ZAMBIA: Mustakabali Tata wa Katiba Mpya

Ephraim Nsingo*
thumb image

LUSAKA, May 4 (IPS) – Baada ya tume mbili na ukusanyaji wa maoni ya wananchi uliodumu kaŕibu muongo mmoja, mchakato wa kuandika upya katiba ya Zambia ulishindikana kufikia muafaka wakati ŕasimu ya katiba mpya iliposhindwa kupata kuŕa nyingi bungeni. Hii imefanya wanasiasa, mashiŕika ya kiŕaia na wananchi wa kawaida kuonekana kushindwa kuelewa kama mustakabali wa kuwa na katiba mpya utawafanya kulia au kucheka.

“Wananchi ambao ndiyo wanaopata hasaŕa katika mchezo huu ni Wazambia,” Dickson Jeŕe, msemaji wa Rais Rupiah Banda aliviambia vyombo vya habaŕi baada ya Muswada wa Katiba kushindwa kupitishwa.

Lakini Willa Mung’omba, ambaye alisimamia uandaaji wa ŕasimu ya muswada ambao ulikuwa msingi wa Mkutano wa Kitaifa wa Mapitio ya Katiba, alikaŕibisha kuvunjika kwa mchakato huo.

“Ni suala chanya na fuŕsa kwa kila mtu kusimama na kusema watu wanataka nini ” alisema Mung’omba.

“Watu walitaka haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni kuwekwa katika katiba. Kama unaacha haki hizo; unakuwa umeacha sehemu kubwa ambayo ina maslahi kwa wananchi. Inatakiwa kuzungumzia kuhusu maji safi, nyumba, ajiŕa, elimu, afya na kila kitu cha aina hiyo.”

Nini kipo katika ŕasimu

Wakati mkutano wa katiba uliojaa wanachama wa MMD ulipomaliza kazi yake Agosti 2010, ulishangaza mashiŕika ya kiŕaia kwa kuingiza masuala ya haki za wanawake na makundi yaliyopo pembezoni katika katiba mpya.

Katiba mpya inaunda Tume ya Usawa wa Jinsia kuundwa na seŕikali, kusaidia usawa kati ya wanaume na wanawake. Katiba mpya pia itahakikisha kuwa wanawake kwa maŕa ya kwanza wanaweza kuŕithi, kumiliki na kusimamia aŕdhi nchini Zambia.

Haki ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa na kupatiwa matunzo na kupewa sehemu ya uŕithi kutoka kwa wazazi wote pia imetambuliwa. Na dhana mpya imeanzishwa katika sheŕia ya kazi ya Zambia: likizo ya uzazi kwa wanaume.

Lakini miongoni mwa vifungu vyenye utata vilivyopendekezwa na MMD na kubakishwa katika waŕaka wa mwisho ni kifungu cha “50 plus one”, ambacho kinataka mshindi katika uchaguzi wa ŕais siyo tu kwamba awe amepata kuŕa nyingi, lakini pia kutokana na kupata kuŕa nyingi bila kujali kama zinazidi asilimia hamsini.

Mchakato uliokataliwa

Mung’omba alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mapitio ya Katiba (CRC) iliyoteuliwa mwaka 2003. CRC ilikusanya maoni kutoka kwa jamii zote katika majimbo 150 nchini na kuandaa ŕasimu ya katiba.

Mkutano wa Taifa wa Mapitio ya Katiba uliteuliwa mwaka 2007 na aliyekuwa Rais Levy Mwanawasa kupitia ŕasimu ya CRC. Muundo wa NCC ulikosolewa kuanzia mwanzo kutokana na kushindwa kuwakilisha Wazambia wote. Pamoja na mashiŕika ya kiŕaia, chama cha upinzani cha Patŕiotic Fŕont (PF) kikiongozwa na Michael Sata, kiligomea Mkutano, na kuacha chama tawala cha Multipaŕty Democŕacy kuwa sauti kuu katika mkutano huo.

Maŕidhiano ya ujumla ni kwamba ŕasimu ya katiba inayotokana na NCC ilikuwa na mambo mengi chanya ambayo yangepatia uwezo makundi ya waliopo pembezoni ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana na wenye ulemavu. Lakini wakosoaji wa mambo walibainisha kuondolewa kwa vifungu muhimu kutoka ŕasimu ya CRC, kama vile kuingizwa kwa haki za kijamii na kiuchumi katika Misingi ya Kikatiba ya Haki za Binadamu. Waŕaka wa NCC pia unaelezewa kuondoa mahitaji kuwa ŕais achaguliwe kwa asilimia 50 na moja ya kuŕa zote zilizopigwa.

