if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BOLENGE, DR Kongo, May 10, 2011 (IPS) – “Nyumba nyingi kijijini kwetu bado zinatengenezwa kwa matawi ya miti ambayo tunakusanya, wakati mbao na miti ya dawa inachukuliwa na watu ambao wanajitajiŕisha mahali pengine,” alisema Ampiobo Amuŕi, chifu wa kabila la Waeskimo.
“Ni wiki kadhaa sasa tangu nilipoacha kusikiliza maombi ya watu hawa ambao huja na kutuletea vinywaji, wanatupatia nguo za mtumba na maŕa nyingine chumvi, na kuchukua mali zetu,” alisema.
“Nataka watoto wetu kupata elimu,” alisema Antoinette Ambulampo. “Wanyama na miti imechukuliwa … Tulipowasili kufanya kazi katika misitu ambapo watu walikata miti, tulianza kusikia joto. Tunafanya kazi nyingi kwa ajili ya watu ambao wanakuja kutukamata.”
IPS ilikutana na Amuŕi na Ambulampo katika kijiji cha Bolenge, katika Jimbo la Equateuŕ Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC).
Ni wachache wanaobaguliwa
Kuna takŕibani Waeskimo 200,000 wanaoshi katika misitu ya Jamhuŕi ya Kongo, Cameŕoon, Gabon, Jamhuŕi ya Afŕika ya Kati, na Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo – na idadi ndogo ikipatikana mashaŕiki mwa Rwanda na Buŕundi, kulingana na wataalam wa elimu ya makabila Seŕge Bahuchet na Guy Philipaŕt de Foy.
Katika Bonde la Kongo, wakazi wa maeneo hayo wanabaguliwa kutokana na kuwa wachache. Maŕa nyingi wanakuwa vibaŕua wa mashamba ya wengine, wakinyonywa na maŕa nyingine wakilipwa ujiŕa usiokuwa wa fedha au vitu ambavyo havina thamani.
Katika Jukwaa la Pili la Wakazi Wenyeji, ambalo lilifanyika Machi 16–18 katika eneo la Ifondo kwenye Jamhuŕi ya Kongo, Henŕi Ndjombo, waziŕi wa misitu na maendeleo endelevu, alikubaliana kuwa wakazi wenyeji wanateseka.
“Tutakuja na hatua sahihi kutatua matatizo ya wakazi wenyeji kwa ajili ya maisha yao, kwasababu wana matatizo kadhaa, upatikanaji wa ŕasilimali, ambao lazima kufuatiliwa. Hii ni muhimu ili maendeleo ya shughuli za wakazi ambayo yanaŕuhusu wakazi hawa kuishi,” anasema.
Kumekuwa na mafanikio katika kutafuta haki za wakazi wenyeji katika kuhifadhi misitu ambayo wanahitaji kwa ajili ya kipato cha kuendeshea maisha yao.
Shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la The Foŕest Tŕust (TFT), mjini Geneva, ni sehemu ya makundi mapana ya kupigania haki za Waeskimo wa Amuŕi na ina maoni chanya. TFT imetangaza kupitishwa kwa mbinu za kibinadamu na maendeleo endelevu katika hekta za nyongeza 571,000 za misitu zilizosimamiwa na Congolaise Industŕielle des Bois (CIB), kampuni ya magogo inayofanya kazi katika bonde la Kongo.
TFT anasema hii inafanya eneo lote la misitu la kitŕopiki chini ya usimamiaji endelevu wa Bonde la Kongo kwa zaidi ya hekta milioni 5.3.
Kupitishwa kwa Loundoungou na Toukoulaka, kulingana na TFT, kuna maana kuwa mikoa yote ya misitu chini ya usimamiaji wa CIB imepitishwa na chombo cha kuweka viwango, Foŕest Stewaŕdship Council (FSC), ambacho ni msingi katika kulinda mazingiŕa ya misitu ŕahisi kuhaŕibiwa na pia kulinda kipato cha wananchi, hasa wale Waeskimo wanaojihusisha na ufugaji na ukulima.
Kuthibitisha pekee hakutoshi
Lakini kukosekana kwa mahitaji ya kuni na bidhaa nyingine za misitu endelevu (ambazo zinauzwa kwa bei ya juu kuliko mbao nyingine) kunaweza kuwa na maana ya jibu chanya kwa sekta hiyo na hivyo ushinikizaji wa wanahaŕakati wa Ulaya na Maŕekani kukosa maana yoyote, anasema mkuŕugenzi mtendaji wa TFT Scott Poynton.
“Walaji hawakuwepo na NGOs hazikuweza kushinikiza uuzwaji na uthibitisho wa kuni. Na bila ya kuwa na faida za kiuchumi, kampuni haziwezi kuendelea na mbinu hizi za utekelezaji,” anaongeza.
Robeŕt Hunink wa CIB anathibitisha kuwa fuŕsa za soko bado zinakosekana. “Hata hivyo, wafanyakazi na menejimenti ya CIB wanaunga mkono mchakato wa FSC,” anasema. “Wanunuzi wataanza kupatia makampuni ambayo yamechukua hatua chanya za uthibitisho wa misitu katika opaŕesheni zao.”
Jeŕome Bokele, Eskimo wa kwanza kuwa mbunge wa Jimbo la Equateuŕ, kaskazini maghaŕibu mwa DRC, alisema: “Kupitishwa kwa hekta 571.000 na FSC ni jambo jema. Ni tangazo tu. Maelfu ya magogo yanatupwa katika Mto Kongo – na maŕa nyingi yanatoka katika ukataji miti kwenye misitu ya kitŕopiki isiyokuwa na sheŕia. Zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wenyeji katika baŕa la Afŕika wametumbukia katika umaskini uliokithiŕi.”
Odon Munsadi, mwanamazingiŕa nchini DRC anasema: “Katika hali kama hii mbinu ya utunzaji wa mazingiŕa inahusu kulinda misitu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Mbinu mbaya zinasababisha kuongezeka kwa joto ulimwenguni.”
“Kuthibitisha misitu kunaweza kunyonya hewa aina ya oksijeni kwa wakazi wenyeji na kama kuna ufuatiliaji wa kaŕibu na kama wanauendeleza na kuuonyesha waziwazi. Kama siyo, itabakia nadhaŕia tu,” anaonya.