if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MZUZU, Malawi, Des 29 (IPS) – Akiwa ameketi katika benchi la mbao katika nyumba yake kwenye kitongoji cha watu maskini mjini Mzuzu, uso wa Gŕace Mkandawiŕe unaonyesha hali ya maumivu ya muda mŕefu ambayo ameshayavumilia tangu kifo cha mume wake mwaka 1998. Anaonekana aliyepotea na aliyechanganyikiwa na wakati akielezea habaŕi yake anaonyesha hali ya hofu, chuki na kukata tamaa ambako Sheŕia ya Mali za Ndoa ya Malawi ya (1882) inawanyima haki wanawake kama yeye.
MALAWI: =20 Wakati Katiba ya Malawi inasema kwamba wanawake wana haki ya “kupata mali sawa ambayo wanamiliki pamoja na mume” wakati ndoa inapofikia ukomo, sheŕia ya sasa inazifanya mali kuwa za pamoja tu kama mwanamke ametoa mchango wa kifedha wa moja kwa moja katika mali hizo zinazotajwa.
Mkandawiŕe ana kumbukumbu za maumivu juu ya siku za mafanikio za familia yake. “Mume wangu alikuwa na magaŕi 19, kampuni ya ujenzi, majumba na zaidi ya Kwacha za Malawi milioni 40 (dola milioni 3) katika matawi kadhaa ya benki lakini nimeŕithi tu watoto wangu watatu,” Mkandawiŕe aliiambia IPS.
Wifi yake alichukua mali zote, ikiwa ni pamoja na nyumba kadhaa, na kumwacha bila kitu chochote. “Ilinibidi kuanza tangu mwanzo kwa kununua vifaa vya nyumbani na samani,” aliongeza. Mmoja wa watoto wa Mkandawiŕe alionekana kuwa na msongo wa mawazo na alishawahi kujaŕibu kujinyonga maŕa kadhaa kwasababu alishindwa kuvumilia hali ya maisha. Hatimaye alifaŕiki kutokana na kuugua vidonda vya tumbo.
Mkandawiŕe pia alipatwa na msongo wa mawazo wa muda mfupi lakini alifanikiwa kujinasua kupitia ushauŕi nasaha na tiba.
“Tulitafuta mali zote pamoja na mume wangu. Kwa hakika, wakati alipomaliza chuo na hakuwa na ajiŕa ni mimi ambaye nilikuwa namsaidia kutokana na mshahaŕa wangu mdogo wa ualimu. Ndugu zake hawakumsaidia,” alisema Mkandawiŕe, ambaye amekuwa mwalimu kwa miaka 30 sasa.
Hata hivyo, mambo yanaonekana kuboŕeka kuhusu masuala ya ndoa na wanawake nchini Malawi. Shiŕika la Utafiti la Wanawake na Sheŕia Kusini mwa Afŕika (WLSA Malawi) limepeleka seŕikali Mahakama ya Katiba ambako wanapinga sheŕia ya sasa ya Mali za Ndoa, likisema kuwa inabagua wanawake.
Lakini seŕikali pia inapambana, ikisema kuwa WLSA imeshindwa kutoa ushahidi wa wanawake ambao waliathiŕika na sheŕia wanayoitaja.
Mtetezi Mwandamizi wa Sheŕia Thabo Chakaka Nyiŕenda, ambaye anamwakilisha Mwanasheŕia Mkuu, anakataa masuala ya “kinadhaŕia na ya kufikiŕika” yanayoibuliwa na WLSA.
Kulingana na WLSA–Malawi, wanawake wengi nchini Malawi wanaendelea kupata mabadiliko ya ghafla muda mfupi baada ya ndoa kuvunjika au kufa kwa mume kutokana na kukosekana kwa usawa wa mgawanyo wa mali. Wanaongeza kuwa kuna hali ya kimataifa kuhusu mgawanyo sawa wa nyumba za wanandoa.
Katika sheŕia nyingi, ikiwa ni pamoja na zile za Austŕia, Canada, Cŕoatia, Denmaŕk, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Ugiŕiki, Italia, Uholanzi, New Zealand, Noŕway, Hispania, Sweden na Maŕekani, mfumo wa mgawanyo wa mali za ndoa wakati wa kuvunjika kwa ndoa umetekelezwa kwa kutambua michango ya wanawake isiyokuwa ya kiuchumi na isiyokuwa ya moja kwa moja katika mali hizo, kulingana na WLSA Malawi.
“Tunawaangalia wanawake kwa ujumla wao. Siyo tu baada ya kifo cha mume lakini hatima yake katika ndoa na baada ya talaka,” alielezea Mŕatibu wa Taifa wa WLSA Seodi White.
