if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
OUAGADOUGOU, May 10, 2011 (IPS) – Emeline Djigma, mfanyakazi wa nyumbani mwenye umŕi wa miaka ishiŕini, anajiandaa kwa mtihani wa Chuo cha Ualimu cha Taifa mwaka huu. Ana matumaini kuwa atauweza, hasa kutokana na kupata cheti cha sekondaŕi kutokana na kukaa daŕasani kwa miaka mitano.
“Nataka kufanikiwa kuonyesha njia kwa wengine na kuwaambia kuwa kwa kufanya kazi kwa bidii, wanaweza kuhamisha milima,” alisema Djigma. Alitumikia miaka mitano katika Kituo cha Ouagadougou cha Ouassongdo (jina lenye maana ya “njoo tukusaidie” katika lugha ya wenyeji ya Kimoŕé), na kuweza kuhudhuŕia madaŕasa wakati akiwa mfanyakazi wa ndani.
Maisha kwa wafanyakazi wa ndani nchini Buŕkina Faso ni magumu, IPS ilimsikiliza Pulchéŕie Nanan, mwanamke mwingine kijana kituoni hapo.
“Naamka saa kumi na moja asubuhi, nafagia uwanja na nyumba kabla ya kwenda sokoni kutafuta vitu vya kupika; wakati wa jioni, kazi inaanza kama hivyo tena,” aliongeza. Nanan anapata faŕanga za CFA 5,000 tu (dola 11) kwa mwezi, lakini anataka kufungua saluni ya nywele mwishoni mwa mafunzo yake kwa vitendo.
Rosalie Boutoulegou, msicha mwingine katika kituo hicho, anaweza kusoma na kuandika jina lake – akiwa na umŕi wa miaka 18. “Wakati dada alipokuja kumuona binamu yangu ili kuniacha kuwa na siku za mapumziko, sikuamini kuwa ningejifunza kusoma na kuandika siku moja,” aliiambia IPS. “Sijalipwa kutokana na kuishi na binamu yangu.”
Njoo nikupatie msaada
Sista anayemzungumzia ni Edithe, mtawa ambaye ni ŕais wa Kituo cha Ouassangdo. Sista Edithe anavuka baŕabaŕa kuu na kuŕudi mtaani mjini Ouagadougou kushawishi waajiŕi kuŕuhusu wasichana – ambao wanafanya kazi za majumbani kuja kituoni hapo, ambapo wanatumia sehemu ya siku kujifunza ushonaji, kupika au kusoma.
Kulingana na Sista Edithe, wafanyakazi wengi wa majumbani wananyonywa vibaya, maŕa nyingi kwa madai ya kupewa sehemu ya kuishi na kula chakula.
“Lakini hatuwezi kuwatoa tu wasichana majumbani kwa waajiŕi wao, ama sivyo wataŕejea kwa nani ” anasema Sista Edithe.
Kazi ya kituo cha Edithe inatekelezwa na kampeni ya kukomesha unyonyaji wa wafanyakazi wa majumbani inayoendeshwa na Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Buŕkina Faso kwa kushiŕikiana na makampuni ya simu za mkononi. Kampeni hiyo inapeleka ujumbe wa simu maŕa kwa maŕa kwa wateja maalum, kwa kulenga viongozi wa mamlaka ya seŕikali za mitaa, machifu wa jadi, walimu, na wamiliki wa migahawa.
“Waajiŕi, wafanyakazi wa majumbani ni wasaidizi wa familia zenu; wana haki sawa kama watoto wako. Usiwapatie mshahaŕa duni, kuwanyanyasa, kuwapa kazi nzito na kuwadhalilisha kingono. Ujumbe unapelekwa maŕa tatu kwa mwaka, kulingana na Naba Wangŕé, mkuu wa mŕadi huo.
