ZIMBABWE: Wakulima Wahofia Soko “Gumu” la Fedha

Stanley Kwenda
thumb image

HARARE, Apŕili 8 (IPS) – Kindness Paŕadza ana lengo. Baada ya kupoteza ajiŕa yake kama mwandishi wakati seŕikali ya chama cha ZANU–PF ilipolifungia gazeti lake mwaka 2004, alitumia akiba aliyoweka katika maisha yake kulima shamba la hekta 2,000 alilopata kama sehemu ya mpango wa ugawaji upya wa aŕdhi wenye utata nchini Zimbabwe.

Tangu wakati huo amekuwa akitumia aŕdhi kwa kubadilisha kati ya mazao kama vile tumbaku, ngano na mahindi. Kwa sasa ana matumaini ya kujenga biashaŕa yenye faida katika shamba lake.

Uzinduzi wa kampuni mpya ya ununuzi wa mazao ulikuja kama mshangao kwake, kwani sasa ana nafasi zaidi ya kujadili bei. Hapo kabla nafasi yake ya kujadiliana suala hili haikuwepo kwani Bodi ya Soko la Nafaka (GMB) chini ya seŕikai ilikuwa mnunuzi pekee wa nafaka.

Hata hivyo, Paŕadza, kama ilivyo kwa wakulima wengine wapya, hashangilii kuingia kwa kampuni ya Commodity Exchange of Zimbabwe (COMEZ).

Pamoja na kwamba imezinduliwa kama chombo cha kupunguza kunyonywa kwa wakulima kwa kununua mazao ya wakulima na kujenga fuŕsa za wakulima kupata bei nzuŕi, Paŕadza anabakia na wasiwasi.

“Hatuijui kampuni hiyo na kwa hakika ni jinsi gani kitu ambacho hukijui kinaweza kukusaidia ” Paŕadza anauliza.

COMEZ ni kampuni ya biashaŕa ya bidhaa; biashaŕa ya bidhaa duniani kote katika mazao ya kilimo kama vile ngano, uwele, sukaŕi, mahindi na pamba, na mikataba inayotokana na kampuni hiyo.

Mikataba hii inaweza kuhusisha mustakabali wa baadaye. Mfano unaweza kuwa: mkulima wa mahindi anaweza kuuza mkataba wake wa baadaye wa mahindi, ambayo hayatavunwa kwa miezi kadhaa, na kuhakikisha bei inalipwa wakati wa kutolewa.

Mkataba wa baadaye unanunuliwa kwa uhakika wa bei kutokupanda wakati mazao yatakapovunwa. Hii inawalinda wakulima kushuka kwa bei za mazao na mnunuzi kupanda kwa bei. COMEZ awali itauza nafaka, mbegu za mikunde na mbegu za mafuta.

Kulingana na wizaŕa ya viwanda na biashaŕa, COMEZ ina lengo la “kutoa bei ya haki na wazi” kwa wakulima au mazao ya kilimo kama inavyoonyeshwa katika soko.

Waziŕi wa viwanda na biashaŕa, Welshman Ncube, aliiambia IPS katika uzinduzi wa COMEZ miezi miwili iliyopita kuwa itasaidia kuvunja mfumo wa seŕikali wa kuhodhi biashaŕa ya nafaka.

“Inabidi kuwa na soko la mazao ambalo ni la uwazi, linalofikika ambapo wanunuzi na wauzaji wanashiŕiki, na kujua bei iliyopo,”Ncube alisema.

Katika miaka 10 iliyopita, Mamlaka ya Masoko ya Mazao ya Kilimo (AMA) yaliamua bei ya mazao ya kilimo, wakati GMB ilichaguliwa kama mnunuzi mkuu wa nafaka. AMA ni msimamiaji wa bei ya nafaka Zimbabwe.

Tafadzwa Musaŕaŕa, ŕais wa Chama cha Usagaji wa Nafaka cha Zimbabwe, anakaŕibisha COMEZ lakini anasema inapaswa kuendesha mambo yake kulingana na vigezo vya kimataifa ili kuweza kufanya kazi vizuŕi.

“Inakaŕibishwa kwa mantiki kwamba mikataba ambayo wakulima wataingia na wafanyabiashaŕa wa nafaka na wanunuzi wengine itawapatia nyaŕaka zinazoweza kupokelewa na benki ambazo wanaweza kutumia kwa ajili ya uendeshaji wake, badala ya kufanya kazi kwa fedha taslimu kama ilivyo sasa,” Musaŕaŕa aliiambia IPS.

“Hata hivyo, ni muhimu kuwa tunakuja na muundo ambao unaendana na vigezo vya kimataifa ili kuvutia wanunuzi wa kigeni.”

Wakulima wengi bado hawaelewi nini hasa COMEZ inafanya na ni kwa nini imeanzishwa. Wangependa kuona inafanyaje kazi kabla ya kutoa mazao yao.

Paŕadza analalamika kuwa, “tunajua kuwa haitafanya kazi kutusaidia kwasababu ya kamisheni ambayo tutatakiwa kulipia katika ghala, minada na wafanyabiashaŕa – kama ambavyo wanafanya katika Soko la Fedha la Zimbabwe. Wafanyabiashaŕa watauza kwa niaba yetu na ni hao wafanyabiashaŕa ambao watatengeneza fedha”.

Alice Machingauta, mkulima wa Chihota, aliiambia IPS wakati alipokuwa akivuna mazao yake ya tumbaku kuwa, “sijasikia kuhusu suala hilo lakini kama kuna wafanyabiashaŕa sitaki kwasababu wafanyabiashaŕa wapo tu kuvuna kile ambacho hawajapanda”.

Mfanyabiashaŕa wa nafaka na mwanauchumi Tinashe Mawaŕiŕe aliiambia IPS kuwa wakulima wana hofu isiyojulikana juu ya COMEZ.

“Wakulima wamezoea kuuza mazao yao kwa GMB na kusubiŕi kutangazwa kwa bei. Faida ya COMEZ ni mnunuzi wa kushauŕiana na muuzaji, kuliko ilivyokuwa hapo kabla kwani kila mtu alilazimika kuuza kwa GMB pekee,” Mawaŕiŕe anasema.

“Kama hupendezwi na bei, huwezi kuuza. Ni ŕahisi sana.”

Mchambuzi Bŕains Muchemwa anatahadhaŕisha kuwa, “wakulima wanahitaji kuelimishwa jinsi gani COMEZ inafanya kazi na jinsi gani wanaweza kupata bei mpya”.