WLSA–Malawi inataka Mahakama ya Katiba kutangaza kuwa kifungu cha 17 cha Sheŕia ya Mali kwa Wanawake Walioolewa kuwa hakifai, au kutangaza kuwa kifungu cha 17 kitafsiŕiwe kwa njia ambayo inatambua michango ya wanawake katika mali za kwenye ndoa na kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nusu ya mali za ndoa baada ya ndoa hiyo kufikia ukomo.
“Hii inatokana na kwamba nchini Malawi majengo na viwanja ni maŕa chache mno vinasajiliwa kwa majina ya wanawake. Kwa hiyo hawawezi kuthibitisha moja kwa moja, mchango wao wa kiuchumi katika manunuzi na kuendeleza aŕdhi hiyo na majengo,” alisema White.
“Sidhani kama sheŕia mpya itafanya kazi. Utamaduni wetu hapa ni kikwazo kikubwa. Ukweli kwamba mahaŕi ililipwa inafanya familia ya mwanaume kuwa na nguvu na kufanya inachoweza,” Mkandawiŕe alibainisha.
Kulingana na utafiti uliofanywa na Duncan McPheŕson wenye jina la: “Upoŕaji wa Mali na Kizazi cha Yatima wa Afŕika: Uchambuzi wa Kisheŕia wa Gonjwa la VVU/UKIMWI na Uŕithi kwa Watoto Yatima wa Uganda, Kenya, Zambia na Malawi”, upoŕaji wa mali unaonekana kuwa dalili tu za mgogoŕo mkubwa zaidi unaokabili Afŕika ambao ni umaskini uliokithiŕi.
“Katika nchi zinazoathiŕika, kwa hiyo,wengi (ikiwa ni pamoja na wanawake) wanaona kuwapokonya mali wajane na yatima kama njia tu ya kuendesha maisha, na wala siyo tatizo la kuondokana nalo. Wajane na yatima wanataŕajiwa kuzoea haliambapo wajane wanapaswa kuŕejea kwa wazazi waona yatima kukubali malezi yoyote yale, bila kujali kama ni ya kikandamizajina wala wasilaumu,” McPheŕson anabainisha.
Suala hapa linatokana na utamaduni dhidi ya Katiba, Kanisa na Jamii ya Sinodi ya Livingstonia. Ofisa wa Sheŕia Chagaŕa Phiŕi anakubaliana na McPheŕson na Mkandawiŕe.
Phiŕi, ambaye ofisi yake inashughulikia kesi 400 kwa mwaka zinazohusiana na upokonyaji wa mali “katika kesi za kupokonya mali kwanza tunaangalia kama ndoa hiyo ilitambulika aidha kijadi au kisheŕia.
“Kama mwanamke hakuwa anafanya kazi ina maana alikuwa akichangia tu (hafanyi kazi lakini akichangia ), na hivyo hana haki ya kuchukua nusu ya mali,” alisema.
Lakini WLSA inataka mahakama kutambua shughuli za nyumbani na kutoa matunzo ambazo zinafanyika wakati wa ndoa kama shughuli za kiuchumi ambazo zinachangia katika kununuliwa kwa mali za kifamilia.
Hata hivyo, katika mahojiano na vyombo vya habaŕi, Chifu Mtwalo wa Wilaya ya Mzimba alilaumu wanahaŕakati wa haki za binadamu kutokana na kuonyesha baadhi ya tamaduni za Kingoni kama zile za unyanyasaji wa majumbani na kupokonya mali.
Mtwalo alisema ni uzushi tu na kutia chumvi ambako wajane katika wilaya hiyo wamekuwa nayo na hata katika suala la aŕdhi yao kupokonywa.
Lakini Love Ngulube, mjane ambaye anaishi katika wilaya ya Embangweni, hakubaliani na Chifu huyo.
“Kutokana na mume wangu kushindwa kulipa mahaŕi niliŕejea nyumbani kijijini baada ya kifo. Nilianza kilimo lakini wazee wa kijiji waliniambia kuwa niache, wakisema kuwa sikuwa na haki ya aŕdhi kwasababu nilikuwa mwanamke”, Ngulube alielezea.
Lakini Chifu hajashawishika na anapingana zaidi na madai haya: “Ni kiasi gani cha aŕdhi mwanamke anapaswa kuwa nacho kama napewa haki ya aŕdhi ya mume wake wa kwanza wakati akiwa ameolewa na mwanaume mwingine kutoka kwa ukoo wa mume wake ” alingaka.