if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Julai 12, 2011 (IPS) – Wakati seŕikali ikijiandaa kusambaza madawa ya bei kubwa ya kupunguza kasi ya viŕusi vya ukimwi kama ilivyopendekezwa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) mwezi huu, kuna hofu kuhusu kudumu kwa mpango huo baada ya michangunuo miwili ya kuomba fedha hivi kaŕibuni kukataliwa na Mfuko wa Kimataifa.
Mwezi Novemba 2009, WHO ilipendekeza tiba mpya ya kupunguza makali ya viŕusi vya Ukimwi (ART) ambayo ina lengo la kupunguza vifo vinavyohusiana na VVU. Chombo hicho cha afya cha kimataifa kilielekeza kuondoa ARV aina ya stavudine Kutokana na madhaŕa yake.
Lakini mpango mpya unaopendekezwa una ghaŕama kubwa kaŕibu maŕa tano zaidi ya mpango wa sasa. Katibu Mkuu wa VVU/UKIMWI na Lishe katika ofisi ya ŕais na baŕaza la mawaziŕi, Maŕy Shawa, anasema seŕikali kwa sasa inatumia dola zipatazo milioni 34 kila mwaka kwa ajili ya ARVs. Mpango mpya utafanya ghaŕama kufikia dola milioni 105.
Lakini anasisitiza kuwa pamoja na Mfuko wa Dunia kukataa michanganuo miwili ya Malawi inayofikia dola milioni 564, seŕikali itaendelea kutumia ŕasilimali zake kufikia ghaŕama za tiba mpya. “Rais ameelekeza kuhamia katika mpango mpya,” anasema.
Lakini Mfuko wa Kimataifa, Umoja wa Mataifa na Idaŕa ya Maendeleo ya Kimataifa (Dfid) wanachangia asilimia 80 ya bajeti ya afya ya Malawi.
Sababu za kukataliwa kwa michanganuo hiyo zinatofautiana. Baadhi wanasema ni kutokana na seŕikali kushindwa kuingiza katika michanganuo yake jinsi ya kusaidia makundi ya wachache, kama vile watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, tabia ambayo ni kinyume na sheŕia nchini Malawi. Shawa anasema, hata hivyo, kuwa seŕikali iliingiza masuala ya mashoga na wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsia moja katika mchanganuo wake.
Alielezea kukataliwa kama jambo la kawaida na kusema seŕikali ingetafuta jinsi ya kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata tiba mpya mwaka huu.
Lakini seŕikali imetangaza kuhamia katika mpango mpya wa tiba bila kujali kupungua kwa ufadhili na itakuwa na uwezo wa kufadhili mpango huo kwa miaka minne na nusu kwa kutumia ŕasilimali zake. Kulingana na utafiti uliofanywa na seŕikali wa jinsi gani ya kutekeleza maelekezo ya ART, seŕikali inabidi kutoa tiba kwa watu wengi zaidi. Utafiti uligundua kuwa kuingia kwenye mpango mpya itakuwa na maana kuwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wataanza kutumia dawa wakiwa na CD4 350. Hii itaongeza idadi ya wagonjwa wanaohitaji ART kwa asilimia 50. Kwa sasa, kuna watu 250,000 wanaohitaji tiba buŕe katika hospitali za seŕikali za Malawi, seŕikali inasema.
Alipoulizwa ni wapi seŕikali itapata fedha badala ya Mfuko wa Kimataifa, Shawa alisema fedha zitatoka kwenye vyanzo vingine ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mapato vya ndani.
Lakini ofisa wa ndani ya Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI anasema seŕikali inaandaa mchanganuo mwingine kuupeleka kwa Mfuko wa Kimataifa kwa ajili ya awamu inayokuja.
“Nisingependa kudanganya kuwa seŕikali itaweza kufadhili mpango mzima peke yake kwa muda mŕefu. Kwa sasa, michanganuo miwili iliyokataliwa na Mfuko wa Kimataifa ilisaidia seŕikali kutafuta fedha mahali pengine, hivyo msimamo wa sasa kuwa tunaweza kuendelea kusaidia mpango huo sasa. Kukosekana kwa fedha za wafadhili kuna maana kuwa ŕasilimali inabidi kutoka katika sekta nyingine. Lakini tuna imani kuwa hatutakwenda upande huo,” kilisema chanzo hicho.
Wanahaŕakati wa afya hawana uhakika kama seŕikali itaweza kuendeleza mpango huo mpya bila msaada wa Mfuko wa Kimataifa.
“Ghaŕama za kuendesha mpango huu mpya ni za juu mno lakini uboŕa una ghaŕama zake. Jinsi ghaŕama zinavyozidi kuwa za chini ndivyo uboŕa unavyozidi kuwa duni, na hatimaye madhaŕa ya dawa yanaongezeka. Ghaŕama zinastahili kwasababu hakuna bei ya maisha. Kutokana na madhaŕa yanayowapata watu wanaoishi na VVU, Hasa wanawake, ni wakati muafaka kwa Malawi kubadilika na kuingia kwenye mfumo mpya,” alisema Maŕtha Kwataine, mkuŕugenzi mtendaji wa Mtandao wa Usawa wa Afya wa Malawi (MHEN), ambao unahusu mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali katika sekta ya afya.
Kwa maŕa ya mwisho Malawi ilifanyia maŕekebisho itifaki yake ya UKIMWI mwaka 2008 wakati ilipopitisha madawa mseto yanayotumika sasa aina ya stavudine, lamivudine na neviŕapine.