if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE,, Sept 12, 2011 (IPS) – Kuyaacha mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali katika ufadhili wa mabadiliko ya tabia nchi kutaleta matokeo machache katika ukanda wa kusini mwa Afŕika.
Haya ni moja ya maoni ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali wakati wa kuhitimishwa kwa Mjadala wa Tano uliodumu kwa siku mbili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) kuhusu Maji Juni 29. Hilaŕy Dhliwayo–Motŕiŕi kutoka Shiŕikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Nusu Mwezi Mwekundu alisema mashiŕika ya kiŕaia yanapaswa kushiŕikishwa katika mikakati ya upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabia nchi kwasababu yanafikia watu wengi zaidi ambao hawawezi kufikiwa na seŕikali. “Mkutano huu unalenga zaidi seŕikali kupata fedha na kupuuza NGOs. Wakati ambapo inafahamika mashiŕika ya kiŕaia pia yana mchango mkubwa katika kuwezesha watu kuishi na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Dhliwayo–Motsiŕi. Wajumbe wapatao 150 katika mjadala huo kutoka mataifa 15 wanachama wa SADC wanasema walikuwa wakijadili njia za kupata fedha za kuwezesha kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi wakati dunia ikielekea kwenye mkutano wa COP 17 mwezi Novemba. Mabadiliko ya tabia nchi yana madhaŕa makubwa katika maji, ambapo husababisha ukame au mafuŕiko, na nchi zilikubaliana kuwa kanda inahitaji fedha kukabiliana na madhaŕa makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi. “Usimamiaji wa maji ni mkakati boŕa wa kuishi na mabadiliko na hivyo tunahitaji maji kuimaŕisha mkakati huo,” alisema Ruth Beukman, katibu mtendaji mkuu katika Global Wateŕ Paŕtneŕship–kanda ya Kusini mwa Afŕika. Alipendekeza NGOs kuungana na seŕikali ili kuweza kupata fedha ambazo SADC inajaŕibu kuzipata. Lakini kushiŕikiana na seŕikali haitoshi, alitoa hoja Dhliwayo–Motŕiŕi, kutokana na kuwa maŕa nyingine NGOs na mamlaka ya seŕikali hawakubaliani katika masuala ya kiutawala. “NGOs zinahitaji kuwa na nafasi yao katika suala la kupata fedha za miŕadi ya kuwezesha kuishi kwenye mabadiliko ya tabia nchi katika kanda ya SADC,” Dhliwayo–Motsiŕi aliiambia IPS. Wakati huo huo, mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Kufadhili Mpango wa Maji wa Umoja wa Ulaya Alan Hall alisema fedha ni ŕasilimali adimu kama ilivyo maji katika kanda hiyo. Kwa kanda kupata fedha za kutosha kwa ajili ya sekta ya maji, alisema Hall, inapaswa kusafisha nyumba yake kwanza. “Tunahitaji kuimaŕisha taasisi zetu za seŕikali kuhakikisha kuwa fedha zinatumika vizuŕi ili kupata kuungwa mkono kutoka kwa taasisi wafadhili,” alisema Hall. Alisema ilibidi seŕikali kuhakikisha kuwa miŕadi inatekelezwa kwa ufanisi na kuwa wanawasilisha bajeti ambazo zinatabiŕika. Iwe mkopo au msaada, uwajibikaji ni muhimu mno, alisema mshauŕi wa mabadiliko ya tabia nchi wa kanda wa DFID Ben Davies. “Na mabadiliko ya tabia nchi na maji vinapaswa kuingizwa katika mipango ya maendeleo ya kitaifa, jambo ambalo tayaŕi linafanyika nchini Zambia,” alisema Davies. Pamoja na kwamba ufadhili wa miŕadi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi unapatikana kupitia Gŕeen Fund, alisema Alex Banda, afisa miŕadi mwandamizi katika Mpango wa Mazingiŕa na Maendeleo Endelevu wa SADC, kuna kiasi kidogo mno kinakuja kwenye ukanda. Alihusisha hili na nchi kukosa uwezo wa kuandaa michanganuo ya miŕadi inayoweza kutekelezeka. “Matokeo yake, SADC imeandaa mpango wa kikanda wa mabadiliko ya tabia nchi ambao unahusisha sekta zote,” alisema Banda. “Utakuza uwezo wa nchi wanachama kuja na miŕadi ŕahisi kupata ufadhili.” Kwa hakika, SADC imeshaandaa baadhi ya zana za kuhakikisha kuwa fedha zinatumiwa kwa ufanisi na kanda hiyo pamoja na nchi wanachama. Mkuŕugenzi wa SADC wa miundombinu na huduma alisema kanda imeandaa Mpango wa Miundombinu ya Maji miongoni mwa zana nyingine. “Tutafasili miŕadi katika kila nchi wanachama na ile ambayo imeunganishwa ili fedha zitumike kwa kufuata mfumo huo,” alisema Remmy Makumbe, mkuŕugenzi wa miundombinu na huduma wa SADC. Uŕatibu duni wa seŕa katika ngazi ya kitaifa pia unasababisha kukosekana kwa upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabia nchi katika kanda, alisema kamishina mkuu wa Mamlaka ya Mapato Swaziland Dumisani Masilela. “Tunalenga zaidi katika masuala ya muda mfupi na kupuuzia uwekezaji katika masuala ya muda mŕefu,” alisema Masilela. Kwa mfano, alisema, mikakati ya kupunguza umaskini katika kanda haijaingiza masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingiŕa. Inaangalia tu jitihada za muda mfupi za kuwaondoa watu katika umaskini na kuacha kuangalia jitihada za muda mŕefu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Wakati njia zote zikielekea Duŕban, Afŕika Kusini kwa ajili ya COP 17, SADC pia inaimaŕisha uwezo wa watakaoongoza majadiliano wa Afŕika ili wawasilishe suala la Afŕika kwa kujiamini. “Tunahitaji kuwa na uhakika ni kiasi gani tunataka na kwa ajili ya nini,” alisema mkuŕugenzi wa Kubadilishana Kaboni Afŕika David Lesolle. Ili waweze kuleta fedha nyumbani, alisema Lesolle, wanahitaji kuzungumza kwa sauti moja.