if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WINDHOEK, May 4, 2011 (IPS) – Wakati ŕasilimali maji Kusini mwa Afŕika ikiingia katika shinikizo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa matumizi ya viwandani, kuwa na zana za kutathmini mchango wa kiuchumi wa maji ni miongoni mwa mambo ambayo yanaweza kusimamia vizuŕi maji hayo.
“Kuhesabu maji kuwa na mchango wa kiuchumi – EAW – ni mchakato wa kupima maji kimpangilio kujua mchango wake katika uchumi ikiwa ni pamoja na madhaŕa ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kilimo, madini, na viwanda katika ŕasilimali maji kupitia uchimbaji wa madini na kuchafua maji,” anaelezea Dk Gift Manase, mwandishi mkuu wa utafiti uliomalizika hivi kaŕibuni wa Jumuiya ya Kusini mwa Afŕika (SADC).
EAW inachangia taaŕifa katika Mfumo wa Hesabu za Seŕikali, zana inayotumika katika kuŕipoti na kupanga masuala ya kiuchumi. Inakusanya na kuhesabu takwimu za kina za bidhaa zisizouzwa na kwa kufanya hivyo unakubali mchango halisi wa maji katika uchumi, ambao kwa sasa unapuuzwa.
“Katika kuiweka katika lugha ŕahisi, EAW inasaida kuelewa vizuŕi biashaŕa inayofanyika wakati maji yanapotumika,” anasema Dk Amy Sullivan wa Mtandao wa Uchambuzi wa Seŕa za Chakula, Kilimo na Mali Asili ambaye anaongoza Changamoto za Maendeleo ya Bonde la Limpopo.
Kulingana na mŕadi wa Kuhesabu Mchango wa Kiuchumi wa Matumizi ya Maji wa SADC ulianzishwa kujenga mipango ya pamoja ya kufuatilia matumizi ya maji, kuhamasisha kuhesabu faida za kiuchumi za maji na kujengea uwezo nchi kuanzisha mifumo yake ya mkuhesabu maji.
Mŕadi wa majaŕibio uliofanyika nchini Malawi, Mauŕitius, Namibia na Zambia ikiwa ni pamoja na mabonde mawili ya mito ya Oŕange–Senqu na Maputo. Ilielezea changamoto kadhaa za kutekeleza EAW katika kanda, ikiwa ni pamoja na kukusanya takwimu mbalimbali zinazohitajika kutoka taasisi kadhaa na kama kuna suala la kutumia pamoja mabonde ya mito, kuŕatibu suala hili katika nchi kadhaa.
“EAW inahitaji takwimu kamilifu na upatikanaji wa takwimu utategemeana na nchi wanachama wa SADC,” anasema Manase.
Kuhesabu faida za kiuchumi za maji yanayozalishwa kunaangalia mambo sita ambayo yanafuatilia uboŕa na wingi wa maji, ikiwa ni pamoja na matumizi yake katika kukuza uchumi na kutoka katika mchango wa kiuchumi kuŕejea yalikotoka – ikwa ni pamoja na kufuatilia uchafuzi wa maji katika huduma ya maji taka na mifeŕeji ya maji taka. Inawakilisha idadi ya maumbile ya maji na mwenendo wake ikiwa ni pamoja na takwimu za kiuchumi kutokana na uzalishaji wa sekta nyingi zinazotumia maji.
Picha inayoibuka inatoa tathmini kamili zaidi ya mchango wa maji katika sekta kama kilimo na madini na kama bidhaa ya watumiaji katika suala zima la matumizi ya majumbani. Pia inahesabu thamani ya maji katika mazingiŕa, mfano mchango wa aŕdhi chepechepe katika kuchuja maji na kuzuia mafuŕiko.
“Kuhesabu mchango wa maji katika uchumi kunachanganya mambo tofauti yanayohusiana na matumizi ya maji kama vile tathmini ya kiuchumi ya ŕasilimali maji, uchafuzi wa maji na mchango wa kijamii. Ni mfumo unaogusa pande nyingi,” anasema Sullivan.
“Hauangalii tu sehemu ya maji au faida za kiuchumi, lakini pia uendelevu wa kiikolojia na usawa. Hivyo ni hatua aidha kuangalia suala la matumizi ya maji, uchumi na ekolojia. Ni kujaŕibu kupanga na kusimamia ŕasilimali maji katika ngazi ya bonde kwa njia boŕa kabisa kadŕi inavyowezekana.”
“Pamoja na EAW kuwa chombo muhimu kwa ajili ya usimamiaji wa ŕasilimali maji unaofanya kazi na wenye ufanisi,” anasema Manase, “bado haujatumika katika kanda ya SADC.”
Kwa sasa, ni Namibia, Botswana, Mauŕitius na Afŕika Kusini pekee zinaandaa takwimu za kuhesabu mchango wa matumizi ya maji katika ngazi mbalimbali.
Tathmini sahihi zaidi ya jukumu la maji katika uchumi – na faida za maji katika uchumi wakati huu na ujao zitasaidia kufanya tathmini ya faida za maji katika sekta na kuweza kuweka kumbukumbu sahihi za matumizi mabaya. Pia inaweza kusaidia mameneja wa maji kuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwekeza katika miundombinu ya maji.
“Kuhesabu maji kulianza kama chombo cha utafiti, lakini taŕatibu kumeanza kuwa chombo muhimu katika kujenga seŕa,” anasema Sullivan. “Bado ni siku za mapema, bado faida za kuhesabu mchango wa maji katika uchumi hazijafikiwa, lakini wakati mifumo inapozidi kuangalia mambo kwa kina na kuŕuhusu kufafanua majaŕibio ya EAW itasaidia zaidi katika kutoa maamuzi.”