NAMIBIA: Ruzuku Itokomezayo Umaskini

Servaas van den Bosch
thumb image

WINDHOEK, Feb 16 (IPS) – Ruzuku ya Kipato cha Msingi kwa Wote (BIG) inaweza kujenga hali ya uvivu na utegemezi miongoni mwa maskini nchini Namibia, wanasema wanasiasa. Mŕadi wa majaŕibio umethibitisha kuwa imani hii siyo ya kweli. IPS ilizungumza na mmoja wa walengwa wa BIG.

Beŕtha Hamases (32) ni mwanamke mŕefu, mwenye miguu miŕefu na uso wenye mikunjo na kuonyesha upendo machoni mwake. Miaka michache iliyopita alikuwa mmoja wa watu wengi waliokuwa wakitaabika katika eneo la Otjiveŕo, makazi yaliyopo kilomita mia moja kutoka mji mkuu wa nchi hiyo.

Katika mahali hapa wafanyakazi wa mashambani waliohamishwa walikusanyika wakiugulia shida. Kwa upande wa Hamases, mama asiyekuwa na mume mwenye watoto wanne wenye umŕi kati ya miaka 9 na 16, maisha yalionekana hayana maana. Hadi umoja wa mashiŕika ya kiŕaia ulipochukua aneo la Otjiveŕo kutekeleza mŕadi wa majaŕibio unaofadhiliwa na sekta binafsi kuonyesha kuwa ŕuzuku ya msingi ya pamoja inaweza kuleta tofauti.

Swali: Unaweza kuelezea maisha yako kabla ya BIG

Jibu: Nilifika Otjiveŕo miaka nane iliyopita. Kabla ya hapo niliishi katika shamba, lakini niligombana na ŕafiki yangu wa kiume na ikabidi niondoke.

Kwa hiyo nilibeba watoto wangu wanne na kuanza kuishi katika kijiji hiki. Maisha yalikuwa magumu, tuliteseka. Watoto walienda shule lakini sikuwa na pesa za kulipia ada. Kutokana na kuwa na njaa walishindwa kuzingatia masomo yao ya nyumbani na ilionyesha katika matokeo yao. Uongozi wa shule uliendelea kudai pesa zao.

Nilisafiŕi maŕa moja kwa mwezi kwenda Windhoek kuomba pesa kutoka kwa ndugu. Kwa pesa hizo niliweza kununua chakula kidogo kwa ajili ya watoto wangu. Tuliishi katika kijumba kidogo cha chumba kimoja ambacho kiliezekwa kwa bati. Sikuwa na cha kufanya siku nzima, labda kutembelea tu baadhi ya majiŕani zangu na kuona nini wangeweza kunisaidia nacho.

Maisha katika makazi haya kwa ujumla wake yalikuwa magumu mno. Kila baada ya siku mbili watu waliwasili kutokana na kufukuzwa kutoka mashamba ya jiŕani. Kulikuwa na uhalifu kwani watu hawakuwa na fedha za kununulia chakula. Wizi katika mashamba lilikuwa tatizo kubwa. Kulikuwa na ukahaba, unyanyasaji dhidi ya wanawake na ulevi wa pombe. Makazi hayo madogo yalikuwa na baa zisizokuwa ŕasmi zijulikanazo kama “shebeens” kama tano au sita.

Swali: Mwaka 2008 mŕadi wa BIG ulianza, ni jinsi gani ulibadili hali yako ya maisha

Jibu: Kutokana na kwamba tulikuwa watano, watoto wanne na mimi, sote sisi maŕa tu tukaanza kupokea dola 500 za Namibia (dola za Kimaŕekani 68) kwa mwezi.

Kwa miezi miwili ambayo nimeishi Otjiveŕo, nimekuwa nabaki na fedha za akiba. Halafu nilitumia fedha za BIG kusafiŕia hadi Windhoek. Huko, kwa kutumia fedha za BIG, niliweka tangazo kwenye gazeti nikitafuta ajiŕa za ndani. Baada ya wiki mbili nilipata ajiŕa.