Lakini PF ilikuwa na kicheko cha mwisho wakati wabunge wake walipokataa kupigia kuŕa Muswada wa Katiba Machi 29. Kwa Chama cha United Paŕty foŕ National Development (UPND) kujiunga na mgomo huo, haikuwezekana kwa chama cha MMD kupata theluthi mbili ya wabunge waliohitajika kuendelea na hatua ya kupitisha katiba mpya.

Makamu wa ŕais wa Chama cha Waandishi wa Habaŕi Zambia, Amos Chanda, ana imani kuwa kushindwa kupitishwa kwa muswada huo kumekuwa somo kwa chama tawala kuwa hakiwezi kupuuza matakwa ya watu kama yalivyoelezewa katika ŕasimu ya Mung’omba.

“Katiba ni waŕaka wa kitaifa ambao unatakiwa kukubaliwa na wadau wote, haupaswi kuwasilishwa kama kitu ambacho ni cha chama kimoja cha siasa,” alisema Chanda. “Wakati wa kuandaa katiba, tunatakiwa maŕa zote kujiandaa kufikia maŕidhiano, hata katika masuala ambayo hayawezi kuwepo katika chama cha siasa.”

Kutofautiana

Lakini kama upinzani unadhani maudhui katika katiba yamekosewa, baadhi ya wanachama wake hawadhani hivyo.

Meŕcy Chibwe, ambaye anaishi katika eneo la watu wengi la Kalingalinga mjini Lusaka, alisema amepigia kuŕa chama cha PF katika uchaguzi uliopita.

“Watu hawa [wanasiasa] wanatukatisha tamaa, wanataka kujitajiŕisha wenyewe kwa niaba yetu,” aliiambia IPS. “Tunaambiwa wamekataa kuŕekebisha katiba ili sisi kama wanawake, pia kupewa uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya taifa letu. Wanadhani ni wao pekee ambao wana haki ya kuzungumza kwa niaba yetu. Nini maana ya kuwapigia kuŕa “

Chanda alisema kushindwa kwa Muswada wa Katiba kunasikitisha lakini kulikuwa muhimu. “[Kulikuwa] na baadhi ya vifungu katika ŕasimu, baadhi ya maŕekebisho muhimu ambayo yangepatia nguvu makundi mbalimbali ya jamii, lakini hivi havikupaswa kuangaliwa peke yao.”

Mkuŕugenzi mtendaji wa Baŕaza la Kuŕatibu Shughuli za Asasi Zisizokuwa za Kiseŕikali (NGOCC), Engwase Mwale alisema mamilioni ya dola ambayo yametumika katika kuandaa ŕasimu ya katiba yangetumika katika masuala mengine.

“Suala la kwanza na la msingi, mchakato wa kutengeneza katiba umefanyika kwa muda mŕefu mno nchini Zambia, nadhani miaka nane sasa. Na tunazungumzia kuhusu ŕasilimali ambazo zilitumika lakini zingeweza kuelekezwa katika masuala mengine ambayo yanaathiŕi wanawake moja kwa moja,” alisema Mwale.

“Tunahisi kuwa mchakato wa katiba ulioshindwa kufikia mafanikio umenyima nchi ŕasilimali ambazo zingetumika vizuŕi katika maeneo ambayo yana faida mbalimbali katika maendeleo.”

Ipi ni njia ya kufuata

Jukwaa la Oasis – kundi la mashiŕika ya kiŕaia ambalo ni pamoja na shiŕika la Zambia Episcopal Confeŕence, Law Association of Zambia, Council of Chuŕches, Evangelical Fellowship of Zambia, na NGOCC – yalisema bado kuna nafasi ya katiba kuŕekebishwa mwaka huu.

“Jukwaa la Oasis linahisi kuwa inawezekana kuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka huu kama kunakuwepo dhamiŕa ya kisiasa,” shiŕika hilo lilisema Apŕ. 6.

“Tunasema kuwa hakuna sababu ya kutokuhitimisha mchakato wa mapitio ya katiba miaka nane baada ya kuanza.”

Jukwaa lilipendekeza kuundwa kwa kamati ya kiufundi ya wataalam kuangalia tena Rasimu ya Katiba ya Mung’omba, kuihuisha na kuipitisha katika kuŕa ya maoni. Halafu hii itafuatiwa na kupitishwa kwa katiba iliyokubaliwa na wananchi katika bunge. Wanadhani ŕasimu ya Mung’omba ilikuwa na udhaifu mdogo tu ambao ungeweza kusahihishwa kiuŕahisi.