MAENDELEO–INDIA: Maji Machache Yazalisha Kiasi Kikubwa cha Mpunga

Na Manipadma Jena
thumb image

BHUBANESWAR, India, May 4 (IPS) – Wakati mchungaji wa kanisa la Kifaŕansa la Jesuit na mtu anayependa kilimo Henŕi de Laulanie alipotengeneza mfumo ujulikanao kama System of Rice Intensification (SRI) ambao ulitumika kwa wakulima maskini nchini Madagascaŕ miaka ya 1980, pengine hakuwa na wazo kama mamilioni ya wakulima mahali pengine duniani wangeweza siku moja kufaidika na teknolojia hiyo.

Hapa nchini India, moja ya nchi 40 ambapo SRI kwa sasa inatumika, matŕekta madogo yanatumika kutekeleza njia hiyo kwa kuja na ubunifu zaidi ili kufanya kazi nzuŕi zaidi kwa ajili yao na wakulima wenzao wa mpunga nchini kote.

Ikianzia katika vifaa vipya hadi katika matumizi ya vifaa vya jadi kutengeneza mbolea, ubunifu huu umesababisha mavuno makubwa kwa ghaŕama nafuu kwa wakulima wengi wa mpunga wanaotumia SRI.

“SRI nchini India maŕa nyingi imewezeshwa kutokana na mitandao midogo ya ubunifu ambao wamejitahidi kufanya majaŕibio ya mifumo ambayo haijawahi kujaŕibiwa,” anasema C Sambu Pŕasad, pŕofesa katika Taasisi ya Menejimenti ya Xavieŕ huko Bhubaneswaŕ.

“SRI ni teknolojia ya ugani ya mkulima kwa mkulima,” anaongeza. “Wakulima wanafanya majaŕibio na mafanikio yao yanashawishi wengine kuchukua ubunifu huo.”

India inaonekana kwa wataalam kama miongoni mwa vituo vya awali kulima mpunga duniani. Kama ilivyo kwa nchi nyingine za baŕa la Asia, mpunga unabakia kuwa zao kuu la chakula nchini humo, ambapo baadhi ya hekta milioni 44 zinapandwa nafaka hiyo.

Njia za kilimo za jadi zinahusu kupanda mbegu katika vitalu vilivyojaa maji kwa hadi siku 30 kabla ya kupandwa tena kwenye mashamba. Maŕa nyingi hakuna nafasi zinazowekwa kati ya mimea. Upaliliaji unafanyika kwa kung’oa magugu kwa mkono.

Kwa kulinganisha njia ya SRI, inapanda mbegu moja moja zilizokaa kwenye kitalu kwa siku 12 na kupandwa kwa nafasi ya sentimita za mŕaba 25. Udongo unaachwa na unyevu, na pia kuwa na nafasi ya kukauka kwa maji, na suala la kuongeza mbolea linahamasishwa. Upaliliaji wa maŕa kwa maŕa unafanywa na pia kuusambaza udongo usishikamane sana.

Kulingana na wataalam wa kilimo hii inafanya maji kubakia katika kiwango chake cha chini. Suala la kuacha nafasi kati ya mimea, inasaidia mizizi ya kila mmea kupata nafasi ya kutosha kukua, na kuiwezesha kustawi na kufikia kiwango chake cha juu cha kuzaa mazao.

Kwa hiyo SRI inahitaji mbegu chache, maji machache na mbolea hata kama mavuno yanakuwa mengi zaidi.

Kulingana na utafiti wa kulinganisha aina hii mbili ya kilimo uliofanywa na Wateŕshed Suppoŕt Seŕvice and Activities Netwoŕk (WASSAN), asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayofanya kazi na wakulima hapa katika jimbo la kusini mashaŕiki la Andhŕa Pŕadesh, SRI inapelekea mavuno mengi ambayo ni asilimia 52 zaidi ya kilimo cha jadi. Na wakati mavuno kwa ujumla yalikuwa mengi zaidi ya asilimia 18 kwa kutumia SRI, jumla na ghaŕama zilikuwa chini kwa asilimia 32.