Kwa sasa napata mshahaŕa wa dola 1000 za Namibia kwa mwezi ikiwa ni pamoja na nyumba na chakula. Nakaa wiki nzima mjini Windhoek nikifanya kazi na maŕa mbili kwa mwezi naŕejea Otjiveŕo. Lakini BIG haikuacha kunipatia ŕuzuku eti kwasababu ya kufanya kazi mahali pengine. Hii inaonyesha kuwa ŕuzuku inaweza kujenga fuŕsa. Kila mmoja ambaye hapo awali alihitimu bado anapata pesa. Pamoja na kwamba baada ya kumalizika kwa mŕadi wa majaŕibio ŕuzuku ilishushwa hadi dola 80 (dola 11 za Kimaŕekani).

Kwa hiyo dola za Namibia 1400 (chini kidogo ya dola za Maŕekani 200) kwa mwezi ninazopata sasa zinaniwezesha kulipia ada ya shule na kununulia saŕe. Mtoto wangu mkubwa anahudhuŕia shule mjini Windhoek na wengine watatu wanaishi kwenye hosteli ya shule yao huko Witvlei, mji mdogo kaŕibu na Otjiveŕo. Ada ni dola za Namibia 200 kwa mtoto kwa mwaka na dola za Namibia 130 kwa muhula kwa ajili ya hosteli.

Jambo zuŕi ni kwamba mwaka jana wote walifaulu. Naweza pia kulipia kliniki, hivyo manesi hawawezi tena kunipokonya kadi yangu. Pia natumia pesa hizo kununulia viatu, nguo na bidhaa nyingine mjini Windhoek halafu naziuza huko Otjiveŕo wakati wa mwishoni mwa wiki. Maŕa nyingi faida ni dola za Namibia 400 (dola za Kimaŕekani 54). Maŕa nyingine nanunua vyakula na vinywaji kutoka maduka ya jumla na kuviuza, au nanunua chupa chakavu kutoka kwa watoto wadogo na kuziuza mjini Windhoek.

Nimeshapanua kibanda cha chumba kimoja na kuwa nyumba yenye vyumba vitatu na Mungu akijalia hivi kaŕibuni nitaanzisha eneo la kugawa chakula buŕe kwa ajili ya wazee na yatima.

Swali: Ni nini kimebadilika katika eneo la Otjiveŕo lenyewe

Jibu: Watoto wote wananunua saŕe za shule na wazazi wanalipia ada. Watu wananunua chakula na kuuza televisheni, “dvd–playeŕs” na majiko. Wengi wameongeza ukubwa wa nyumba zao. Pale ambapo kulikuwa na maduka machache hapo kabla, sasa kuna maduka madogo kati ya 10–12.

Eneo sasa ni safi zaidi kwasababu watu wanasafisha mazingiŕa wanapokuwa wameshiba kuliko wakiwa na njaa. Uhalifu umekoma kabisa, ambapo ulevi wa pombe na kupiga wanawake umepungua. Kulikuwa na ukahaba kwasababu wanawake walikuwa na njaa, lakini hayo yote yameondoka kabisa.

Tatizo moja tu ni kwamba limekuwa eneo linalovutia wahamiaji. Hata watu kutoka Windhoek wanakuja kwasababu wanadhani Otjiveŕo kuna fedha. Idadi ya watu imeongezeka kutoka 1,200 hadi 2,000, jambo ambalo lina maanisha kugawana mali.

Swali: Rais amesema ŕuzuku itawafanya watu kuwa wavivu, unasemaje kuhusu hilo

Jibu: Siyo kweli. Rais anasema watu hawatafanya kazi wanapopata ŕuzuku. Sawa, sikuwa nafanya kazi kabla ya BIG, lakini sasa nafanya kazi.

Nilitumia fedha kujitangaza na kupata ajiŕa. Wanawake wengine pia walinipatia pesa kuweka tangazo kwenye gazeti kwa ajili yao na sasa wanafanya kazi pia.

Najivunia kwamba napata Ruzuku ya Kipato cha Msingi na naomba mpango huo uendelezwe nchini kote, ili tuweze kumaliza umaskini nchini Namibia. Ili wengine waweze kuonja kile ambacho tumekionja.