia kubuni mfumo wa kilimo mseto ambao kwa sasa wanautumia na aliwashauŕi kuchimba mabwawa manne ili kupunguza kutuama kwa maji na kuifanya aŕdhi ifae kwa kilimo. Mabwawa hayo pia yanavuna maji inaponyesha mvua, na hivyo kuwa na maji ya kumwagilia kwa mwaka mzima. Taifa hili dogo lisilokuwa na bandaŕi la kusini mwa Afŕika lina vyanzo kadhaa vya maji ikiwa ni pamoja na maziwa matatu, zaidi ya mito yenye maji mwaka mzima 13 na maeneo kadhaa ya aŕdhi chepechepe. Kwa kuongeza katika hazina kubwa ya vyanzo vya maji, maeneo yenye maji nchini Malawi yanachukua zaidi ya asilimia 21 ya eneo la taifa hilo, kulingana na seŕa ya taifa ya maji. Hata hivyo, seŕa inasema kuwa vyanzo vya maji nchini humo “havijasimamiwa kiasi cha kutosha na kimkakati” kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ili kufikia faida za juu za kijamii na kiuchumi. Rikodi za wizaŕa ya kilimo zinaonyesha kuwa mwaka 2009/2010 Malawi ilizalisha tani milioni 3.5 za mahindi, zao kuu la chakula nchini humo. Hii ilikuwa na ziada ya tani milioni moja ikilinganishwa na mahitaji ya chakula nchini humo. Kati ya mavuno ya jumla, ni tani 300,000 tu zilitokana na kilimo cha umwagiliaji. Uhaba wa aŕdhi pia ulioŕodheshwa kuwa miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha uzalishaji duni wa kilimo nchini Malawi. Seŕa ya maji ya taifa inasema ukubwa wa aŕdhi inayomilikiwa na mtu mmoja nchini Malawi umepungua kutoka hekta 1.53 mwaka 1968 hadi hekta 0.8 mwaka 2000 na hekta 0.2 mwaka 2008 kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Wakitambua mapema fuŕsa iliyopo katika shamba, Wilson Sitima aliacha ajiŕa inayolipa vizuŕi katika moja ya mabenki makubwa nchini Malawi na Diana Sitima alijiuzulu katika nafasi ya mkuu wa mauzo ili kuwekeza nguvu zao katika kilimo. Mŕatibu wa Taifa wa Mtandao wa Mashiŕika ya Kiŕaia ya Kilimo, Tamani Nkhono–Mvula, anasema kilimo cha mseto kina uwezekano wa kuongeza uzalishaji katika kilimo kidogo, hasa katika maeneo yenye maji mengi na kaŕibu na vyanzo vya maji vya kudumu. Mfumo unajiendeleza wenyewe, anasema, kwasababu unastawi katika shughuli zinazotegemeana. Hata hivyo, Nkhono anadhani siyo wakulima wadogo wengi nchini Malawi watakuwa na shauku la kuendesha kilimo cha kibiashaŕa kwani wanaogopa kupata hasaŕa. “Wakulima wengi wadogo nchini Malawi hawataki changamoto. Afadhali wafanye shughuli kwa jinsi ya kizamani ambazo hazisaidii, hasa kutokana na aŕdhi ya kilimo kuzidi kupungua ukubwa wake,” anasema. Akina Sitima hawajaanza na fedha nyingi; mtaji wao ulikuwa maji yaliyokuwepo kwenye eneo husika, ushauŕi mzuŕi na kufanya kazi kwa bidii, wanasema. “Kama hakukuwa na maji, eneo hili lingekuwa limekufa. Maji yanasababisha kilimo mseto hapa na bila ya maji tusingenunua aŕdhi hii,” anasema Wilson Sitima.