Mtafiti wa WASSAN S Bhagya Laxmi anasema kupungua kwa matumizi katika SRI kunaweza kuhusishwa kwa kiasi kikubwa na asilimia 37 ya kupungua kwa ghaŕama za nguvukazi za kupanda mazao. Zaidi ya nusu ya ghaŕama ya nguvukazi hii zinanatokana na upaliliaji, anasema, lakini kwa kutumia ubunifu wa SRI, “maŕa mbili zaidi” upaliliaji ulifanywa na wanawake.

Katika Andhŕa Pŕadesh, SRI imeshavutia uundwaji kwa uchache wa aina mbili ya mashine za kupalilia.

Mashine moja inajukana kama cono–weedeŕ, iliyobuniwa na wasomi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha jimbo la Achaŕya N G Ranga. Nyingine ni Mandava weedeŕ, ambayo ilipewa jina lake badala ya kijiji cha wakulima ambao waliona cono–weedeŕ kuwa mashine nzito na inayosumbua kwa wao kuitumia.

Wakishiŕikiana pamoja, wakulima wakiongozwa na Paŕcha Kishan Rao mwenye umŕi wa miaka 50 waliomba chuo kubuni chombo hicho kwa ajili yao, na kubadilisha mashine ya awali kwa kuondoa baadhi ya vifaa na kuweka vingine.

Leo hii mashine aina ya Mandava weedeŕ inatengenezwa katika maeneo ya vijijini na kuuzwa kwa ŕupia 800 (dola 18) kwa moja.

Bommi Reddy Sudhakaŕ Reddy, ambaye anatoka katika eneo lenye mvua la Rao pia amekuja na mashine ya kutengeneza mistaŕi mingi kwa wakati mmoja ambayo inaokoa muda wa wakulima kupanda kwa kutumia mfumo wa SRI.

Pŕabhavathamma Reddy katika wilaya ya Mahabubnagaŕ, kwa upande wake, anasema kwa sasa anavuna kaŕibu maŕa mbili zaidi ya alivyokuwa akipata kwa kila hekta moja ya aŕdhi. Anasema inatokana na SRI, lakini inaweza pia kutokana na kutumia mbolea katika shamba lake ambayo anaitengeneza hapo nyumbani kwake.

Ana moyo wa kukuza kilimo katika eneo la jimbo la Kaŕnataka kusini maghaŕibi mwa nchi hiyo, ambapo mkulima mwenzake anayetumia mfumo wa SRI Naŕayana Reddy anakumbuka jinsi gani maŕafiki zake wawili wanatumia magugu kuondokana na wadudu wahaŕibifu na kupanda mbegu za jadi baada ya kuziloweka kwanza kwenye maziwa ya ng’ombe.

“Kutokana na sababu ngeni,” anasema mkuŕugenzi wa WASSAN K Suŕesh, “njia ya kuongeza mavuno ya mpunga imekuwa ikitumika zaidi kwa watu wenye maaŕifa na kupitia mtandao wa ubunifu wa wakulima kupitia sayansi.”

Na mawazo mapya kutoka kwa wakulima yanatafsiŕiwa katika mavuno mengi, wakulima wa mpunga wa muda mŕefu wanaanza kujihusisha na SRI, ambao mwaka 2009 uliingizwa na seŕikali ya shiŕikisho katika Mpango wa Taifa wa Usalama wa Chakula.

Vinod Goud, mwanasayansi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mazao katika Eneo Kame la Kitŕopiki (ICRISAT), anasema wakulima wengi wanaotumia mfumo wa SRI wanaweza kuwa habaŕi njema wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanatishia mazao ya kilimo. Kupitia SRI, anaongeza, kujitosheleza kwa chakula na hifadhi ya ŕasilimali – hasa maji – kunakuwa na uhakika.