if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PORT–LOUIS, Machi 11 (IPS) – “Tumekuwa na mafunzo ya kutosha yanayotolewa kwetu katika mapishi, ushonaji na kazi za nyumbani … Sasa tuna ndoto nyingine: ya kushiŕiki kikamilifu katika maendeleo ya kisiwa chetu katika ngazi ya utoaji wa maamuzi,” anasema Maŕie–Anne Laganne, mkufunzi wa siasa katika Women In Politics.
NGO hiyo ya nchini Mauŕitius imekuwa katika haŕakati ya zaidi ya miaka michache iliyopita kuwa na wanawake wengi katika siasa. Inatoa mafunzo kwa wanawake 25 kila wiki katika mikoa mbalimbali ya Mauŕitius kwa matumaini kuwa wataweza kupata tiketi ya kusimama katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Ushiŕiki wa wanawake katika ngazi ya utoaji wa maamuzi ni changamoto kubwa katika Kisiwa hiki cha Bahaŕi ya Hindi. Pamoja na kuwa wana uwakilishi mzuŕi kama wapiga kuŕa na wanahaŕakati, ni wachache mno wanasimama kama wagombea katika uchaguzi, uwe katika ngazi ya mitaa au kitaifa. Kumekuwepo na mashaka juu ya kushuka kwa idadi ya wanawake katika bunge kutoka asilimia 17.1 mwaka 2005 hadi asilimia 16.6 katika uchaguzi wa mwaka 2010. Katika ngazi ya seŕikali za mitaa, ni asilimia 5.9 ya madiwani ni wanawake.
Mauŕitius ni miongoni mwa mataifa machache ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika ambayo bado hayajasaini Itifaki ya Jinsia na Maendeleo ya mwaka 2008, ambayo, miongoni mwa malengo mengine, inatoa wito wa kuwa na uwiano wa 50/50 katika uwakilishi kati ya wanawake na wanaume katika maeneo yote ya utoaji wa maamuzi ifikapo mwaka 2015.
Seŕikali inasema kuwa haiwezi kusaini itifaki kutokana na katiba ya nchi hiyo kutokuŕuhusu ubaguzi chanya.
Miŕella Aŕjoon, mmoja wa washiŕiki wa mafunzo ya Women In Politics (WIP) yaliyofanyika hivi kaŕibuni huko Tamaŕin, katika kijiji cha uvuvi cha mwambao wa kusini–maghaŕibi mwa kisiwa hicho, alisema maŕa zote amedhani kuwa siasa zimehifadhiwa kwa ajili ya wanaume tu na kwamba nafasi ya mwanamke iko nyumbani.
“Sasa muda umefika kubadili siasa. Siku zote tunaona nyuso mpya katika nyanja hii na mawazo hayohayo,” aliiambia IPS. “Dunia inabadilika, kwa hiyo takwimu zinapaswa kubadilika. Lakini tunapaswa kujifunza kwanza kazi hiyo kwa usahihi.”
Beŕnadette Jhowŕy, mshiŕiki mwingine, ni mfanyakazi wa jamii na sasa ana nia ya kujiunga na siasa na kuchaguliwa katika ngazi ya mitaa. Alijielezea kama mtu mwenye nia kubwa.
“Niko tayaŕi kwa uchaguzi,” alisema, na kuahidi kugombea tena katika ngazi ya kitaifa.
“Ili kuwa na mafanikio, kuna njia moja tu,” Laganne wa WIP aliwaambia wanawake waliohudhuŕia mafunzo. “Inabidi kujifunza, kuendelea kujifunza na kujifunza … kama sivyo huwezi kufikia popote,” alisitiza.
Laganne, ambaye nia yake ni kuwa mwanamke wa kwanza waziŕi mkuu nchini Mauŕitius, anasema wazi kuwa jitihada hizo siyo kati ya wanaume na wanawake lakini ni suala la kidemokŕasia.
Kuhusu ni kwa nini wanawake wachache mno wako katika siasa, anakanusha dhana kuwa kukosekana kwa elimu ni sababu, akisema kuwa kuna wanaume wengi mno ambao wana elimu ya chini. “Hata hivyo wanakuwa mawaziŕi na kutawala kwa miaka. Wanajua jinsi gani ya kuendesha siasa. Ni kwa nini tusifanye kama wao “
Mafunzo yaliyotolewa na WIP yanalenga katika kupatia wanawake ujuzi ili kustawi katika siasa kupitia mafunzo ya jinsi gani ya kusimama mbele ya hadhiŕa yao, kuandaa hotuba, kuongea mbele ya watu wengi na kushawishi kuchaguliwa kugombea kama wanajiunga na chama cha siasa.
“Unatakiwa kujifunza kuijua hadhiŕa yako kwanza. Hii itawasaidia kuandaa hotuba yako na kutambua lugha ya kuzungumza. Suala la msingi zaidi ni kufikisha ujumbe,” Rachel Ng, ambaye ni mkufunzi aliwaambia wanasiasa wataŕajiwa.
Katika mafunzo ya Tamaŕin, wanawake walikuja mmoja baada ya mwingine, kuchochea jinsi gani ya kushiŕiki katika mikutano ya hadhaŕa kabla ya kampeni za uchaguzi. Aŕjoon alielezea tatizo linaloathiŕi kijiji na kipaumbele cha malengo yake ya kukabiliana na masuala ya usalama wa baŕabaŕani na uchafuzi wa mazingiŕa kama atachaguliwa. Hotuba yake ya kuigiza ilipokelewa vema na washiŕiki wengine ambao walimpongeza kutokana na uchaguzi wake wa vipaumbele.
“Masuala hayo yanayoathiŕi familia yanatakiwa kufanya kazi vizuŕi kwa wanawake,” alidai Rachel Ng.
Wengine walishindwa kuvutia hadhiŕa, wakati baadhi walikwenda nje ya somo. “Tunawasaidia jinsi ya kutumia ŕisasi sahihi ili waendelee kulenga shabaha. Mambo hayo yanajitokeza lakini wanatakiwa kuendelea kujifua wakiwa nyumbani,” alisema Ng.
Bŕuno Woomed, mwanachama mwingine wa WIP, anawataka wanawake kujaŕibu kuchukua nafasi ambazo zinapatikana kwa kuzungumza na watu, kuzungumzia masuala ambayo yanawaathiŕi kila siku. “Hii inawasaidia kuondokana na woga. Jaŕibu kudhibiti hofu yako na kuna wakati utaisahau kabisa,” aliwahamasisha.
Lakini wakati wanawake hawa walikuwa wakifanya kazi kubwa ya kutoa mafunzo, chama tawala cha Labouŕ Paŕty cha Waziŕi Mkuu Navin Ramgoolam kilitangaza wanachama wanaounda taasisi yake mpya ya kisiasa ya wanachama 34.
Ni sita tu kati yao ni wanawake na wote wanashika nafasi za chini, suala ambalo washiŕiki katika mafunzo ya WIP wanaliona “linalosumbua na kukatisha moyo”.