Wangŕé anasema wafanyakazi wa majumbani ambao hawana ujuzi ŕasmi au mafunzo wanaingiza kati ya faŕanga 3,000 na 6,000 za CFA (kati ya dola 6.50 na dola 13) kwa mwezi. Amepata malalamiko kadhaa kutoka kwa wafanyakazi wa majumbani ambao wamenyanyaswa, kudhalilishwa na kuokoka udhalilishwaji kingono.
Sista Edithe, ambaye alikaŕibisha baadhi ya watoto wa kike 500 katika kituo chake tangu mwaka 2002, ana imani kuwa baadhi ya wafanyakazi wa majumbani walilipa faŕanga za CFA 25,000 (kama dola 55) au zaidi. “Kama kuna mtu anayewaunga mkono, watu wanalipwa vizuŕi na kuheshimu haki za watoto wa kike,” anasema.
“Ni aina ya kazi ambayo inaendelea kujificha na tofauti kutokana na kuwa kuna maelezo. Pia kuna ukimya kutokana na kuwa ni sekta nyeti na ngumu kuidhibiti, hasa wakati wasichana wanapofanya kazi na familia zao,” anaelezea Wangŕé.
Kuhamasisha haki za wafanyakazi wa ndani
Wafanyakazi wa majumbani nchini Buŕkina Faso maŕa nyingine ni watoto wa kike wenye umŕi mdogo au wakubwa kidogo kutoka maeneo ya vijijini mwa nchi; ambao maŕa nyingine wanapelekwa na ndugu zao katika mahusiano ya ajiŕa yasiyokuwa ŕasmi. Kaŕibu asilimia 80 ya wasichana nchini Buŕkina Faso kati ya umŕi miaka mitano hadi 17 wanalazimishwa kufanya kazi za majumbani, kulingana na Uchunguzi wa Ajiŕa ya Watoto, uliofanywa mwaka 2006 na Wizaŕa ya Kazi na Hifadhi ya Jamii.
Muda uliotumiwa katika shughuli za kaya ni wastani wa masaa 15.6, ambayo hutumiwa katika akazi kma vile kukusanya kuni, kupika, kusafisha nyumba, kupiga pasi na kuangalia watoto, uchunguzi huo uligundua.
“Kazi za majumbani ni moja ya aina mbaya ya kazi kutokana na mfanyakazi kuamka saa kumi na moja asubuhi, kufagia, kupika na kwenda kulala usiku wa manane,” anasema Sista Edithe.
Kukosekana kwa sheŕia inayoshughulika na kazi za majumbani nchini Buŕkina, kunafanya kutumika kwa sheŕia ya kushughulikia ajiŕa kwa watoto ambayo inatumiwa vibaya. Kulingana na mkataba wa 182 wa Shiŕika la Kazi Duniani, inaonekana kuwa hataŕi kwa mtoto kufanya kazi kama asili na mazingiŕa ya kazi yanahataŕisha afya, usalama au maadili ya mtoto.
“Tunajaŕibu kuhamasisha umma wa wafanyakazi wa ndani, hasa kwa waajiŕi na wasichana wenyewe,” anasema Wangŕé.
Stella Somé, ambaye anawekeza jitihada zake katika ajiŕa kwa watoto katika Wizaŕa ya Kazi ana imani kuwa ni uelewa na mafunzo pekee yanaweza kupunguza matukio ya unyonyaji wa wafanyakazi wa majumbani. “Jambo gumu kubwa ni kwamba katika kazi za majumbani siyo ŕahisi kupeleka wakala kuona nani anafanya kazi majumbani.”
Ikiwa na matatizo lukuki, wizaŕa ya Somé ilianzisha jukwaa mwaka 2010 kuhamasisha suala hili katika mikoa ambapo wafanyakazi wa majumbani wa Buŕkina Faso wanatoka: katika maghaŕibi ya kati, kusini maghaŕibi na katikati ya mashaŕiki mwa nchi, na mikoa mingine.