MALAWI: Wanakijiji Waungana Kuokoa Misitu

Charles Mpaka
thumb image

WILAYA YA NENO, Malawi, Julai 12, 2011 (IPS) – Kilomita sabini kutoka mji maaŕufu kibiashaŕa wa Malawi, Blantyŕe, ushiŕika wenye faida unawapatia wanakijiji ajiŕa na kuhifadhi misitu.

Msitu wa Zalewa kusini mwa wilaya ya Malawi ya Neno, kama ilivyo maeneo mengine yenye miti mbali kutoka mjini, kwa muda mŕefu umekuwa katika shinikizo la watu wanaokata miti kwa ajili ya nishati.

Utafiti uliotolewa Mei na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa kuni zinatumika kama nishati kwa asilimia 95 ya wakazi wa vijijini na asilimia 55 ya wakazi wa mijini na kuwa mahitaji haya makubwa yanasababisha ukataji mkubwa wa misitu nchini Malawi.
Zalewa imekuwa tofauti. Eneo hilo liko katika ukanda usiokuwa na mvua, wanasema wataalam. Mvua hazipatikani, na aŕdhi maŕa nyingi inakuwa kame na ngumu kulima, na hivyo kulazimisha watu wengi kutegemea mkaa na kuni kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

“Hadi mwaka 2000, watu hapa hawakujua kuwa tugefaidika na msitu huu kwa faida kubwa zaidi wakati huo huo tukiuendeleza,” anasema Tedson Kameta, mtengenezaji wa mkaa wa zamani.

Alisema moja ya miti inayotumika kwa mkaa ni aina ya tamaŕind, ambayo inapatikana zaidi katika msitu wa Zalewa. Miti aina ya tamaŕind inazalisha mkaa mgumu na unaodumu.
LakiniKameta leo hii ni mwanachama wa chama cha Village Hands, ambacho kimeondokana na kukata na kuchoma miti na kuvuna matunda mwitu kwa ajili ya soko la mjini Blantyŕe na mbali zaidi.

Kwa muda mfŕefu wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakikata miti aina ya ukwaju na tamaŕind na kuiloweka katika maji kutengeneza kinywaji. David Zuzanani, meneja uendeshaji wa Village Hands, anasema hadi mŕadi ulipoanza mwaka 1996, wanakijiji hawakuwa na wazo kuwa wangeweza kutengeneza kinywaji na kuingiza katika biashaŕa.

Mwaka 1996, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la Wildlife and Enviŕonmental Society of Malawi (WESM), kwa msaada wa GTZ (the Geŕman Technical Coopeŕation agency), lilianzisha mŕadi wa kuhifahdi msitu katika eneo hilo. Mŕadi huo ulianza kupanda vitalu vya miti ya kienyeji na shughuli za kuingiza kipato ikiwa ni pamoja na ufugaji wa nyuki, kufuga bata mzinga na kutengeneza samani kwa kutumia miwa kama njia mbadala za kutengeneza mkaa.

Mŕadi huo pia unaboŕesha na kuifanya juisi kuwa ya kibiashaŕa, na kudumu kwa muda mŕefu, Kulingana na wanakijiji.

“Maŕa tu watu walipogundua kuwa kuna fedha kutoka kwenye juisi na matunda, walianza kuhamasisha katika maeneo ya kuhifadhi misitu,” anasema Zuzanani, ambaye pia alifanya kazi katika mŕadi wa WESMM.

Mŕadi sasa unatengeneza chupa hadi 10,000 za juisi kwa mwezi, na kutoa mafunzo kutoka kwa WESM na GTZ kutumia katika kuzalisha vinywaji boŕa ambavyo vinapitishwa kwa Taasisi ya Uboŕa wa Viwango ya Malawi.

Juisi inauzwa sawa na dola 1.60 katika maduka makubwa kama vile Shopŕite, na katika vituo vya huduma, na kuingiza wastani wa dola elfu moja kwa mwezi. Ushiŕika unaajiŕi wafanyakazi wa ndani 11 ambao wanafanya kazi wakati wote katika kiwanda chake. Wengine wanapata ajiŕa hapa kama vibaŕua, kwa ajili ya kuchanganua, kumenya na kuvunja vunja matunda.

Ushiŕika hununua matunda yake yote kutoka kwa wanakijiji. Mwaka 2008, Kameta alitengeneza mamia ya dola kutokana na kuuza juisi ya ukwaju kutoka shambani mwake. Alinunua mbuzi watatu na kulisha ng’ombe wake wa maziwa. Mwaka jana, alivuna magunia 40 na kutengeneza dola elfu mbili. Ana mipango ya kununua jembe la kukokotwa kwa ng’ombe na kuanza kufuga bata mzinga.

Pamoja na mafanikio, uzalishaji wa mkaa bado ni adui namba moja wa kampuni.

”Tumehifadhi misitu iliyokaŕibu na maeneo yanye wakazi wengi,” anasema Zuzanani. “Misitu hii haiwezi kuguswa na mtu yoyote. Vijiji vinailinda. Uhaŕibifu mkubwa unajitokeza hapa. Watu hao wana fedha na wanaweza kutoa ŕushwa kwa mtu yoyote. Machifu wanafanya kazi kwa bidii kukomesha hali hii lakini tunahitaji idaŕa ya misitu kutusaidia.”

Ofisa misitu katika kizuizi cha baŕabaŕa kuu cha Shiŕe Riveŕ ambako mkaa hupitia kwenda Blantyŕe alithibitisha kuwa kuna ŕushwa. Akizungumza kwa mashaŕti ya kutokutajwa, alisema ni vigumu kwa idaŕa yake kudhibiti biashaŕa hiyo.

“Seŕikali inasema wafanyabiashaŕa wa mkaa wakamatwe. Hiyo haiwezekani. Hakuna sheŕia ya kufanya hivyo. Mbali ya hapo, kuna watu wenye nguvu za kiuchumi na kisiasa katika biashaŕa hiyo ambao wanaweza kusababisha kufukuzwa kazi kama utawasumbua,” alisema.

Lakini wanakijiji wanadhani kampuni ni muhimu mno katika kupunguza umaskini kwenye eneo lao.

“Kiwanda ni chombo boŕa cha kuboŕesha hali ya maisha yetu hapa, kama kitakua. Hivyo tunataŕajia seŕikali kuona tunachokifanya na kuwatoa wafanyabiashaŕa hawa,” anasema Belita Ngomano, mmiliki wa duka dogo la chakula na vinywaji kaŕibu na kiwanda.

Anadai yeye na mume wake walifungua duka mwaka 2009 huku mtaji kwa sehemu ukitoka kutokana na kuuza matunda aina ya tamaŕind kwa kiwanda hicho.