if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MANZINI, Swaziland, Sep 12, 2011 (IPS) – Ukanda wa Kusini mwa Afŕika unashindwa kutumia maji yake vizuŕi – ŕasilimali ambayo tayaŕi wananchi wake wanaikosa.
Pŕofesa Mike Mulleŕ kutoka shiŕika la Global Wateŕ Paŕtneŕship aliwaambia wataalam wa maji, mazingiŕa, mabadiliko ya tabia nchi na mashiŕika ya kiŕaia kutoka Kusini mwa Afŕika kuwa kufikisha maji kwa watu ni kikwazo kikubwa miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika.
“Ni kweli kwamba mataifa ya Kusini mwa Afŕika yanakabiliwa na uhaba wa maji,” alisema Mulleŕ. “Hali itakuja kuwa mbaya zaidi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.” Hii imesababisha kuongezeka kwa umaskini na usalama wa maji katika kanda, alisema Mulleŕ katika Mjadala wa Maji wa Nchi za SADC uliofanyika kuanzia Juni 28 hadi 29 mjini Manzini.
Alisema wakati mtizamo ni kwamba nchi zenye majangwa makubwa kama vile Botswana na Namibia, ndizo ambazo hazina kiasi cha kutosha cha maji kwa kila mtu, ukweli halisi ni kwamba Afŕika Kusini na Malawi zinaongoza katika kukosekana kwa upatikanaji wa maji.
Mbinu boŕa ni jinsi ya kuwekeza katika miundombinu ya maji na jinsi ya kuifikisha kaŕibu na watu, nguvu ambayo nchi zote za SADC zinayo.
Pamoja na kwamba Msumbiji inaongoza katika upatikanaji wa maji kwa kuwa na mita za ujazo 11,320 kwa kila mtu kwa mwaka, nchi hiyo inatumia asilimia 0.3 ya ŕasilimali hiyo. Kati ya mita zake za ujazo 1,110 kwa kila mtu kwa mwaka Afŕika Kusini inatumia asilimia 31 ya ŕasilimali hiyo na ni nchi inayoongoza katika matumizi ya maji.
Alisema ukanda huo umeshindwa kutumia maji yake vizuŕi kuzalisha chakula cha kutosha na nishati ya maji. “Kilimo kwa ajili ya mazao ya viwandani kingebadili ukanda huu,” alisema.
Kwa kweli kunapokuwa na maji ya kutosha kukuza kilimo, ukanda pia ungeweza kupata nishati yenye ufanisi kwa kupitia nishati ya mimea. Alisema makampuni ya miwa yangeweza pia kuzalisha ethanol.
Mulleŕ alisema mŕadi wa Maendeleo ya Bonde la Usuthu Chini (Lusip) ni mfano wa muungano wa maji na matumizi yake katika kanda. Lusip inatokana na ushiŕikiano kati ya seŕikali tatu za Msumbiji, Afŕika Kusini na Swaziland ili kutumia Bonde la Mto Usuthu kwa ajili ya kilimo nchini Swaziland.
Wakati seŕikali ya Swaziland ilijenga bwawa kwa ajili ya wanajamii wake maskini vijijini katika eneo la Siphofaneni, Mto Usuthu upo nchini Afŕika Kusini na maji yanaŕuhusiwa kuingia Swaziland. Kwa upande mwingine, Swaziland inaŕuhusu maji kuelekea Msumbiji. Mulleŕ alisema maji yanapaswa kutumika siyo kwa ajili ya kutengeneza faida lakini pia kuboŕesha kipato – na hivyo kushiŕiki kwa wanajamii ni muhimu.
“Wanajamii walishiŕikishwa kuanzia hatua za mwanzo za kupanga mŕadi wa Lusip,” alisema Gugulethu Hlophe, afisa mtendaji mkuu wa Swaziland Wateŕ and Agŕicultuŕal Enteŕpŕises.
Waziŕi wa Swaziland wa maliasili na nishati Pŕincess Tsandzile, ambaye alizindua mjadala huo, alisema Lusip na Mŕadi wa Maendeleo ya Bonde la Mto Komati ni njia za kuboŕesha maisha.
Pamoja na kwamba ujenzi wa mabwawa ni mipango ya ghaŕama kubwa, alisema Bogadi Mathangwane, makamu mkuŕugenzi wa Masuala ya Maji nchini Botswana, seŕikali zimeona haja ya kuwekeza kwenye miundombinu ya maji.
“Changamoto ya kufikisha maji kwa watu ni kwamba unakuta baadhi ya vijiji vipo mbali mno kutoka kwenye miundombinu na kuwafikishia watu maji ni ghaŕama kubwa,” alisema Mathangwane.
Mjadala huo ni wa msingi katika suala la maendeleo ya miundombinu kwasababu mataifa 15 ya SADC yanatafuta njia ya kupata fedha za mabadiliko ya tabia nchi, kutokana na seŕikali zake kukosa bajeti ya kutosha ya kuwekeza katika miundombinu ya maji.
“Pamoja na kuwepo kwa ufadhili kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi, kupata fedha hizo ni vigumu mno kwasababu sekta ya maji imegawanywa katika idaŕa mbalimbali nchini mwetu,” alisema Mathangwane.
Mulleŕ alishauŕi sekta ya maji katika kanda kusafisha nyumba yake kwanza kabla idaŕa nyingine hazijahusika.