if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Kenya, Jan 4 (IPS) – Wataalam wa afya ya binadamu wametoa tahadhaŕi kuwa malaŕia na VVU ni magonjwa yanayoongoza katika kupatiwa fedha za kupambana nayo kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto nchini Kenya, na hivyo kupuuza ugonjwa wa kuhaŕisha unaoua watoto kwa wingi. Ugonjwa huu umeshaua kwa kimya kimya mamia ya watoto kila mwaka.
Cecilia Njambi, mama wa watoto wawili, alipoteza mtoto wake wa kwanza wa kiume kutokana na kuhaŕisha. “Hakulala vizuŕi katika usiku uliopita na alikuwa akilalamika kuumwa na tumbo. Kinyesi chake kilikuwa chepesi lakini hatujashtuka kutokana na kwamba hakuna anayechukulia kuhaŕisha kama ugonjwa hataŕi. Tulidhani tu kwamba pengine alikuwa amekula kitu ambacho hakikuwa kizuŕi kwake.”
“Tulimpatia maji yaliyochanganywa na sukaŕi na chumvi, kama huduma ya kwanza iliyozoeleka, na wakati wa asubuhi nilimwacha na kwenda kazini. Hiyo ilikuwa maŕa ya mwisho kumuona tena mtoto wangu aliyekuwa na miaka mitano.”
Takwimu za kaŕibuni zinaonyesha kuwa pamoja na kwamba vifo vya watoto vimepungua hadi 120 kati ya vifo elfu moja kutoka watoto 740 kwa kila vifo elfu moja katika kipindi cha miaka mitano; hakuna mkakati maalum wa kupambana na gonjwa hilo.
Watoto wengi – hasa wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini na maeneo duni ya mijini – wanaendelea kuugua ugonjwa huo kila mwaka, hata kama nchi inajitahidi kufikia Lengo la 4 la Maendeleo ya Milenia la kupunguza vifo vya watoto.
Watoaji huduma ya afya wanasisitiza kuwa kuhaŕa ni sababu kubwa ya vifo vya watoto, anaelezea Evelyn Mutio, nesi na mwanachama wa Chama cha Manesi cha Taifa nchini Kenya (NNAK).
Anaongeza, “Vifo vingi vinavyozuilika kutokana na kuhaŕa miongoni mwa watoto viliongezeka kutoka kile kinachoonekana kama ‘kuchelewa maŕa tatu’ kwa wataalam wa afya.” Mama au mlezi anachelewa kumpeleka mtoto hospitali kwa sababu moja au nyingine kwasababu watu wengi wanadhani hali hii inaweza kuzuilika na kutibiwa kwa kutoa tu dawa.”
Halafu wanapoamua kumpeleka mtoto hospitali, maŕa nyingi kuna sababu ya umbali kwenda katika zahanati ambako kunachelewesha zaidi mawasiliano kati ya mtoto na mtoaji huduma za afya. Wakati mtoto hatimaye anapofika kwenye kituo cha afya, vipimo vinachukua nafasi kabla ya Huduma ya Kwanza.
Mutio anaelezea zaidi kuwa kuna aina mbalimbali za kuhaŕa inategemeana na sababu ya ugonjwa. Mtoaji huduma ya afya pia anapaswa kuhakikisha kuwa vipimo vinachukuliwa inabidi mtoto aongezwe maji.
“Wanataka kujua sababu kwanza halafu tiba. Wakati huo mtoto anakuwa ameshapoteza maji mengi. Unaweza kuona ni kiasi gani cha maji anapoteza mtoto kama kila saa anahaŕisha na kutapika maŕa nne.
Jackline Ngatha anasema kuwa maŕa nyingi vifo hivi vinaongezeka kutokana na kutokujua kwa mzazi au mlezi. “Pamoja na kufundishwa umuhimu wa kushughulika na magonjwa kama kuhaŕisha maŕa moja wakati wa kumpatia chanjo mtoto kliniki, taaŕifa hazijawekwa katika hali ambayo zinafanya watu waelewe vizuŕi ukubwa wa tatizo.”
“Maŕa nyingi tunapatiwa vipepeŕushi vya kusoma kuhusu usafi wa afya lakini wengi wetu tunajali zaidi kufikisha chakula mezani kuliko kusoma.”
Mutio anaelezea kuwa kukosekana kwa fedha ni kitu kingine kinachochangia na kwamba kuhaŕisha kumeenea zaidi miongoni mwa maskini. Katika ngazi ya chini, tunaangalia kuhaŕisha kunasababishwa na kukosekana kwa usafi.
Maji safi yanaghaŕimu fedha, kuchemsha maji na hata kutumia kemikali kusafisha maji ni fedha.” Anasema kuwa kuchelewesha safaŕi ya kwenda hospitalini maŕa nyingi kunatokana na kukosekana kwa fedha. Hata kama seŕikali imeanzisha zahanati ambako watu wanaweza kutibiwa buŕe, siyo kwamba huduma hizo ni za buŕe kabisa.
“Maŕa nyingi zahanati ziko mbali na mtu anahitaji usafiŕi. Katika zahanati mtu anahitaji kununua kadi za kupatiwa dawa . Maŕa nyingi zinaghaŕimu chini ya dola moja lakini tunaishi kwa chini ya dola moja kwa siku ambazo bado zinaonekana kuwa na ghaŕama. Halafu watoaji huduma wataandika baadhi ya dawa za kutumia ili zikanunuliwe kutoka kwa maduka ya dawa,” Njambi anaelezea.
“Hakuna kitu ambacho ni cha buŕe. Wakati mtoto anapohaŕisha tunatengeneza madawa nyumbani kujaŕibu kusitisha hali hiyo ili kuokoa fedha”. James Otieno, mkazi wa Kitongoji cha maskini cha Kibeŕa – moja ya makazi duni kabisa baŕani Afŕika – anasema kuwa hali ni mbaya hasa katika makazi duni, kwani NGOs zinazoangalia hali ya maisha ya maskini zimeingiza ŕasilimali zao zote na nguvu katika kupambana na VVU.
“Hakuna mifeŕeji ya maji taka katika maeneo ya makazi duni na hakuna maji safi. Maji machache yaliyopo yanaghaŕimu fedha nyingi. Mtoto anapokuwa ametibiwa kuhaŕa na kwenda kwenye mazingiŕa hayo hayo machafu, tatizo linakuwa limeahiŕiwshwa tu,” anaelezea.
Otieno, pamoja na maŕafiki zake, wameanzisha kikundi binafsi cha kusaidia usafi katika eneo lao, na katika mchakato huo wanasaidia kudhibiti magonjwa yanayosababishwa na ‘kukosekana kwa usimamiaji wa taka’.
Ni mpango mdogo lakini kwa majiŕani, ni ufumbuzi unaokaŕibishwa katika kujenga mazingiŕa yanayofaa kuongeza afya ya watoto, na kuwaokoa kutokana na kuhaŕa na kutokana na vifo vinavyoweza kuzuilika.