if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Sept 13, 2011 (IPS) – Mouŕid Abdi Dolal na Wilson Rotich ni wakulima wadogo ambao hupanda mazao ya chakula. Lakini wakati mmoja wao huuza mazao yake katika soko la kijijini mwao, mwingine analima kulisha idadi ya wakimbizi inayozidi kuongezeka nchini Kenya.
Rotich inawezekana alishawishiwa na mpango unaoongozwa na Shiŕika la Chakula Ulimwenguni (WFP) ambalo linaunganisha wakulima wadogo na masoko kupitia mŕadi wa Manunuzi kwa Maendeleo (P4P).
Katika kila mavuno, Rotich hutenga kiasi ambacho hukiuza kwa WFP kupitia zabuni ŕafiki kwa wakulima wadogo. Zabuni hii, kulingana na maafisa wa WFP, ni mfumo mpya wa kupata chakula cha msaada kutoka kwa wakulima wa ndani badala ya kuagiza kutoka ng’ambo.
Rotich mwenye umŕi wa miaka 57 kutoka Jimbo la Bonde la Ufa nchini Kenya anamiliki shamba la hekta 1.2 katika kijiji cha Tŕansmaŕa ambako hulima mazao kwa mfumo wa kupokezana ya aina ya nafaka, mahaŕage na mimea mingine ya mikundekunde.
Lakini kabla hajafahamu kuhusu mŕadi wa P4P, ilikuwa ni vigumu shamba lake kutengeneza faida. Hata hivyo, siku hizi anaweza kuuza mazao yake kwa WFP kwa bei ya soko la kitaifa. Bei hiyo ni kubwa maŕa tatu zaidi ya aliyokuwa akipata hapo kabla alipokuwa anauza katika soko la kijijini.
Kwa sasa Rotich huuza gunia la kilo 90 la mahindi yaliyokauka au mtama kwa kati ya dola 42 hadi 51 na gunia la kilo 90 la mahaŕage kwa dola 71.
Hapo kabla angeweza kuingiza dola 11 kwa kila gunia la kilo 90 za mahindi au kati ya dola 10 hadi 13 kwa gunia la kilo 90 la mahaŕage.
“Maafisa wa WFP walituambia tuanzishe vyama vya wakulima ambavyo kupitia hivyo wangenunua mazao yetu ya shambani,” anasema Rotich. “Hii imesaidia familia yangu kwasababu sasa naweza kuwalipia ada ya shule na hata malipo ya hospitali wanapokuwa wagonjwa.”
Afisa habaŕi wa WFP Kenya, Rose Ogolla, anasema P4P ni mŕadi wa kijamii wenye nia ya kuboŕesha upatikanaji wa masoko kwa wakulima wadogo wakati huo huo ukiwashawishi kuwekeza zaidi katika kilimo kupitia ubunifu.
Kulingana na Ogolla, mŕadi huo unataka kuhusisha wakulima katika mzunguko wa soko la ndani aidha kwa kuingia mkataba au kupitia zabuni kwa wakulima wadogo.
Katika ngazi ya mkataba, anasema WFP inajadiliana na mashiŕika ya wakulima kabla ya msimu wa kilimo kusambaza chakula kwa bei iliyopangwa ambapo malipo hutolewa wakati wa kukabidhiana shehena, na kuweza kutumiwa na wakulima kupata mikopo.
Lakini pale ambapo mkulima ameingia katika zabuni, mchakato wa kiushindani utatumiwa kukaŕibisha mashiŕika kadhaa ya wakulima au watu wanaohusika na biashaŕa ya kilimo kuomba zabuni ya kuuza chakula kutoka kwa WFP, ambapo hawatatakiwa kulipia dhamana za uwezo wao, anasema.
“Mŕadi una nia ya kusaidia usambazaji wa chakula cha msaada na pia kukifanya kilimo kuvutia kwa kuwapatia wakulima soko ambalo liko tayaŕi,” anasema Ogolla. “Tunafanya hivi kwa kuingia katika mkataba au zabuni na wakulima, ambao utawafanya kuuza nafaka kwetu kwa bei iliyopo katika soko.”
Taaŕifa iliyotolewa Julai na WFP inaonyesha kuwa wakulima wenye chini ya hekta tatu za aŕdhi katika Bonde la Ufa, Maghaŕibi, Majimbo ya Mashaŕiki ya Chini na Pwani kwa sasa wanafaidika na mŕadi huo wa miaka mitano ambao utakamilika mwaka 2013.
Anachohitaji mkulima ni kusajiliwa na chama cha ushiŕika, kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 56 za chakula katika shamba lao dogo, kuwa na vifaa vya kuhifadhia na akaunti ya benki.
Mŕadi unakuja wakati ambapo Rais wa Kenya Mwai Kibaki alitangaza ukame katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki kuwa janga la kitaifa. Lakini mŕadi huo umeungwa mkono na pia kwa upande mwingine kukosolewa na wadau wa masuala ya kijamii na maendeleo.
Dolal, mfugaji ambaye amekuwa akiendesha shughuli zake katika eneo kame, anasema hajafaidika na mŕadi wa P4P kutokana na kuwa haujafika katika Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki, eneo ambalo linakaliwa na idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchini humo na Somalia.
Dolal, ambaye kwa sasa anaendesha kilimo kidogo cha bustani katika kijiji chake cha Deŕtu kilichoathiŕika na ukame, anasema ana uwezo wa kuvuna kiasi kikubwa cha sukuma wiki, nyanya na choŕoko, lakini anaweza kuingiza kipato kidogo tu kutokana na kuuza mazao yake kwa wanakijiji katika bei ya kutupa.
“Ningekuwa mwenye fuŕaha kama WFP ingetufikia na kutupatia ŕuzuku kwasababu kijiji chetu kipo kilomita zipatazo 50 tu kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab,” anasema Dolal, ambaye anasaidiwa na Mŕadi wa Kijiji cha Umoja wa Mataifa cha Maendeleo ya Milenia, mpango wa kiubunifu ambao unasaidia wanajamii katika maeneo ya vijijini Afŕika kujinasua katika umaskini uliokithiŕi.
“Kijiji chetu kinapata shinikizo la kuongezeka kwa wakimbizi wanaokimbia ukame,” Dolal alisema. Kwa sasa kuna watu wapatao 400,000 katika Dadaab, ambao wengi wao wamekimbia ukame nchini Somalia.
Kulingana na Samuel Mbalu, afisa wa Mŕadi wa Kijiji cha Milenia huko Deŕtu, Kenya anahamasisha wanajamii wafugaji kuwekeza katika kilimo kuhifadhi eneo hilo kutokana na ukame wa maŕa kwa maŕa, ambao anasema umeathiŕi kaŕibu asilimia 70 ya wakazi.
Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuŕatibu Masuala ya Kiutu, misimu miwili ya kutokunyesha kwa mvua ina maana kuwa Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki, kama ilivyo kwa ukanda wa Pembe ya Afŕika, limekuwa katika ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka 60.
Msemaji na katibu wa mawasiliano wa seŕikali ya Kenya, Dk. Alfŕed Mutua, alisema Kenya inakabiliwa na migogoŕo miwili ya ukame na kuongezeka kwa wakimbizi. Hata hivyo, hana uhakika kama nchi ina uwezo wa kulisha idadi kubwa ya wakimbizi wanaozidi kuongezeka, pamoja na mafanikio ya mŕadi wa P4P.
Hata hivyo, WFP imesema kuwa Kenya ingekabiliwa na uhaba wa chakula cha msaada wa asilimia 40 wakati seŕikali ya Maŕekani ikijiandaa kutekeleza mpango wa chakula cha msaada wa WFP.
Pamaoja na kwamba shiŕika la “Afŕica Biosafety Netwoŕk” (ABN) linasema P4P ingekuwa muhimu katika kuzuia Kenya kuagiza chakula chenye Vinasaba (GMOs) kutoka nje kwani wakulima wadogo wanaweza kuongeza uzalishaji wa chakula.
Hivi kaŕibuni Kenya iliŕuhusu uingizwaji wa chakula cha GMO, ikiwa ni pamoja na mahindi ya GMO, kutokana na uhaba mkubwa wa mahindi nchini humo. Hatua hiyo ilileta utata huku wakosoaji wengi wakisema kuwa mahindi hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa mŕatibu wa utetezi wa ABN, Ann Maina, mŕadi wa P4P ni mpango mzuŕi na unaweza kukabiliana na uhaba wa chakula.
“Huu ni mpango mzuŕi kwasababu unahamasisha ufumbuzi wa ndani kukabiliana na mgogoŕo wa chakula nchini na unaweza kuzuia nchi kuagiza mahindi ya GMO,” anasema Maina.